Posts

Showing posts from June 18, 2012

WAKULIMA WA TUMBAKU WAHIMIZWA KUSHIRIKI SENSA

Image
Wakulima wa Tumbaku wilayani Singida, wamekumbushwa kujitokeza kushiriki sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agost 26, mwaka huu. Wito huo  ulitolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Fatma Toufiq, alipozungumza na wakulima pamoja na wakazi wa kijiji cha Mitundu. Alisema sensa hiyo inalenga kupata idadi ya watu waliopo ili kufahamu shughuli za kiuchumi, kielimu na kiundombinu kwa lengo la kupanga maendeleo ya nchi na watu wake. “Sensa ni muhimu na inawezesha kufahamu idadi ya watu katika maeneo yetu ili kufahamu shughuli zao za kiuchumi, kielimu na miundombinu ili tupannge maendeleo” alisema Toufiq. Toufiq alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi wilayani Singida, kujitokeza kwa wingi pindi muda utakapofika ili kila mmoja ahesabiwe kwa faida yake na taifa. Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha Wakulima wa tumbaku (CETCU), kanda ya kati Yassin Dagaki, akitoa taarifa ya maendeleo ya kilimo cha zao hilo , alisema msimu wa mwaka 2009/2010 uzalishaji uliongezeka kwa was

RWANDA YAZIFUNGA MAHAKAMA ZA ZILIZOANZISHWA KUSHUGULIKIA KESI YA MAUAJI YA KIMBARI

Image

WAKUFUNZI WA SENSA WAPIGWA MSASA

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi   ya Taifa ya Takwimu Dkt   Albina Chuwa akitoa ufafanuzi kwa wakufunzi wa Sensa   kwa ngazi ya kitaifa jana mjini Dodoma. Wakufunzi   hao wanaandaliwa kwa ajili ya kwenda katika mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwaelimisha wengi watakaosaidia kufanikisha zoezi la sensa tarehe 26 mwezi Agosti mwaka huu.PICHA NA VICENT TIGANYA WA MAELEZO Baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakiwa watulia kimya kwa dakika mbili kwa ajili ya kuombeleza kifo cha Mhariri wa Jamboleo Willy Edward kilichotokea mjini Morogoro alipokuwa akihudhuria mafunzo ya sense kwa wahariri . Viongozi na wakufunzi hao walikuwa katika mafunzo   ya siku 10 tayari kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za mikoa . Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)yalianza jana mjini Dodoma. Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho akitoa neno la utangulizi kwa   wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakati wa   mafun

BODI YA WATALII WAPONGEZWA

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna Tarish (Kushoto) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania –TTB alipokuwa akifungua kikao cha baraza hilo kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Utalii jijini Dar es salaam hivi karibuni. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki, na kulia ni Katibu wa Baraza hilo Bw Elirehema Maturo. Na: Geofrey Tengeneza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imepongezwa kwa kazi nzuri inayofanya katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na jukumu kubwa la kuitangaza Tanzania kama eneo bora lenye vivutio vingi vya kitalii duniani pamoja na ushindani mkubwa kutoka nchi nyingine na hivyo kufanya idadi ya watalii wanotembelea nchi yetu kuendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka sambamba na kuongezeka kwa pato la Taifa litokanalo na sekta ya utalii. Akifungua kikao cha  Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii hivi karibuni

WAKALI WA DANCERS WASHEREHEKEA MIAKA 4 TANGU KUANZISHWA

Image
SHEREHE za miaka minne ya kundi la Wakali Dancers jana zilifana ndani ya ukumbi wa kisasa wa burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, jijini Dar. Vikundi vya taarab vya Kings, Coast Modern na Kidumbaki kutoka Zanzibar pamoja na Talent Band vilifanya ‘bonge la kufuru’ kwa mashabiki waliofika katika ukumbi huo kwa ajili ya kuburudika wikiendi. Wakali Dancer wakiwa na bendera yenye nembo yao wakati wakisherehekea miaka 4 ya kuanzishwa kundi lao. Kundi la Wakali Dancers likishambulia jukwaa. ...wakizidi kunogesha sherehe hizo. ...wakicheza wimbo wa Thriller ulioimbwa na Michael Jackson. ...wakizidi kupagawisha.

