Posts

Showing posts from June 15, 2012

TAIFA STARS IKIWASILI NCHINI MSUMBIJI

Image
. Kocha Kim Paulsen akiwaongoza wachezaji wake baada ya kushuka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa maputo leo nchini Msumbiji ambako Taifa Stars itakipiga na timu ya Msumbiji The Mambas Jumapili, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la mtaifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Afrika Kusini mwaka ujao. Kocha Kim Paulsen akiwaongoza vijana wake mazeozini Maputo, kujiandaa na mechi dhidi ya Msumbiji Jumapili Kocha Kim Paulsen akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Shamim Nyanduga mara baada ya timu hiyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo
Image
Image

MBEYA WATINGA FAINALI MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS

Image
  mchezaji namba 7 wa timu ya mbeya stanley Kadumu akipokea zawadi ya mpira kutoka kwa msimamizi wa michezo ya AirtelRising Stars kutoka DRFA Daudi Kanuti mara baada ya kufunga mabao 3 katika mechi ya nusu fainali thidi ya timu ya Ilala Timu ya wavulana mbeya ikishangia ushindi baada ya kuifunga ilala mabo 5-2 katika mchezo wa nusu fainali ya michuano yaAirtel Rising Stars Timu ya wasichana wa Mbeya wakifurahia ushindi katika mechi za nusu fainali za Airtel Rising Star zilizofanyika leo ambapo mbeya imeifunga Ilala kwa penati mabao 3-2
Image
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inawataarifu wadau na wapenzi wa soka kuwa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa YANGA kujaza nafasi zilizowazi za Kamati ya Utendaji unaendelea vizuri chini ya Kamati ya Uchaguzi ya YANGA. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepokea kutoka Kamati ya Uchaguzi ya YANGA nakala za fomu za maombi ya uongozi wa YANGA pamoja na nakala za vyeti vya elimu vya waombaji uongozi kama sehemu ya taarifa ya awali ya mchakato wa uchaguzi huo wa YANGA. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa baadhi ya waombaji uongozi wamewasilisha nakala za vyeti vya kuhudhuria masomo ya sekondari  (Secondary School Leaving Certificate)  badala ya nakala za vyeti vya kuhitimu masomo ya elimu ya sekondari ( Certificate of Secondary Education). Kamati ya Uchaguzi ya TFF imekwisha ielekeza Kamati ya Uchaguzi ya YANGA kuwataka wagombea wote kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 10(4) na (5) inayowataka wagombea wote kujaza Fomu Na.1 ya maombi ya uongozi na

MWENDESHA MASHITAKA MPYA WA ICC

Image
Mwendesha Mashtaka Mkuu mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya kukabiliana na Uhalifu wa Kivita ameapishwa mjini Hague hii leo.   Bi Fatou Bensouda, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Haki nchini Gambia,ndiye Mwafrika na pia mwanamke wa kwanza kushikilia cheo hicho. Mojawapo wa wajibu wake wa mwanzo ni kumleta Hague mwana wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muamar Gaddafi, Saif al-Islam Gadaffi, ambaye ameshtakiwa kwa makosa dhidi ya binadamu na wakati huohuo kuongoza mashtaka yanayomkabili aliyekuwa kiongozi wa Ivory Coast, Laurant Gbagbo. Fatou Bensouda amechukua nafasi ya mtangulizi wake aliyeondoka, Luis Moreno Ocampo, ambaye ameongoza mahakama hiyo kwa zaidi ya mwongo mmoja. Kesi ya rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor, ilisikizwa na mahakama mahakama ya Umoja wa mataifa inayosikiliza kesi za waliohusika na vita vya wenyewe kwa wenyewe Sierra Leone. Bi

SIMBA HAINA MPANGO NA NSAJIGWA

Image

WACHEZAJI WAPYA SIMBA WAANZA MAZOEZI

Image
WACHEZAJI wapya waliosajiliwa na klabu ya soka ya Simba kwa ajili ya kuitumikia katika ligi kuu soka Tanzania bara na michuano ya kimataifa. Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga (pichani)amesema kwamba nyota hao wameungana na wale wa zamani waluioanza mazoezi wuijki iliyopita. Kamwaga aliwataja nyota hao wapya ni pamoja na Paul Ngalema, Salim Kinje, Abdallah Juma, Kigi Makassy, Mussa Mude, Patrick Mbivayanga na Ibrahim Kinje.

