Posts

Showing posts from August 2, 2012

MATUKIO MBALI MBALI YA PICHA BUNGENI LEO

Image
Mwigulu Mchemba ( kulia ) wa jimbo la Iramba Mashariki akibadishana hoja na Mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa wote ni wabunge wa CCM  Bungeni Dodoma Maafisa wa Bunge wakiwa makini kufuatilia hoja mbalimbali   za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa Fedha 2012-2013. Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan  ( kulia ) na Mbunge wa Muheza Hebert Mtangi ( kushoto ) wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma . Naibu Spika Job Ndugai ( kushoto ) akimsikilza Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela katika viwanja vya Bunge – D odoma leo.

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AZINDUA SHULE YA URAFIKI

Image
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd leo amezindua ujenzi wa Skuli ya msingi iliyopewa jina la Urafiki inayofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.   Balozi Seif Idd aliyasema hayo katika skuli ya Mwanakwerekwe C wakati akizindua ujenzi wa skuli ya urafiki inayofafdhiliwa  na Serikali ya China kwa Dola za Marekani 1.6. katika sherehe za uzinduzi wa Skuli hiyo yenye madarasa kumi na mbili,Makamu wa Rais amesema kwamba wananchi wa Zanzibar wanathamini mchango unaotolewa na Serikali ya China. Pia alisema Serikali inaupa kipaumbele sana mchango huo kwa kuchangia katika sekta ya Elimu kwani bila ya elimu hakuna maendeleo. Aidha, Balozi Seif Idd amesema kwamba Serikali itachukua kila jitihada kuhakikisha tatizo la vikalio linamalizika katika skuli zote za Unguju na Pemba alisema.  Utoaji wa madeksi hayo

RAMBIRAMBI MSIBA WA MSAFIRI MKEREMI

Image
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mwamuzi wa zamani wa kimataifa Msafiri Mkeremi kilichotokea leo alfajiri (Agosti 2 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora. Licha ya kuwa mwamuzi, Mkeremi aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) sasa TFF kwa vipindi viwili tofauti. Pia aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT).   Vilevile aliwahi kuwa mkufunzi wa waamuzi, mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) Mkoa wa Pwani.   Kwa upande wa vyama vya mpira wa miguu aliwahi kuwa kiongozi katika mikoa ya Tabora, Pwani na wilayani Mpanda katika Mkoa wa Rukwa.   Msiba wa Mkeremi uko nyumbani kwake Urambo, na kwa mujibu wa mtoto wake Masoud Mkeremi, atazikwa Jumamosi kwenye makaburi ya Msafa yaliyoko wilayani Urambo.  

REDDS MISS MWANZA 2012/13 KUFANYIKA AGOSTI 31

Image
Mrembo wa mkoa wa Mwanza 2012/13 atapatikana ijumaa ya agosti 31 katika viwanja vya Yatch Club Mwanza. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na muaandaji wa kampuni ya Sisi Entertainment John Doto, amesema shindano hilo linalovuta hisia za wengi ndani ya mkoa wa Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, litashirikisha warembo tariban 20 kutoka wilaya zote za mkoa Mwanza.

KATIBA MPYA

Image
         Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kimesema wananchi hawajafungwa kutoa mawazo yao katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba,lakini msimamo wa CCM ni kubaki katika mfumo wa muundo wa Serikali mbili. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mjini hapa Jana, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM ZanzĂ­bar, Jamal Kassim Ali alisema kimsingi wananchi wako huru kutoa maoni yao kuhusu aina ya mfumo wa Muungano,lakini kwa wanachama wa CCM ni lazima wafuate msimamo wa Chama hicho. Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kwamba Umoja wake unaamini katika kulinda na kuhifadhi umoja na mshikamano uliopo hivyo ni muhimu kwa wananchi kutokubali kushawishiwa kuvunja Muungano. “Katika suala la Muungano, CCM imeweka wazi kuwa itaendeleza muundo wa Muungano wa Serikali mbili kama inavyoelezwa katika ibara ya 221(a) ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi sisi hatuwezi kuikiuka katiba hiyo” Alisema Jamal.

KIGODAAITAKA TBS KUFANYA UKAGUZI

Image
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amelitaka Shirika la Viwango (TBS), kuhakikisha linafanya ukaguzi wa bidhaa kutoka nje kabla hazijaingizwa nchini ili kuepukana na tabia nchi hii kugeuzwa dampo la bidhaa hafifu. Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana, wakati alipokuwa akizindua Ofisi ndogo ya shirika hilo, inayoshughulika na ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi. Dk Kigoda alisema iwapo shirika hilo litafanikiwa kudhibiti uingizwaji wa bidhaa hafifu nchini anaamini kelele zote zinazopigwa kuwa wao ndio chanzo cha uingizwaji wa biadhaa hizo zitakwisha. “Nawaagiza TBS kupitia madukani na sokoni ili kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa ubora wa bidhaa na zile bidhaa mtakazokuta ni hafifu, zitoweni na kuziharibu na hao wafanyabishara watozwe faini za kuharibu bidhaa zao”alisema Dk Kigoda. Alibainisha kuwa Wizara yake inatarajia kupata taarifa juu ya utekelezaji wa maagizo hayo kwa vipindi vya kila robo mwaka ili kujua utaratibu wa utekeleza

NGASA AHAMIA SIMBA

Image
Mchezaji mharufu nchini Tanzania na Afrika mashariki na kati hii leo amekili yeye mwenyewe akisema kwamba ametia sahii kuichezea Simba S.C mabingwa wa Vodacom Premier league msimu wa 2011-2012 nchini Tanzania uhamisho huo ni mkopo ambapo klabu za Yanga na Azam wamekubali uhamisho huo ingawa kuna maneno ya hapa na pale kwamba mchezaji huyo ajawakilishwa kwenye mchakato wa yeye kuhamia klabu hiyo.