Posts

Showing posts from June 26, 2012

ZIARA YA RAIS WA JAMHURI YA KIARABU YA SAHARAWI ALIPOWASILI HADI ALIPOONDOKA JANA

Image
 President  Jakaya Mrisho Kikwete receives President Mohamed Abdelaziz  of the Saharawi Democratic  Republic HE  Mohamed Abdelaziz at the Dar es salaam State House in Dar es salaam June 25, 2012  President Jakaya Mrisho Kikwete delivers his speech at a Luncheon he hosted in Honour of  visiting President  Mohamed Abdelaziz at the  Dar es salaam State House President Kikwete speaks  A round of applause rings after President Kikwete’s speech  Nice speech Your Excellency… President Mohamed Abdelaziz responds   President Kikwete and his guest applaud the Tanzania Police Brass band   Conductor Inspector Billy Kachale  leads his Brass Band as President Kikwete with his guest look on  President Kikwete readies to award his guest a special Makonde Chess Board gift  A special Saharawi gift for President Kikwete  A symbolic camel  gift for President Kikwete  Thanks for the  Saharawi robe A souvenir photo  President Kikwete

Maporomoka yahofiwa kuuwa wengi

Image
Bududa, Uganda Shughuli za uokozi zinatarajiwa kuanza tena leo asubuhi mashariki mwa Uganda ambako vijiji vitatu vilifunikwa na udongo kufuatia maporomoka ya udongo yaliyokumba eneo la Bududa. Shirika la msalaba mwekundu nchini Uganda limesema kuwa zaidi ya watu kumi na wanane wamefariki dunia katika maporomoko hayo. Zaidi ya nyumba kumi na tano zimezikwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika eneo hilo. Shirika hilo limesema maafisa wake wanaendelea kuwatibu waliojeruhiwa katika mkasa huo, katika eneo hilo lenye rutuba la Bududa, linalokuza kahawa na lililopo karibu na mbuga ya wanyama ya mlima Elgon. nyumba zimefunikwa futi16 chini Mwandishi wa habari, Stephene Mulaa, aliyezuru eneo la tukio amesema kuwa, ''kufikia jana jioni hakuna mwili hata mmoja ulikuwa umepatikana, kwa sababu inakadiriwa kwamba

ASKOFU GAMANYWA

Image
Askofu  Sylvester Gamanywa, Rais wa Wapo Mission International. Katika toleo lililopita tulianza uchambuzi wa nadharia za kitheolojia ambazo zimekuwa chimbuko la chuki dhidi ya Israeli ndani ya kanisa. Nadharia hizo ni “Theolojia ya Mbadala”, “Theolojia ya Utenganisho” na “Theolojia ya Mabaki”. Kati ya hizi nadharia tatu, inayoongoza kwa chuki dhidi ya Israeli ndani ya kanisa ni ile “Theolojia ya Mbadala”. Hebu tuchunguze kwa ufupi baadhi ya vipengele vinachoashiria kuchochea na kueneza chuki dhid ya Israeli: Chanzo na madhara ya thelojia ya mbadala Nadhari ya Theolojia ya Mbadala ilianza  kati ya karne ya pili na ya tatu tangu kuzaliwia kwa kanisa na ikaanza kujenga mizizi yake yapata muda wa miaka 200 tangu mwanzo wa kanisa. Kilichotangulia ni kuweka kutengeneza “hadharia” kwanza, na baadaye ndipo yakatafutwa maandiko ya kuhalalisha ubaguzi na chuki dhidi ya Israeli. Baada ya nadhariia hii kuota mizizi katika kanisa la wasio wayahudi, ikajitokeza jeuri, ukaid

MSHINDI WA JENERETA JIJINI MWANZA

Image
  Isaya Charles (wa pili kulia), mkazi wa Igoma Jijini Mwanza akionyesha ishara ya dole gumba huku akiwa amejawa na furaha wakati alipokuwa akipokea zawadi ya jenereta kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) mkoani Mwanza Octavian Magire (wa pili kushoto). Isaya alishinda jenereta hiyo baada ya kushiriki promosheni ya "Vumbua Hazina Chini ya Kizibo inayoendeshwa na kampuni hiyo. Wengine katika picha ni wapambe waliomsindikiza mshindi kupokea zawadi yake.   Isaya Charles (wa pili kulia) mkazi wa Igoma Jijini Mwanza akipokea zawadi ya jenereta aliyoshinda kupitia promosheni ya "Vumbua Hazina Chini ya Kizibo" inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL). Anayekabidhi zawadi hiyo ni Meneja Mauzo wa SBL mkoani Mwanza Octavian Magire (wa pili kulia). Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) mkoani Mwanza, Octavian Magire (kushoto) akitoa maelezo mafupi kuhusiana na promosheni ya "Vumbua

WADAU WALALAMIKIA KIINGEREZA

Image
Wadau wa Sanaa wamehoji uhalali wa wasanii wa filamu kutumia kiingereza kwenye majina ya filamu zao huku wakishangazwa na kazi hizo kubeba maudhui ya kizungu zaidi. Wakizungumza wiki hii kwa nyakati tofauti kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa, wadau hao walishangazwa kitendo cha filamu hizo kutumia majina ya kizungu wakati hapa kwetu kuna filamu nyingi kutoka nje zinazotumia lugha za kihindi, kichina, kifaransa  na zinafanya vizuri. “Hoja kwamba, wanatumia majina ya kiingereza ili kuteka soko la kimataifa ni ya kitoto, mbona hapa kwetu kuna filamu nyingi za kihindi na kichina zinanunuliwa kwa wingi? Hapa kuna udhaifu katika kutengeneza filamu zenye ubora tujikite huko”alisema Mzee Nkwama Bhallanga. Kwa mujibu wa wadau wengi waliozungumza, filamu ni taaluma inayozungumza kwa kutumia picha na vitendo zaidi hivyo haihitaji mtazamaji kufahamu lugha iliyotumiwa ili afahamu maudhui na ujumbe unaowasilishwa na kazi husika ya filamu. “Maneno kwenye filamu si muhim