Posts

Showing posts from August 22, 2012

AMSHA AMSHA LA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 MOSHI MJINI

Image
Mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya kutoka Clouds FM akizungumza na mmoja wa mashabiki wa kituo hicho cha redio,mapema leo mtaa wa Ghala mjini Moshi,ikiwa ni sehemu ya mchakato mzima wa amsha amsha ya tamasha kubwa la Serengeti Fiesta,ambalo linatarajiwa kufanyika mjini humo siku ya ijumaa katika chuo cha ushirika.wasanii watakao shiriki kadhaa ni Joh Makini,Mwana FA,Linah,Godzilla,Juma Nature,Ommy Dimpoz,Bob Junior,Sheta,Ferooz,Richard Mavoko,washindi wa Supa Nyota na wengineo kibao. Kama vile haitoshi kutakuwepo  na wasanii lukuki wa bongofleva akiwemo na aliyeshiriki shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezzoo. Washkaji nao hawataki kupitwa kabisa na shughuli nzima ya mambo yanayoshushwa na Clouds FM,hapa walikuwa wakisikiliza kipindi cha amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lililokuwa likirushwa live hewani ndani ya mji wa Moshi mapema leo mtaa wa Ghala. Kiongozi wa msafara wa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjini M

TTB yawatunuku Vyeti watanzania waliofanya vyema katika Utalii

Image
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB Dk Aloyce Nzuki wa tatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na watanzania hao wakiwa wameshika vyeti vyao kushoto ni Wilfred Moshi, Respicius Baitwa wa pili kutoka kulia na Juma K. Nugaz aka Antonio Nugaz wa tatu kutoka kushoto wengine ni Geofrey Meena Meneja Masoko wa TTB na Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa pili kutoka kushoto. Bodi ya Utalii Tanzania TTB leo imetoa vyeti kwa watanzania watatu walioipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika masuala ya Utalii. Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania Dk Aloyce Nzuki Akizungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya tukio muhimu la kuwatunikia vyeti watanzania wa tatu amesema watanzania hao waliweza kupeperusha bendera ya Tanzania vizuri hasa katika masuala ya utalii, kwa hapa Tanzania na nchi za nje. Watanzania hawa wameweza kufanya mambo makubwa ambayo kwa kiasi kikubwa sana yamechangia kwenye sekta ya utalii.Watanzania ambao

CCM KUKATA RUFANI DHIDI YA HUKUMU YA KESI UCHAGUZI IGUNGA

Image
CHAMA  Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakikuridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga, Dk.Peter Dalali Kafumu. Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye mchana leo, imeseme kufuatia kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa jana na Jaji wa Mahakama hiyo, Mary Shangali,  kitakata rufani. "Chama Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa jana Agosti 21, 2012 na Mahakama Kuu kanda ya Tabora. Kimejiridhisha na kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora Dokta Dalali Peter  Kafumu.Kusudio hilo linatokana na kutorishwa na hukumu hiyo". imesema taarifa hiyo. Jana Jaji  Mary Shangali katika hukumu yake, alisema ametengua ushindi wa Dk. Kafumu baada ya kurishishwa na madai saba kati ya 17 yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo na Mlalamilikaji, aliyek

RAIS KIKWETE AKAGUA GHALA LAKE LA MAHINDI MSOGA LEO

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na mjukuu wao Aziza Ridhiwani (3) katika ghala ya mahindi yaliyovunwa kwenye shamba lao kijijini Msoga, nje kidogo ya mji mdogo wa Chalinze, Mkoa wa Pwani. Rais Kikwete ni mkulima na mfugaji kijijini hapo na ameonesha kufurahishwa sana na mavuno makubwa ya mahindi shambani kwake. Hii  katika kutekeleza kwa vitendo sera ya Serikali  ya kuendeleza kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya sekta ya kilimo katika Tanzania.

JIANDAE KUHESABIWA

Image

DALALI PETER KAFUMU AVULIWA UBUNGE

Image
  Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora imetengua matokeo ya Ubunge wa Mbunge wa jimbo la Igunga Mh. Dalaly Peter Kafumu ambaye alichukua nafasi hiyo baada ya mbunge wa zamani wa jimbo hilo Rostam Azizi Kujiuzulu. Mahakama hiyo imemvua Ubunge Dk. Kafumu hii leo katika Hukumu ya kesi ya Kupinga matokero iliyofunguliwa na aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Chadema, Joseph Kashindye dhidi ya Dk Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi.   Mbali na Dk Kafumu, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi huo, Protace Magayane. Shauri hilo lilianza kusikilizwa rasmi Machi 26 na Jaji Mary Shangali.   Zaidi ya malalamiko 15 yaliwasilishwa katika Mahakama hiyo na profesa Safari kwamba waziri wa ujenzi dk. Magufuli alitoa ahadi kwenye mkutano wa kampeni kwamba atawajengea daraja la Mbutu wananchi wa igunga kama watamchagua dk.Kafumu kuwa mbunge wao pia profesa Safari alidai kwamba was

