Posts

Showing posts from June 11, 2012
Image
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimpa pole Mbunge wa  Rombo, Joseph Selasini, wodini, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, leo. Selasini amehamishiwa Muhimbili kutoka KCMC, kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mkono alioumia katika ajali aliyopata hivi karibuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita
Image
  Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kuongoza shughuli ya kuuaga mwili wa muasisi wa Chadema na Naibu Gavana wa benki kuu wa zamani, Bob Makani, leo. Wanaomkaribisha ni viongozi wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Wilbrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe.   Rais Kikwete akiwa na viongozi wa Chadema, Mbowe, Dk. Slaa na Zitto Kabwe   Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba Mpya, Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba, na Waziri Mkuu mstaafu ambaye ni Mjumbe wa Tume hiyo, Dk. Salim Ahmed Salim, wakiwasili kwenye viwanja vya Karimjee.   Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akimsalimia  Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta   Mwenyekiti wa IPP, Reginard Mengi akisalimiana na Profesa Philemon Sarungi kwenye msiba huo   Dk. Slaa akimkaribisha Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye alipowasili kwenye msiba huo kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam  Kisha akamkumbatia
Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KLABU ya soka ya Simba imepokea kwa furaha taarifa kwamba Rais wa Shirikisho la Mpira was Miguu Tanzania (TFF), Leodger Chila Tenga, ameagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na namna mchezaji wa Simba na Taifa Stars, Kelvin Patrick Yondani, alivyoondoka kambini usiku wa kuamkia Juni 7 mwaka huu. Katika barua ambayo Tenga ameiandikia Simba, ameahidi kwamba uchunguzi utafanyika katika maeneo makuu mawili. Mosi, iwapo ni kweli Yondani aliondoka kambini usiku, pili iwapo aliondoka kwa ruhusa maalumu au alitoroka.  Tenga ameahidi kwamba kama ikibainika kwamba aliondoka bila ruhusa, basi hatua zitachukuliwa kwa wote waliohusika chini ya taratibu za maadili kwa wachezaji  (Players Code of Conduct). Kutokana na kauli hiyo ya Tenga, uongozi wa Simba umeamua sasa kwamba hautozungumza lolote kuhusiana na masuala ya Yondani. Tayari timu imewasilisha vielelezo vyake TFF na kote kwingine ambako suala hilo linaweza kufika. K

EXTRA BENDI

Image
MWENYEKITI wa chama cha waandishi wa habari za michezo Tanznia (TASWA) Juma Pinto (Kati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuzo za wanamichezo bora zibnazotolewa na chama hicho, kulia ni Katibu Mkuu wa Taswa Amiri Mhando na kushoto no meneja Uhusiano wa SBL Iman Lwiga, Bendi ya  muziki wa dansi ya Extra Bongo inatarajiwa kutumbuiza katika hafla hiyo itakayofanyika JUni 14 katika ukumbi wa Diamond Jubillee VIP.

MASHUJAA BENDI

Image
Rais wa Mashujaa Musica, Charlz Baba BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa Wanaposoposo' Ijumaa ya Juni 15 wameandaa shindano maalum la mavazi ya kizamani. Wapenzi wa muziki wakaovaa mavazi ya kizamani watapata zawadi shindano litakalofanyika kwenye ukumbi wa Business Park Dar es Salaam. Meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter, alisema kuwa watu watakaoingia katikan onesho la bendi hiyo  watapata zawadi. Alisema wamejipanga kuhakikisha wanatoa zawadi nzuri kwa wapenzi watakakuja katika onesho hilo wakiwa na mavazi ya kizamani, ili na vijana watambue kama nguo za zamani zinaheshima na kutambulika. Sospeter alisema kila atakayeingia akiwa amevaa vazi la kizamani atakuwa amejiingia katika kushindania zawadi hizo ambazo ni simu za mkononi na pesa taslim. "Tumejipanga kuhakikisha tunarudisha mavazi ya kizamani ili vijana watambue zamani kulikuwa na mavazi yake ambayo tufauti na sasa na yalikuwa kivuti kikubwa kuliko sasa kila mtu anaamua ajivalie kivvyake"alisema Sop