KATIBUMKUU AKABIDHI GARI ZIWA TANGANYIKA

Image
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akizindua Gari aina ya LAND CRUISEL ambalo limetolewa na Ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika[AFDB]hii ni gari ya pili ya Mradi ya Kuboresha Shughuli za Uvuvi na Mazingira katika Ziwa Tanganyika kulia Mratibu wa Mradi Dk Hadson Nkotagu,Mkurugenzi Msaidizi Mazingira Bi Magdalena Mtenga[Picha na Ali Meja] Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akimkabidhi Dk Hadson Nkotagu Gari aina ya Land Cruisel la Mradi wa Ziwa Tanganyika ambalolimetolewa Chini ya Ufadhili wa Banki ya Maendeleo ya Afrika[AFDB] hii ni gari ya pili ambayo imetolewa kwa shughuli za Mradi kuboresha Uvuvi katika Mwambao wa  Ziwa Tanganyika,Mikoa ya Kigoma,Rukwa na Katavi Shughuli hiyo imefanyika Ofisini kwa makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Mjini Dar es Salaam[Picha na Ali Meja]

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MRADI WA KUBORESHA ELIMU MKOANI MTWARA LEO

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaangalia na kuwasikiliza wanafunzi wa  Shule ya Msingi Kambarage, walipokuwa wakijifunza kwa njia Kompyuta wakati alipofika shuleni hapo leo Juni 15, 2012, kwa  ajili ya kuzindua Mradi wa Kuinua Elimu ya Msingi ijulikanayo kama 'Tz 21 Century Basic Education Program, mradi  uliofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID). Kushoto kwake Mtaalam wa Mitaala wa Mradi huo,  Adrehem Kayombo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaangalia na kuwasikiliza wanafunzi wa  Shule ya Msingi Kambarage, walipokuwa wakijifunza kwa njia Kompyuta wakati alipofika shuleni hapo leo Juni 15, 2012, kwa  ajili ya kuzindua Mradi wa Kuinua Elimu ya Msingi ijulikanayo kama 'Tz 21 Century Basic Education Program, mradi  uliofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID). Kushoto ni Balozi wa Marekani

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA MATIBABU YA FISTULA

Image
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA ,akiwa amemshika mtoto mchanga baada ya kukabidhiwa na wazazi wake baada ya ushuhuda walioutoa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula- Tanzania ,katika viwanja vya Mnazi mmoja Juni 15,2012. (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT Dk, Wilbroud Slaa. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO) . Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Erwin Telemans akitoa maelezo wakati wa Uzinduzi  wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya FISTULA Tanzania ,Juni 15 2012 katika viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar eSalaam , Uzinduzi rasmi umefanywa na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete,(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO). Baadhi ya wagojwa waliotibiwa FISTULA wakiimba na kutoka ushuhuda wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula Tanzania ,Juni 15,2012 jijini Dar es Salaam, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO). Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi

RAIS WA ZANZIBAR AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA CHUO VIKUU VYA CHINA

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Kiongozi wa Ujumbe wa Wakuu wa Vyuo Vikuu vya China, Dk.Jiang Bo,wakati ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuonana na Rais   leo       [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na  Ujumbe wa Wakuu wa Vyuo Vikuu vya China, unaongozwa na Dk.Jiang Bo,(wa tatu kushoto) wakati ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuonana na Rais na kuzumza nao leo.     [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

TAIFA STARS YAWASILI RASMI MSUMBIJI

Image
Taifa Stars imewasili Maputo saa 5 asubuhi kwa saa hapa tayari kwa mechi dhidi ya Msumbiji (The Mambas) na kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi Nyandugu.   Stars yenye kikosi cha wachezaji 20 chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen imefikia Hotel 2010 LDA iliyoko karibu na Uwanja wa Taifa Zimpeto ambapo mechi hiyo itachezwa Jumapili kuanzia saa 9 kamili kwa saa za hapa ambapo Tanzania itakuwa saa 10 kamili.     Kwa mujibu wa programu ya Kocha Kim, timu itafanya mazoezi leo na kesho katika muda ule ule wa mechi ya Jumapili ambayo itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar. Mpaka timu inawasili hapa hakuna mchezaji yeyote mwenye matatizo ambayo yanaweza kusababisha asicheze mechi ya Jumapili.

RAIS DK.SHEIN AFUNGUA MADRASA

Image
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama  ishara ya ufunguzi wa madrasat Nurullah Kitope Zanzibar,iliyopo Wilaya ya Kaskazini B Unguja,Mkoa wa  Kaskazini,(kulia) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,pia Mwakilishi wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi,jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Mohamed Raza .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akifuatana  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,pia Mwakilishi wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi,pamoja na viongozi wengine alipowasili katika Jengo la Madrasat Nurullah Kitope,kwa ajili ya kulifungua rasmi,lililojengwa kwa ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi  wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza.          [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]  Baadhi ya

