Posts

Showing posts from July 1, 2012

SHEREHE YA KUWAAGA WANACHUO WA DIPLOMA YA ENVIRONMENTAL HEALTH SCIENCE ILIVYOFANA

Image
Mdau David Mathias Kanyelele wa kwanza kushoto kwa waliokaa mbele akisikiliza kwa makini mambo yaliyokuwa yanaendelea Party yenyewe inakuja soon.....

HOTUBA YA MH. RAIS KIKWETE YA MWISHO WA MWEZI WA JUNI

Image
Ndugu Wananchi,               Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza nusu ya kwanza ya mwaka 2012 salama.  Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza nanyi kila mwisho wa mwezi, leo napenda kuzungumzia mambo mawili. Jambo la kwanza ni suala la usafirishaji haramu wa binadamu nchini na la pili ni la mgomo wa madaktari.  Usafirishaji Haramu wa Binadamu Nchini Ndugu Wananchi;               Bila ya shaka mtakuwa mmezisikia taarifa za tukio la kushtusha na kuhuzunisha la kukutwa maiti 43 za watu wasiojulikana, zilizotupwa katika kichaka kilichopo kijiji cha Chitego, Wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma tarehe 26 Juni, 2012.  Pamoja na maiti hao, walipatikana watu 84 wakiwa hai lakini wote wakiwa wamedhoofu na baadhi yao wakiwa mahututi.  Hatua za haraka zilichukuliwa kuwasafirisha watu hao hadi Dodoma ambapo wale waliokuwa mahututi walifikishwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu na wengine w

MANAHODHA STARS WANG'ARA VODACOM

Image
Nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja na msaidizi wake Aggrey Morris wameng’ara katika hafla ya kampuni ya Vodacom kukabidhi zawadi kwa wachezaji, klabu, waamuzi na makocha waliofanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2011/2012.   Katika hafla hiyo iliyofanyika jana usiku (Juni 30 mwaka huu) hoteli ya Double Tree Hilton, Dar es Salaam, Morris anayechezea Azam aliibuka mchezaji bora wa ligi hiyo wakati Kaseja anayedakia Simba alikuwa kipa bora.   Kila mmoja alizawadiwa sh. 3,312,500 katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye. Kaseja aliwashinda makipa Mwadili Ally (Azam) na Deogratias Munishi (Mtibwa Sugar) wakati Morris aliwashinda Haruna Niyonzima (Yanga) na Haruna Moshi (Simba).   John Bocco wa Azam aliyefunga mabao 19 ndiye mfungaji bora, refa bora ni Martin Saanya kutoka Morogoro ambaye aliwashinda Oden Mbaga (Dar es Salaam) na Amon Paul (Mara) wakati kocha bora ni Stewart Hall wa Azam aliyewashinda Charles Kilinda (JKT Ru

SERIKALI KUBORESHA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI

Image
SERIKALI imesema kuwa ipo kwenye mchakato wa kuviboresha viwanja mbalimbali vya ndege hapa nchini ukiwemo uwanja wa ndege wa Arusha kwa kuufanyia matengenezo makubwa uweze kuruhusu kutua kwa ndege kubwa za kimataifa. Waziri wa uchukuzi ,Dkt Harisson Mwakyembe aliyesema hayo jana baada ya kupokea taarifa fupi wakati akiongea na wafanyakazi wa kiwanja cha ndege cha Arusha baada ya kufanya ziara fupi mkoani hapa. Dkt Mwakyembe alisema kuwa uwanja wa ndege wa Arusha unaumuhimu wa kipekee katika kuendeleza utalii wa ndani na kueleza kuwa serikali itafanya kila njia kuhakikisha kuwa uwanja huo unapanuliwa na kuwa na uwezo wa kutua ndege kubwa. Alisema amekuwa akipata malalamiko mengi kuwa uwanja huo umekuwa ukitumika kunyangánya wateja wa uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) huku maombi hayo yakitaka uwanja huo ufungwe. ‘’nimepata taarifa za kutaka kufungwa kwa  uwanja huu wa ndege wa Arusha kwa kuwa unatumika kunyangánya abilia wa uwanja wa KIA ,nimejiridhisha kuwa kiwanja hiki kina