Posts

Showing posts from August 16, 2012

WAREMBO WA REDD'S MISS ILALA 2012 WATAMBULISHWA RASMI JIJINI DAR LEO

Image
Mratibu wa Shindano la Redd's Miss Ilala 2012,Gadner G. Habash akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge mchana huu wakati wa kuwatambulisha warembo watakaoshiriki kwenye fainali ya Redd's Miss Ilala 2012.washindi watafanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye fainali ya Redd's Miss Tanzania 2012.Wengine Pichani toka Kulia ni Mratibu Mwenza wa Shindano hilo,Juma Mabakila,Cylivia Mashuda na Neema Mbula ambao ni walimu wa warembo hao. Baadhi ya warembo watakaoshiriki Shindano la Redd's Miss Ilala wakiwa kwenye kikao hicho kama wanavyoonekana. Hapa lazima ilala itoe Redd's miss Tanzania 2012. Warembo wakiwa wamepozi. Warembo katika picha ya Pamoja

KCB NAYO YATOA MSAADA

Image
  Afisa Masoko wa  B enki ya KCB  Tanzania  tawi la Morogoro,Herieth Mwakifulefule akimsaidia kumvisha kiatu Kulwa Mussa, ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la Tatu katika shule ya msingi  ya  Ujirani ya jamii ya wamasai iliyopo katika kijiji cha Kienge B, baada ya benki hiyo kutoa msaada wa madawati 80 yenye   thamani ya shilingi milioni4.8. mtoto huyo tangu darasa la kwanza amekuwa akishika na fasi ya   kwanza katika darasa lao. ****** BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni nne na laki nane (4.8m) kwa shule ya msingi Ujirani iliyopo katika kata ya Mkundi manispaa ya Morogoro. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati hayo, Meneja wa KCB Tawi la Morogoro Carlos Msigwa alisema kuwa lengo la msaada huo lilikuwa kusaidia upungufu wa madawati katika shule hiyo na hivyo kuwawezesha wanafunzi kusoma vizuri Meneja huo alisema kuwa Benki ya KCB inatambua umuhimu wa elimu bora katika maendeleo y

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AZINDUA SHULE YA SEKONDARI MAENDELEO HUKO NAKASANGWE MADALE JIJINI DAR ES SALAAM

Image
  Mwenyekiti wa Kia motors, Cho Kwi Hyun akikabidhi Kuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik mfano wa ufunguo wa moja ya magari manne ambayo kampuni hiyo imetoa kwa shule ya Maendeleo iliyopo  Nakasangwe Madale wakati wa hafla ya uzinduzi wa shule hiyo leo kulia ni Mkurugenzi Shirika (GNI), Yang Jin OK na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali Mtaa Madale Alex Mbuya  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akihutubia wananchi wakati wa uzinduzi wa shule ya Maendeleo iliyoko Nakasangwe Madale jijini Dar es salaam iliyojengwa  kwa msaada wa kampuni ya  KIA na HYUNDAI za Korea kupitia shirika la Vijana mbalimbali kutoka Shirika la GNI nchini Korea walioshiriki kujitolea kujenga shule ya Sekondari Maendeleo Nakasangwe huko Madale  wakiwa katika hafla ya uzinduzi leo

AHADI KUTOKA NMB

Image
NMB YAAHIDI KUBORESHA KILIMO CHA WAKULIMA WADOGO WADOGO KWA KANDA YA KASKAZINI BENKI ya NMB  kanda ya kaskazini imesema kuwa ina mikakati mbalimbali ya kuweza kuimarisha kilimo hasa kwa wakulima wadogo wadogo sanjari na kutoa mikopo mbalimbali kama vile Pembejeo kwa wakulima hao wadogo wadogo ili kufanya Kilimo chao kuwa cha Kisasa zaidi Hayo yameelezwa na Bw Ally Jamali ambaye ni afisa uhusiano kilimo katika benki hiyo wakati alipokuwa akiongea na Waziri Mkuu Bw Mizengo Pinda ambaye alitembelea banda la NMB katika viwanja vya Nane nane (TASO)mapema juzi Aidha bw Jamali alisema kuwa ili kumkomboa Mkulima wa sasa Benki hiyo imejidhatiti kuhakikisha kuwa  wakulima wadogo wadogo wanapata huduma za msingi ili nao waweze kufikia malengo yao mbalimbali ambayo wamejiwekea Alifafanua kuwa kwa sasa kupitia mfum wa Stakabadhi ya mazao ghalani (WRS) wwakulima wa kanda ya kaskazini wameweza kupata mikopo ya aina mbalimbali ambapo lengo ni kukomboa zaidi Kilimo kwanza