Posts

Showing posts from June 29, 2012

OMOTOLA KATIKA UMANJA WA JK

Image
Mwigizaji Omotola Jalade wa pili kushoto akikabidhiwa zawadi na za khanga, shanga na viatu Wema Sepetu wakati akiondoka kuelekea Nigeria jana usiku. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole ambao waliratibu ziara ya msanii huyo. Mwingine wa msanii Snura.  Omotola akijaribu bangili za kimasai alizopewa kama zawadi 

Wageni watekwa wakiwa kambini Kenya

Image
  Polisi nchini Kenya wamesema kuwa wafanyikazi sita wa shirika la kutoa misaada kwa wakimbizi wametekwa nyara katika kambi ya wakimbizi ya Ifo ilioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. kambi hiyo inatoa hifadhi wakimbizi nusu milioni Waliotekwa ni wafanyikazi wa shirika la Norwegian Refugee Council, ambalo linatoa huduma kwa wakimbizi kutoka Somalia wanaoishi kwenye kambi hiyo.   Msemaji wa Shirika hilo, amedhibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa katibu mkuu Elizabeth Rasmussen alikuwemo kwenye msafara uliovamiwa lakini amenusurika. Hata hivyo shirika hilo halijatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo na watu waliotekwa. Mkuu wa wilaya ya Lagdera ambako kambi hiyo ipo Robert Kimanthi amesema waliotekwa ni raia wa Canada, Norway, Mfilipino, Mpakistani na Wakenya wawili. Wote ni wanaume. Kulingana na polisi watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki walishambulia msafara wa magari katika kambi hiyo ambayo inatoa makaazi kwa zaidi ya wakimbizi nusu milioni kutoka Somali
Image
Mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) wataanza kutetea ubingwa wao Julai 14 mwaka huu dhidi ya Atletico ya Burundi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye ametangaza ratiba ya michuano hiyo leo (Juni 29 mwaka huu) katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).   Timu 11 zitashiriki katika michuano hiyo itakayoanza Julai 14 hadi 28 mwaka huu ambapo kwa siku zitachezwa mechi mbili (saa 8 mchana na saa 10 jioni) huku Tanzania Bara ikiwakilishwa na Yanga, Simba na Azam. Mechi ya kwanza siku ya ufunguzi (saa 8 mchana) itakuwa kati ya APR ya Rwanda na Wau Salaam ya Sudan Kusini.   Kundi A lina timu za Simba, URA ya Uganda, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Ports ya Djibouti. Azam, Mafunzo ya Zanzibar na Tusker ya Kenya ziko kundi B.   Yanga inaunda kundi

RATIBA YA KAGAME CUP

Image
Sat. 14 th July   1  APR vs WAU SALAAM          Uwanja wa Taifa            2pm                        2 YANGA vs ATLETICO           Uwanja wa Taifa            4pm   Sun. 15 th July   3 AZAM vs MAFUNZO             Chamazi                          4pm   Mon. 16 th July   4 VITA CLUB vs PORTS           Uwanja wa Taifa            2pm                         5 SIMBA vs URA                     Uwanja wa Taifa            4pm   Tue. 17 th July   6 ATLETICO vs APR                Uwanja wa Taifa            2pm                        7 WAU SALAAM vs YANGA       Uwanja wa Taifa            4pm   Wed. 18 th July  8 VITA CLUB vs URA               Uwanja wa Taifa            2pm                         9 PORTS vs SIMBA                  Uwanja wa Taifa           4pm   Thu. 19 th July   10 ATLETICO vs WAU SALAAM  Uwanja wa Taifa          2pm                        11 MAFUNZO vs TUSKER          Uwanja wa Taifa          4pm   Fri. 20 th July    12 PO