SUPA 5 YAFUNIKA JIJINI ARUSHA

Image
.Mmoja wa wasanii anaeitikisa anga ya muziki wa hip hop nchini,anatamba na tuzo mbili za muziki huo huo huo wa hip hop,Roma akiamsha amsha hadhira kubwa ya watu iliojitokeza jioni ya leo kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel,Airtel Jiunge na Supa5,uliofanyika jana kwenye viwanja vya NMC mjini  Arusha na kuhudhuriwa na umati mkubwa watu. Sehemu ya Wakazi wa Arusha wakishangilia ujio wa huduma mpya ya Airtel Supa5 .Anajiita Mwamba wa Kaskazini,Msanii mwingine mahiri katika miondoko ya muziki wa hip hop nchini,Joe Makini  akitumbuiza kwenye jukwaa jana kwenye viwanja vya NMC jijini Arusha,wakati kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Jiunge na Supa5 kwa wakazi wa Arusha. Wakazi wa jiji la Arusha wakiendelea kuhamia na kujiunga kwa wingi  na Airtel. .Sehemu ya Wakazi wa Arusha wakishangilia ujio wa huduma mpya ya Airtel Supa5 Msanii  mahiri wa muziki wa kizazi kipya kutoka ku

WEMA SEPETU KUMSHUSHA NYOTA WA FILAMU

Image
Nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jalade katika pozi matata Nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jaladekatika kivazi cha ofisini Nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jalade katika kivazi cha kutokea MSHINDI wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, anatarajia kumdondosha nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jalade hapa nchini. Wema Sepetu, ambaye kwa sasa anatamba kwenye tasnia ya filamu anatarajia kumleta Omotola kwa ajili ya kusindikiza uzinduzi wa filamu yake mpya iitwayo Super Star. Filamu hiyo ya Super Star, inazungumzia maisha ya Wema kuanzia utotoni kushiriki kwake Miss Dar Indian Ocean, Miss Kinondoni, Miss Tanzania hadi kuingia kwenye filamu. Kwenye filamu hiyo Wema ameshirikiana na wasanii mbalimbali akiwemo mwimbaji wa Machozi Band, aitwaye Mwinyi. Omotola, ambaye atatua Tanzania wiki hii, alianza kutamba kwenye tasnia hiyo baada ya kutoka na filamu iitwayo Iva mwaka 1993. Hadi sasa nyota huyo amecheza jumla ya filamu 52, zikiwemo, Ties That Bind (20

SEMINA YA VIONGOZI WA KIDINI ZANZIBAR YAFANYIKA LEO

Image
Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa hutuba yake katika ufunguzi wa semina ya siku moja kwa  Viongozi wa kidini katika kukuza dhana ya Utalii kwa wote,iliyofanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo,(kulia) Msahauri wa Rais masuala ya Utalii, Issa Ahmed Othman,na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo, Said Ali Mbarouk,(kushoto) Katibu mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Ali Halil Mirza.   Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa kidini katika kukuza dhana ya Utalii kwa wote,mara baada ya kuifungua semina ya siku moja iliyofanyika leo  katika ukumbi wa Salama Bwawani   Baadhi ya Viongozi wa madhehebu mbali mbali ya kidini wa Mkoa wa Mjini  Magharibi wakisikiliza  kwa makini hotuba ua ufunguzi wa  semina ya siku moja ya Viongozi wa kidini katika kukuza dhana ya Utalii kwa wote,iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mw

EPIC BSS YAMALIZA KAZI MKOA WA DODOMA

Image
Madam Ritah Paulsen akipokea mtoto kutoka kwa  mshiriki huyu aliyekuja nae katika shindano hilo kabla  kuanza kuimba. Mkuu wa kitengo cha mawasiliano  Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa EBSS 2012   Awaichi Mawalla akichangia damu   Na Mwandishi Wetu Dodoma PAZIA la shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) kwa mkoa wa Dodoma limefungwa rasmi huku vipaji kibao vikiwa vimejitokeza na kuwavutia majaji. Kilichovutia zaidi ni washiriki wa miaka 16 ambao walionekana kuimba vema na kuwa kivutio hata kwa washiriki wenzao waliofurika katika ukumbi wa Royal Village. Akizungumzia shindano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo Ritha Paulsen alisema kuwa amevutiwa na wingi wa washiriki mkoani hapa hasa idadi ya washiriki wasichana pia. Alisema kuwa ikiwa ni mara ya kwanza kuruhusu washiriki wa miaka 16 kuingia katika usaili wa EBSS 2012 ameshuhudia hazina kubwa ya vipaji  vya washiriki wa umri huo. Katika

