Posts

Showing posts from June 19, 2012

MSIMAMO WA MBUNGE JOHN MNYIKA

Image
Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.   Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

DULLY SYKES AOMBA MSAMAHA

Image
Msanii maarufu wa bongo fleva Dully Sykes amewaomba msamaha mashabiki wake kwa kauli aliyoitoa jana katika kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds fm. Akiongea katika kipindi cha ampifaya Dully amesema sababu iliyomfanya atoe kauli ile ni hasira alizokua nazo wakati anapigiwa simu na Sudy Brown. Dully Sykes jana katika kipindi cha XXL kupitia segment yake ya you heard inayosimamiwa na Gossip cop Sudy Brown,        Sudy alimpigia simu Dully kutaka kujua suala la nyimbo ya Mwana FA inayokwenda kwa jina la amen ambayo dully amepewa shavu, nyimbo hiyo inasemekana imekopiwa kutoka kwenye nyimbo ya cecile wa Jamaica. Baada ya kupigiwa simu dully alitoa kauli zilizotafsiriwa kama ni matusi. Lakini kwa kuonesha kutambua kosa lake dully ameomba msamaha mashabiki wake.

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI

Image
Marehemu Willy Edward (kulia) akiwa na Rais Jakaya Kikwete enzi za uhai wake. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Fenella Mukangara kuomboleza kifo cha Mhariri Mtendaji wa Gazeti la JamboLeo, Ndugu Willy Edward Ogunde kilitokea usiku wa kuamkia jana, Jumapili, Juni 17, 2012  mjini Morogoro. Katika salamu zake za rambirambi, Mheshimiwa Rais Kikwete amesema kuwa ameshtushwa na kusikitishwa na kifo cha ghafla cha Ndugu Willy Edward Ogunde ambaye amepoteza maisha akiwa bado kijana ingawa tayari alikuwa amekwishakutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya tasnia ya habari kutokana na umakini wake, uzingatiaji  wa weledi kikamilifu na misingi mingine mikuu ya uandishi wa habari. “Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi kifo cha ghafla cha Ndugu Willy Edward Ogunde ambaye nimejulishwa kuwa kilitokea usiku wa kuamkia jana,

RAIS KIKWETE AWAAPISHA WAJUMBE SITA WA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi  amewaapisha wajumbe sita wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi. Wajumbe walioapishwa ni Bw. Cornel Kananila Mtaki ambaye anakuwa Mwenyekiti  wa tume hiyo ambapo makamisha ni  Bibi Mary Cresent Massay, Bibi Salma Abdi Chande na Bw. Evod Paul Mushi. Makamishna wenginei Bw. Sauli Herbet Kinemela na Bw. Yahya Kitambazi Msigwa. Wajumbe wa tume hii wanashika nafasi ya tume ya awali ambayo ilimaliza muda wao mapema mwaka 2011, ambapo wajumbe wa tume iliyoapishwa leo waliteuliwa mwishoni mwa mwaka 2011. Wakati huo huo Rais amekutana na kufanya mazungumzo na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Viongozi wa Chama cha riadha nchini ambapo amewataka viongozi hao wafufue mchezo wa riadha hapa nchini. “Kama kuna kitu mnataka serikali isaidie itawasaidia , lakini mchezo wa riadha kama michezo mingine,  inahitaji juhudi za vilabu vya michezo yenyewe, na serikali inachangia tu lakini jukumu kubwa ni lenu.”.  Rais amesema na kuwapa changa

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWANA WA MTOTO WA MFALME

Image
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na/akimsinidikisa Mwana wa Mfalme na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mhe. Abdulaziz Bin Abullah Bin Abdul Aziz Al Saudi  jana, juni 18, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifanya mazungumzo. Rais Jakaya Kikwete akimsindikiza Naibu Waziri Mkuu wa Kenya ambaye pia ni Waziri wa Serikali za Mitaa Mhe. Musalia Mudavadi baada ya maongezi yao Ikulu jijini Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mchungaji Keishi Miyamoto, Rais wa Arigatou na Mwenyekiti wa Bodi ya Myochikai na Mlezi-Mwenza wa Kongamano la Mtandao wa Kimataifa wa Dini kwa Watoto (Global Network of Religions for Children)  jana Juni 18, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifanya mazungumzo.

HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA KUUNDA KATIBA

Image
Tuesday, June 19, 2012 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba, Katibu wa Tume Assaa Rashid (kushoto kwa Mwenyekiti) na Dkt. Salim Ahmed Salim, Mjumbe wa Tume katika mkutano Ukumbi wa Karimjee. Ndugu Wanahabari, Nianze kwa kuwashukuru kwa kuitikia mwaliko wetu. Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilianza kazi mwanzoni mwa Mwezi Mei, 2012 na kipindi hiki tumekitumia kwa maandalizi na sasa tuko tayari kuanza awamu ya kwanza ya kazi yetu, yaani kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi. Baada ya hapo itafuata awamu ya pili ya kuandaa taarifa, mapendekezo na Rasimu ya Katiba Mpya. Baadaye Tume itakutana na Mabaraza ya Katiba na mwisho Rasimu ya Katiba itafikishwa kwenye Bunge Maalum. Kabla ya kuanza mchakato wa kushauriana na wananchi, ikiwa ni pamoja na safari za mikoani, tumeona ni muhimu na busara kukutana na nyinyi kwanza. Vyombo vya habari ni wadau wakubwa katika mchakato huu. Tume inaamini kwamba vyombo vya habari vina nafasi