UCHAGUZI WA VIONGOZI YANGA

Image
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inawataarifu wadau na wapenzi wa soka kuwa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa YANGA kujaza nafasi zilizowazi za Kamati ya Utendaji unaendelea vizuri chini ya Kamati ya Uchaguzi ya YANGA. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepokea kutoka Kamati ya Uchaguzi ya YANGA nakala za fomu za maombi ya uongozi wa YANGA pamoja na nakala za vyeti vya elimu vya waombaji uongozi kama sehemu ya taarifa ya awali ya mchakato wa uchaguzi huo wa YANGA. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa baadhi ya waombaji uongozi wamewasilisha nakala za vyeti vya kuhudhuria masomo ya sekondari (Secondary School Leaving Certificate) badala ya nakala za vyeti vya kuhitimu masomo ya elimu ya sekondari ( Certificate of Secondary Education). Kamati ya Uchaguzi ya TFF imekwisha ielekeza Kamati ya Uchaguzi ya YANGA kuwataka wagombea wote kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 10(4) na (5) inayowataka wagombea wote kujaza Fomu Na.1 ya maombi ya uongozi na kuamb

MSIBA

Image
Na.Mwandishi wetu. Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias aliyekuwa akisoma kidato cha nne ESACS Academy, amefariki kwa kugongwa na treni maeneo ya kwao kipawa, aligongwa akiwa anasikiliza music kwa headphones huku akichati katika simu yake wakati akitembea kwenye reli. Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia. Marehemu Jackson ndio aliye shinda kwenye Tokelezeiyer Inter-School concert iliyoandaliwa na group  ya Friends 4 Friends tarehe 12 may 2012, pia alishinda dougie competition  wakati 5select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita. Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17, Mungu aipumzishe roho ya marehemu Jackson Thobias kwa amani, Amen.

UMOJA WA VYAMA VYA SIASA WAZUNGUMZA NA WAANDISHI

Image
Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawake na Watoto akielezea  malengo na maendeleo ya Wizara yake kwa Waandishi wa Vyombo mbalimbali hawapo pichani huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.   Katibu Mkuu wa Chama cha siasa TADEA Juma Ali Khatibu akitoa ufafanuzi wa Maswali mbalimbali yalioulizwa na Waandishi wa Habari huko katika Baraza la wawakilishi la zamani Kikwajuni Zanzibar kuhusiana na kuimarisha Amani na Utulivu Zanzibar na Kulaani matukio ya uvunjifu wa Amani yaliotokezea hivi karibuni huko Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR

UMOJA WA VYAMA VYA SIASA WAZUNGUMZA NA WAANDISHI

Image
Katibu Mkuu wa Chama cha siasa TADEA Juma Ali Khatibu akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali hawapo pichani kwa niaba ya Umoja wa Vyama vya TADEA,SAU,NLD na AFP kuhusiana na kuimarisha Amani na Utulivu Zanzibar na Kulaani matukio ya uvunjifu wa Amani yaliotokezea hivi karibuni huko Zanzibar. Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar Vyama vitano vya siasa vimesema mafanikio ya kukua kwa uchumi wa Zanzibar ni matokeo ya kushamiri kwa amani,utulivu na mshikamano wa wananchi. Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari  Mjini Zanzibar, Viongozi wa Vyama   vya TADEA,AFP, NLD, SAU, kwa pamoja vimeridhishwa na ukuaji wa uchumi na kuongezeka kwa pato la wananchi. “Mafanikio ya kukua kwa uchumi wetu yanaendelea kutupa funzo juu ya umuhimu wa kuilinda amani, utulivu na mshikamano wetu ambao umetujengea sifa kubwa” Alisema Katibu Mkuu wa TADEA, Juma Ali Khatib. Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake katika mkutano huo, Katibu Mkuu huyo wa

TIMU YA MBEYA YAFANA AIRTEL RISING STARS

Image
Mchezaji namba 7 wa timu ya mbeya stanley Kadumu akipokea zawadi ya mpira kutoka kwa msimamizi wa michezo ya AirtelRising Stars kutoka DRFA Daudi Kanuti mara baada ya kufunga mabao 3 katika mechi ya nusu fainali thidi ya timu ya Ilala Timu ya wasichana wa Mbeya wakifurahia ushindi katika mechi za nusu fainali za Airtel Rising Star zilizofanyika leo ambapo mbeya imeifunga Ilala kwa penati mabao 3-2 Wachezaji wa timu ya mbeya wa michuano ya Airtel Rising Stars wakifurahia ushindi walioupata leo baada ya kuifunga timu ya Ilala Timu ya wavulana mbeya ikishangia ushindi baada ya kuifunga ilala mabo 5-2 katika mchezo wa nusu fainali ya michuano yaAirtel Rising Stars

SHOMARI KAPOMBE NDIYE MCHEZAJI BORA WA MWAKA 2011

Image
kushoto ni mchezaji bora wa mwaka 2011 wa TASWA Shomari Kapombe akiwa na mgeni rasmi wa sherehe hizo Rais mstaafu Alhaji Ali Hassani Mwinyi wa tatu kutoka kulia akimkabidhi mshindi huyo mfano wa hundi yenye thamani ya shillingi za kitanzania miliono kumi na mbili tu jana usiku.