WAFANYAKAZI WA BANK YA UBA WASAIDIA KITUO CHA HOPE FAMILY

Image
Kushoto ni Bw. Rock Meneja mkazi wa benki ya UBA nchini na kushoto ni Victor Meneja wa tawi la benki ya UBA Kariakoo wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakijiandaa pamoja na wafanyakazi wengine wa benki hiyo katika tawi la City Centre Branch Posta,  kwenda Kigamboni ambako walikuwa na mazoezi ya viungo  na baadae walitoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwa ni vyakula mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mbili, katika kituo cha watoto yatima cha cha Hope Family kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Kutoka kulia ni Jack, Marjory, Asha na Natasha wakipozi kwa picha wakati wakijiandaa kwenda kigamboni kwa ajili ya kufanya mazoezi na kutoa msaada katika kituo cha watoto yatima cha Hope Family kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam. Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya UBA wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kwenda kwenye mazoezi Kigamboni jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

MAGAZETI YA LEO

Image
Image
Image

MAHOJIANO YA MO BLOG NA MILLARD AYO

Image
-PIA AMZUNGUMZIA JINSI ALIVYOONDOKA RADIO ONE NA UHUSIANO WAKE NA MKURUGENZI WA ITV/RADIO ONE. SEHEMU YA KWANZA. Kama ilivyo kawaida kwa wataalamu wa masuala ya habari na kijamii wa mtandao wa MO BLOG unaotisha kwa sasa, Mhariri Mkuu wa Mtandao huo Lemmy Hipolite na Meneja Mipango Zainul Mzige ‘hamad’ uso kwa uso na mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni hapa nchini Millard Ayo. LEMMY: Haya ndugu yangu za masiku hatuonani ila mimi nakuona tu kwenye luninga. AYO:  Aiyaa….! Wakuu ni aje ni kitambo kimepita hatujaonana ila mimi niko poa tu nakaza buti. ZAINUL : Usiende mbali tunajua uko bize lakini hebu kaa kitako uzungumze na mhariri wangu kuhusu mawili matatu watu wasio yajua kuhusu wewe. MO BLOG: Nini kimeshawahi kukutokea maishani ambacho huwezi kukisahau na wasikilizaji na watazamaji wako hawakifahamu. MILLARD AYO: Nilishawahi kupata ajali mbaya kiasi kwamba watu wengi wasingekuwa wananifahamu hivi leo. Ni ajali ambayo iliondoka na rafiki zangu wanne

MBUNGE ATOA MSAADA

Image
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji akizungumza na wafanyabiashara wa bodaboda (hawapo kwenye picha) muda mfupi kabla hajawakabidhi msaada wa pikipiki kumi zenye thamani ya shilingi milioni 20.Kushoto ni katibu wa umoja wa wafanyabiashara wa bodaboda, Maulid Mpondo.Kulia wa kwanza ni Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida,Williamu Haaly na anayefuata,ni katibu wa CCM manispaa ya Singida. Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji akimkabidhi katibu wa umoja wa wafanyabishara wa bodaboda msaada wa pikipiki 10. Pikipiki 10 aina ya sanlag CC150 zilizotolewa msaada ya mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Gullam Dewji kwa vikundi 10 vya wafanyabiashara wa bodaboda mjini Singida. Baadhi ya wafanyabiashara wa bodaboda wa mjini Singida wakiserebuka na kucheza 'KIDUKU' na mbunge wao Mohammed Gullam Dewji muda mfupi kabla ya mbunge huyo kuwakabidhi wafanyabiashara hao msaada wa pikipiki. Na Geofrey Mwakibete na Nathan

KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA MASHIRIKA YA UMMA YASIFU UTUNZAJI WA KINU CHA NMC IRINGA

Image
Mwenyekiti wa kamati ya bunge hesabu za mashirika ya umma Zitto Kabwe na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM ) Lediana Mng'ong'o ambaye ni mjumbe wa bodi wakipata maelezo ya kinu cha NMC Iringa   Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga (CUF) Amina Mwidau akiwa na mbunge wa Mwimbala Mhe.Lugolla    Mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe (kulia) akipata maelezo ya mitambo mbali mbali katika kinu hicho   Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo ya kinu hicho Hiki ndicho kinu cha NMC Iringa kilivyotunzwa vema Mjumbe wa kamati hiyo na mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga (CUF) Amina Mwidau (kulia) akiwa na mbunge wa viti malum mkoa wa Iringa Lediana Mng'ong'o ,RAS Iringa Getrude Mpaka , na mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma imetembelea mali za kilichokuwa Kinu cha Kusaga na Kuhifadhi Chakula (NMC) tawi la Iringa na kujiridhisha kwamba ipo haja ya kumbukumbu zake zote ku