WAREMBO MISS DAR INTER COLLEGE KUSUGUA KISIGINO CHA TWANGA PEPETA,CLUB BILICANAS KESHO

Image
Na Mwandishi Wetu WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss dar Intercollege 2012 jumatano ya keshjo wanatarajiwa kujivinjari katika ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas iliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.                   Shindano hilo limepangwa kufanyika Ijumaa ya Juni 22 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo msanii wa bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa kutumbuiza. Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail amesema leo kwamba, warembo hao watapata kuhudhuria onyesho maalum la bendi ya African Stars "twanga Pepeta' kupitia usiku wa Mwafrika unaorindima kila jumatano katika klabu hiyo. Dina alisema uongozi wa Bilicanas Group umewaalika warembo hao ili kuweza kuburudika pamoja na mashabiki wa muziki wa dansi nchini kwa lengo la kujipoza baada ya mazoezi yao. "Warembo wetu wamealikwa kesho pale Bilicanas ambapo bendi ya Twanga Pepeta hutumbhuiza

WASANII WA FILAMU KUNUFAIKA NA KAZI ZAO

Image
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na baadhi ya Viongozi wa mashirikisho ya wasanii wa filamu na Muziki kuhusu urasimishaji wa kazi za wasanii wa Filamu na Mziki jijini Dar es Salaam (jana). (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM) Na Concilia Niyibitanga- WHVUM Serikali imeamua kuweka mfumo rasmi utakaowawezesha Wasanii wa Filamu na Muziki nchini   kunufaika na kazi wanazozibuni na kuzitengeneza. Hayo yamesemwa leo  Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara wakati akiongea na Viongozi wa Mashirikisho  ya Wasanii wa Filamu na Muziki. Dkt. Mukangara amesema kuwa Serikali imesikia kilio cha Wasanii kwa kuirasimisha Sekta ya Filamu na Muziki ili kuondokana na kilio cha muda mrefu cha Wasanii kutonufaika na jasho lao. Amesema kuwa Serikali itatumia mfumo wa kuziwekea kazi hizo stampu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambazo zitakuwa na usalama kwa nia ya kuondokana na u

WAZIRI FENELLA AFUNGUA MASHINDANO YA UMISETA

Image
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akishuhudia gwaride la maandamano ya wanafunzi wa shule za sekondari wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) uliofanyika Kibaha Mkoani Pwani. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM) Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo,uzinduzi huo ulifanyika jana Mkoani Pwani. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM) Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na wachezaji wa Umoja wa Michezo wa shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) (hawapo pichani) wakati alipokwenda kuzindua mashindano hayo Kibaha mkoani Pwani.Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh.Jumanne Sagini. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM) Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya m

VODACOM YATOA POLE

Image
MAREHEMU WILLY EDWARD Yasema ni pigo kubwa kwa wadau wa habari ·          Yawataka wanahabari kumuenzi  Kampuni ya simu ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha ghafla cha mwanahabari mahiri Bw. Willy Ogunde Edward kilichotokea usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii. “Tunatoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu, waajiri wake na kipekee familia ya wanahabari nchini kwa kuondokewa na mpiganaji na kamanda wetu aliyekuwa sehemu muhimu ya ujenzi wa tasnia ya habari nchini.”Alisema Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza Marehemu Willy Edward alikuwa ni mdau wa habari mwenye msaada na ushauri pale anapohitajika na aliiwakilisha vyema tasnia hii ya habari tangu alipokuwa Majira mpaka kabla umauti haujamkuta akiwa Mhariri wa habari wa Jambo Leo. Marehemuatakumbukwa kwa jinsi ambavyo alikua mahiri katika kazi yake, ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na kwamba mchango wake utaendelea kuwa chachu hasa kwa viz

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUTUNZA AMANI

Image
Viongozi wa dini za Kikristo na Kiislam wametakiwa kutumia vema nyadhifa na fursa walizonazo katika kuhakikisha kuwa waamini wao wanatii sheria bila ya kushurutishwa.   Wito huo umetolewa na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi wakati alipokuwa akizindua kampeni ya utii wa Sheria Bila Shuruti kwa viongozi wa dini za Kiislam na Kikristo.   Mhe. Mwinyi amewataka viongozi hao kutumia fursa wanazozipata kupitia Ibada na Swala katika kuwahubiria waamini wao kuhusiana na suala zima la kutii Sheria bila ya kushurutishwa.   Amesema kuwa kwa kuwa viongozi hao wa dini ndio watu pekee ambao wanakuwa na watu wote katika nyakati zote za maisha yao bila kujali itikadi wala kabila, hivyo ni rahisi kwao kuwashawishi waumini hao watii sheria bila ya kushurutishwa kutokana na imani waliyonayo juu yao.   Aliongeza kuwa endapo kila kiongozi atafanikiwa kuwashawishi waamini wake watii sheria bila ya kushurutishwa, nao wa