Posts

Showing posts from June 1, 2012

ZITTO AIBUKA NA JIPYA

Image
MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA), jana aligeuka mbogo na kuwafukuza watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Nchini (Tawiri) baada ya kubaini kupotea kwa silaha ambazo hadi sasa hazijulikani ziliko. Zitto akiungwa mkono na wajumbe wa kamati hiyo, alisema kamati hiyo imepata hofu kubwa juu ya kutoweka kwa bunduki hizo, na zaidi baada ya kubainika kuwa moja ya silaha zinazoaminika kumilikiwa na taasisi hiyo kuhusishwa na tukio la mauaji mjini Mugumu, mkoani Mara. Mbali na kuwafukuza watendaji wa taasisi hiyo, aliwaagiza kuwasilisha haraka ndani ya wiki mbili, ripoti kamili itakayoeleza kinagaubaga namna silaha hizo aina ya bunduki zilivyotoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu mwaka 1980. Zitto alisema kuwa suala la upotevu wa silaha hizo, na nyingine kuhusika katika matukio ya kihalifu ni nyeti, na hivyo kamati hiyo ya Bunge inahitaji maelez

GO TO www.zanzibar.net

Image
Image
Katibu tawala wa mkoa wa Singida, Liana Hassan (wapili kulia) akionyesha ramani ya jengo la utawala la hospitali ya rufani ya Singida ambayo ujenzi unaendelea. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Singida, Jerome Alute Nape na ujumbe wake wakikagua majengo ya hospitali hiyo Nape akionyeshwa ndani ya moja ya majengo ya Hospitali hiyo KATIBU Tawala wa mkoa wa Singida, Liana Hassan (kushoto) akimpa maelezo Nape kuhusu ujenzi wa hospitali hiyo ulipofika. Kulia ni Alute Nape akimaliza kukagua majnego ya hospitali hiyo

NAPE AKIKAGUA UJENZI MAJENGO YA HOSPITAL YA RUFAA IRINGA

Image

VIEW OF ZANZIBAR HOTEL

Image

AHADI KUTOKA CCM

CHAMA cha Mapinduzi, kimesema ahadi ilizozitowa kwa wananchi katika kuinadi Ilani ya chama hicho inazitekeleza kwa hatua ili kuwaletea wananchi maendeleo katika maeneo yao. Aidha chama hicho, kimesema kinakusudia hadi kufikia mwaka 2015 iwe tayari yake ya Uchaguzi wa mwaka 2010-2015 za kuwaletea Maendeleo, zipo pale pale na itaendelea kufanya hivyo na kuhakikisha kuwa kero mbali mbali zinapatiwa ufumbuzi mapema iwezekanavyo kabla ya 2015 hatuwa kwa hatuwa. Akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Mkanyageni Pemba, Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM, na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia , Profesa, Makame Mnyaa Mbarawa, wakati wa kukabidhi mashine ya kusukumia maji kwa wananchi wa Jimbo hilo, alisema kuwa CCM, ina kila sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa ndicho chama kinachoiongoza nchi. Alisema huduma nyingi za kijamii ikiwemo, barabara, maji safi na salama, afya, miradi ya elimu imeweza kutekelezwa kwa kupitia ilani ya chama hicho cha kuwaletea maendeleo wan
Image

CHEZEA KUKU WEWE

Image

MISS TABATA LEO

Image
Shindano la kusaka Miss Tabata 2012 linafanyika leo (Ijumaa) katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata. Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa bendi za Mashauzi Classic na Mashujaa zitawasindikiza warembo 19 watakaopanda jukwaani kuwania taji hilo. Mratibu wa shindano hilo lililoandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts  alisema kuwa mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh 500,000/- na king’amuzi ambayo imelipia miezi sita yenye thamani ya sh 800,000 iliyotolewa na Multichoice. Mshindi wa pili atapata sh 500,000, mshindi wa tatu sh 350,000 wakati washindi wa nne na watano kila moja atapata sh 200,000. Kapinga alisema warembo watano watawakilisha Tabata kwenye shindano la Miss Ilala. Warembo wengine watakaoingia 10 bora kila moja atapata sh 100,000 wakati waliyosalia watapata Sh 50,000 kila moja. Kapinga alisema shindano hilo pia litatumika kwa ajili ya kusherehekea miaka 10 tangu kuasisiwa kwa shindano la Miss Tabata. “Shindano

REDDS MISS MTWARA KESHO NI KESHO

Image
Warembo watakaopanda jukwani kumtafuta Juni 2, 2012 kuwania taji la Redds  Miss Mtwara 2012 Wakimsikiliza mkufunzi wao Isabela Mpada (MISS RUVUMA 2006),shindano hilo linataraji kufanyika katika ukumbi wa Makonde Beach mjini humo. Vimwana wanaoshiriki shindano la Redds Miss Mtwara 2012 wakiwa katika picha ya pamoja. Warembo wanaowania taji la Redds Miss Mtwara 2012 wakiwa katika picha ya pamoja na muandaaji wa shindano hilo  Rajab Mchatta. Shindano hilo linataraji kufanyika kesho Juni 2, 2012 mjini humo katika ukumbi wa Makonde Beach.

HASHEEM THABEET KUJENGA UWANJA WA KISASA WA MPIRA WA KIKAPU

Image
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Lord Baden Powell, Kanali Idd Kipingu akizungumza machache mbele ya wageni wake waliofika mapema leo shuleni hapo kwa ajili ya kuangalia namna ya kujenga uwanja wa mchezo wa mpira wa kikapu. Mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania, anayechezea timu ya Portland Trail Blazers ya Marekani kwenye Ligi ya NBA, Hasheem Thabeet akizungumza jambo mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari  ya Lord Baden Powell Memorial High School,wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kiwanja cha mpira wa kikapu shuleni hapo mapema leo Bagamoyo,nje kidogo ya jiji la Dar,kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania, Phares Magesa. Hasheem Thabeet ameahidi kuwajengea uwanja wa mpira wa kikapu shuleni hapo. 

VIWANGO VYA SHULE VYA SHUSHWA

Image
Watoto wa sule Ripoti ya kujitegemea ya serikali ya Uingereza imebaini kwamba msaada wa Uingereza kwa nchi za Afrika za Ethiopia, Rwanda na Tanzania umechangia kuporomoka kwa viwango vya elimu katika shule za nchi hizo. Uchunguzi umeonyesha kuwa watoto milioni hamsini na mbili zaidi wanapata elimu kwa sababu ya msaada huo, huku walimu wasio na sifa ya ualimu wakiajiriwa kukabiliana na ongezeko hilo la wanafunzi. Hii ni kumaanisha kwamba kiwango cha elimu kwa ujumla katika mataifa hayo kimeshuka, huku watoto wengi wakimaliza elimu yao bila kujua kusoma wala kuandika na kuhesabu. Malcolm Bruce ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya maendeleo ya kimataifa ya bunge la Uingereza na ameiambia BBC kwamba, ingawa imebainika kasoro hiyo, lakini ni muhimu msaada huo uendelee kutolewa kwa nchi hizo.

LINAH AWASILI NCHINI TZ

Image
Image
Image
Image
Image
Image
Image

NMB YAZINDUA PROMOSHENI YA JENGA MAISHA YAKO NA NMB

Image