Posts

Showing posts from January 9, 2013

VETA KIPAWA KULIPA ADA KUPITIA M-PESA

Image
Mkuu wa chuo cha VETA kipawa, Jijini Dar es Salaam, Eng. Lucius Luteganya, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ulipaji ada kwa wanafunzi wa chuo hicho kupitia huduma ya M – Pesa. Kufuatia ushirikiano kati ya chuo hicho na Vodacom Tanzania. Kushoto ni Mkuu wa ukuzaji biashara – M - PESA Jackson Kiswaga. Meneja mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa, akimuelezea jambo Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Eng. Lucius Lutenganya wakati wa uzinduzi wa ulipaji ada kupitia huduma ya M – pesa kwa wanafunzi wa chuo hicho. Katikati ni Mkuu wa Ukuzaji Biashara – M - PESA, Jackson Kiswaga. Wanachuo wa Chuo cha VETA Kipawa Dar es Salaam kuanzia sasa wataanza kulipa ada kupitia huduma ya M-Pesa baada ya chuo hicho kufikia makubaliano na Kampuni ya Simu za mikononi ya Vodacom kuwezesha huduma hiyo. Chuo hicho ni miongoni mwa Shule na Vyuo vingine kadhaa ambavyo vipo katika hatua za mwisho za mazungumzo na Vodacom ya kuviwezesha kutumia hudum