Posts

Showing posts from September 11, 2012

MAANDALIZI YA MKUTANO

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Theresia Huvisa akizungumza na wandishi wa habari jijini Arusha leo kuhusiana na maandalizi ya mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira kutoka barani Afrika Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo.   Na.MO BLOG -Arusha Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) nchini Tanzania Mh. Theresia Huviza anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa Rais wa Mazingira kwa Afrika katika Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa mazingira unaofanyika Arusha nchini Tanzania kuanzia kesho hadi tarehe 14 mwezi huu.   Waziri Huviza ataongoza kwa kipindi cha muda wa miaka miwili ambapo baada ya hapo nafasi hiyo itachukuliwa na nchini nyingine.  Mkutano huo umefanikishwa na European Union, Ubalozi wa Norway, Global Environmental Facility, UNEP na UNDP na wajibu mwingine ukifadhiliwa na serikali yenyewe.   Bajeti ya maandilizi ya mkutano huo imegharimu takriban dola za kimarekani 350,000 sawa na shilingi