Michuano ya Airtel yaanza Nairobi

Image
Michuano ya Airtel Rising Stars barani Afrika imetimua vumbi   Jijini Nairobi, Kenya. Michuano hiyo imeleta pamoja wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba na itaendelea mpaka Agosti 25. Michuano hiyo ambayo ilianzia kwenye ngazi ya wilaya mpaka Taifa na kufanyika kwenye nchi 15 barani Afrika. Huu ni mpango kabambe wa Airtel Rising Stars, wenye lengo la kuwapa vijana chipukizi fursa ya kuonyesha vipaji vyao. Ikiwa ni ya moja ya michuano mikubwa kabisa barani Afrika, jumla ya timu 18,000 zilishiriki na wachezaji 324,000 – wavulana na wasichana kushiriki. Hii ndio mara ya kwanza kushirikisha wasichana. Michuano hiyo ilifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Kenya, Mh Raila Odinga – akisindikizwa na Mtendaji Mkuu wa Bharti Airtel Afrika – Manoj Kohli Michuano hiyo pia itaashiria uzinduzi wa kliniki mbili za soka za kimataifa zitakaozoendezwa na makocha kutoka klabu kubwa duniani – Arsenal na Manchester United – zote za Uingereza.  Kw

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWATAKA WATANZANIA KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA SENSA

Image
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua kampeni ya uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi kwenye viwanja vya mnazimmoja jijini Dar es salaam Agust 17,2012.Watatu kushoto ni  Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na kulia kwake ni Kamishina wa Sensa, Hajati Amina Mrisho(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

LIGI KUU YA TANZANIA BARA KUCHELEWA KUANZA, TENGA AMTOSA RAGE , SEMINA YA WAAMUZI

Image
Tuesday, August 21, 2012 Kumekuwepo na taarifa tofauti kuhusu kuanza kwa Ligi Kuu ya Bara ambayo kwa mujibu wa kalenda ya Shughuli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), inatakiwa kuanza Septemba 01, 2012. Baada ya kikao cha pamoja baina ya TFF na viongozi wa klabu za Ligi Kuu kilichofanyika Jumatatu ya Agosti 20, 2012 kwenye ofisi za TFF, TFF inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:   1.      Baada ya kikao cha pamoja baina ya TFF, Kamati ya Ligi na viongozi wa klabu zote za Ligi Kuu, ilionekana kuwa kutokana na kutokamilika kwa mazungumzo baina ya TFF/Kamati ya Ligi na mdhamini wa sasa, yaani Vodacom, mwanzo wa Ligi Kuu unatarajiwa kuwa Septemba 15, 2012. Hii inatokana na ukweli kwamba kukamilika kwa mazungumzo baina ya pande husika, ndio kutatoa picha halisi ya Ligi Kuu ya msimu ujao.   2.      Mazungumzo baina ya TFF/Kamati ya Ligi na Vodacom yanatarajiwa kukamilika mwishoni mwa wiki hii kwa kuwa yameshafikia hatua nzuri na hivyo mkataba unaweza

WATATU WATEULIWA KINYANG'ANYIRO CHA UWAKILISHI JIMBO LA BUBUBU

Image
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi imejadili majina ya wanachama watatu wanaowania kuteuliwa na Chama hicho kwa ajili ya kinya’nganyiro cha Uchaguzi mdogo wa Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Bububu. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, ilisema kwamba kikao hicho kimependekeza kwa Kamati Kuu ya CCM majina ya   Husein Ibrahim Makungu (Bhaa), Omar Ibrahim Kilupi na Fatma Salim Said. “Kikao kilipokea na kujadili majina ya wana CCM 3 walioongoza katika kura za maoni   kwenye mkutano mkuu maalum wa Matawi ya Jimbo la Bububu na hatimaye kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya   CCM, kwa hatua za mwisho” Ilisema taarifa hiyo ya CCM. Katika hatua nyengine, Kamati Maalum imempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, kwa   kusimamia vizuri kazi ya   uokoaji

RAIS KIKWETE AREJEA DAR

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe raymond Mushi baada ya kureje usiku huu Agosti 19, 2012 kutoka Maputo, Msumbiji alikohudhuria kikao cha viongozi wa Jumuiya Ya Maendeleo Kusini Kwa Afrika (SADC) uliofunguliwa tarehe Agosti 17,  2021 na kumalizika jana jioni  Agosti  18 2012.  Katika kikao cha Jana Tanzania imechukua uenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama kutoka Afrika ya Kusini ambapo uenyekiti wa SADC umechukuliwa na Msumbiji kutoka Angola. Nafasi hizi ni za mwaka mmoja mmoja Kwa zamu.   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema baada ya kuwasili  usiku huu Agosti 19, 2012 kutoka Maputo, Msumbiji alikohudhuria kikao cha viongozi wa Jumuiya Ya Maendeleo Kusini Kwa Afrika (SADC) uliofunguliwa tarehe Agosti 17,  2021 na kumalizika jana jioni  Agosti  18 2012.  Katika kikao cha Jana Tanzania imechukua uenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama kutoka Afr