Posts

Showing posts from June 12, 2012

WAZIRI MKUU AFUNGUA KIWANDA CHA NYUKI KIBAHA

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua kiwanda cha kusindika asali cha Organic Honey katika kijiji cha Visiga mkoani Pwani kinachomilikiwa na kampuni ya Boleyn International, Juni 9, 2012.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na anyepiga makofi katikati ni Mkrurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Jack Liu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mitambo baada ya kufunguza kiwanda cha kusindika asali cha  Organic Honey katika kijiji cha Visiga  mkoani Pwani  kinachomilikiwa na Kampuni ya  Boleyn  International, Juni 9, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Image
Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Ruvuma Bwana Hassan Mpapi Bendeyeko akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili TATAKI Dkt.Aldin Mutembei akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitabu cha kwanza cha fasihi simulizi ya jamii ya Wakwere ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa Idara ya historia katika chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Kapepwa Tambila. Dkt.Mutembei ambaye pia ni mchapishaji na msimamizi wa tafiti za Tamaduni lugha na fasihi za makabila ya Tanzania alikabidhi pia kamusi Asisi ya Kiingereza-Kiswahili na Kiarabu

UFAFANUZI

KATIBU wa Bunge Dk. Thomas Kashililah ametoa ufafanuzi kuwa mbunge wa Bahi, Omar Badweli anayetuhumiwa kwa rushwa ataendele kuwa mbunge hata kama atahukumiwa kifungo cha chini ya miezi sita jela. Dk. Kashililah alisema hayo jana alipozungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa gazeti hili kuwa mbunge huyo bado ni mtuhumiwa na pia kwa mujibu wa katiba atakoma kuwa mbunge kama atahukumiwa kifungo cha kuanzia miezi sita jela.     Amesema hayo baada ya mbunge huyo Badwel kufunguliwa kesi mahakamani ya tuhuma ya kuomba rushwa ya sh. milioni nane toka halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Pwani.      Dk. Kashililah alitoa mfano wa mbunge wa Mbarali, Modestus Kilufi ambaye hivi karibuni mahakama ilimtia hatiani kwa kosa la kutishia kuua kwa maneno kwa kukusudia na kumuhukumu kwenda jela miezi 10 au kulipa faini ya Sh. 500,000.      Hata hivyo Kilufi alilipa faini hiyo na kuachiwa huru na mahakama ya Mbeya. Alisema hata kama Badwel atafungwa kifungo cha chi

PONGEZI KUTOKA KWA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR

Image
Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Ofisi ya Tume ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) na Tume za Nguvu za Atomic (TAEC) kwa uwamuzi wake wa busara  kwa kuamua kufungua ofisi zao hapa Zanzibar Pongezi hizo alizitoa jana huko Tunguu wakati alipokuwa akizindua Ofisi  hizo alisema kuwa ni faraja kubwa kwa watu wa Zanzibar kupata huduma za Tume ya Sayansi na Teknologia pamoja na Nguvu za Atomic hapa hapa Zanzibar . Alieleza kuwa tume hizo ambazo zimefungua ofisi zake hapa Zanzibar itasaidia kuwapatia elimu mbali mbali wananchi wa Zanzibar wakiwemo wajasiri amali ambao tayari wameweza kupata elimu ambayo imewafanya kuweza kuuuza bidhaa zilizokamilika. Aidha akifafanua alisema kuwa bidhaa hizi ambazo zinatengenezwa na wajasili amali zinawafanya waweze kupata  manufaa ambayo  huongeza  harakati ya maendeleo kiuchumi pamoja na kupunguza umasikini nchini. Balozi huyo alieleza kuwa tume hizi zitasaidia kutoa mchango mkubwa kwa
Image
Mh. spika akizungumza na balozi wa marekani nchini Tanzania ndugu Alfonso Leinhardit