WAKAZI WA IRINGA WAKISHUHUDIA UZINDUZI WA HUDUMA MPYA YA AIRTEL JIUNGE NA SUPA 5

Image
Wasanii chipukizi wa muziki wa bongofleva,waitwao Wavuka Boada wakilishambulia jukwaa mbele ya umati wa wakazi wa Iringa waliojitokeza kwa wingi jana jioni kwenye uwanja wa Mwembe Togwa, mjini humo wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya airtel Supa5 yenye lengo la kutoa huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel.huduma hiyo itaendelea kutambulishwa tena katika mkoa wa Arusha na baadaye jijini Mwanza. Mmoja wa wakazi wa Iringa aitwaye Theresia Mifwa akikabidhiwa simu ya mkononi aina ya sumsung na Meneja Mahusiano wa  Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando, mara baada ya kuichambua vyema huduma ya Jiunge na Supa5 kwa ufasaha ,wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5 uliyofanyika jana kwenye uwanja wa Mwembe Togwa mkoani Iringa. Airtel Jiunge na Supa5 Ilizinduliwa kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Ukitaka kujiunga na huduma hiyo ANDIKA SMS YENYE NENO ‘WIKI’  AU WIKI UTUME KWENDA 15548. Kundi la wasani mahiri w

MAKAMUZI YA MACHOZI BENDI NA BARNABA YALIVYOFANA MWANZA

Image
Langoni ilikuwa unakutana na CD original za Lady jay Dee na Machozi Band   Ze dadaz wakipata flash juu ya red carpet kabla ya kuingia ukumbini, katikati ni Rhoda John, Asha Kissy na mashost zao.     Kutana na Blogger Allan Kisoi pale kati akipata flash na Antonio Nuggas, Barnaba na Hellen. Machozi Band katika Stage la Gold Crest Manza.  Mc wa shughuli usiku huo Albert G. Sengo toka Clouds Fm 88.1 Mwanza Dance la Machozi Band likiendelea. Mduara na mauno yamekolea anatunukishwa mtu kitu cha msimbazi. Mikono kwenye pembejeo na zana maho kwenye kamera na Machozi Band. Mwimbaji mwenye umri mdogo kuliko wote hatari kwenye stage Sam Machozi. Sutumuka ya kwaitoZZZZzzz.com Dance la kwaito. Barnaba alichengua vilivyo. Hadi ladiZ wanakiri kuwa Barnaba ni 'moTTo' Nishakwambia kuwa Barnaba ni 'Motto'  Mwanamuziki haitwi 'Mwanamuziki' bila kujua kutumia japo chombo kimoja wapo cha muziki. Familia kama kawaZZz.. W
Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal pamoja na Mama Salma Kikwete leo waliungana na viongozi wa CHADEMA na viongozi wengine wa kitaifa kutoa heshima zao za mwisho kwa mmoja wa waasisi wa CHADEMA marehemu Bob Makani ambayepia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo ya Naibu Gavana wa Benki kuu katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.(picha zote na Freddy Maro) Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe wakati wa kuaga mwili wa Muasisi wa chama cha CHADEMA marehemu Bob Makani Rais Dkt.Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wakibeba jeneza la marehemu Bob Makani Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za Mwisho Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiteta jambo na mjumbe wa tume ya kukusanya maoni juu ya katiba Prof.Mwesiga Baregu katika viwanja vya Karimjee leo. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ak

TBL YATOA MILIONI 200

Image
KAMPUNI ya Tanzania Breweriers Limited(TBL) imetoa ruzuku ya vitendea kazi vyenye gharama ya shilingi milioni mia mbili kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa Tanzania nzima huku kanda ya kaskazini ikikabidhiwa vitendeakazi vyenye gharama ya shilingi milioni 50 lengo likiwa ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuzisaidia jamii mbali mbali zinazowazunguka. Akikabidhi vitendea kaz i hivyo kwa wafanyabiashara wa kanda ya kaskazini katika tamasha lililofanyika mjini hapa meneja wa bia ya Safari larger Bw. Oscar Shelukindo alisema kuwa kampuni hiyo imejiwekea mpango wa kuhakikisha kuwa wanawasidia wajasiriamali Tanzania nzima ili waweze kujikwamua katika hali ngumu ya kiumskini. Alisema kuwa vifaa hivyo walivyovitoa kwa wafanyabiashara hao ni vitendea kazi ambavyo vitawasaidia kutumika katika biashara zao mbali mbali wanazoziendesha kwa kuwa wako watu wana malengo na maono mazuri ya baishara lakini wanashindwa kufikia malengo kwa ajili ya kukosa vitendea kazi.

30 WAINGIA KWENYE KOZI YA KUJENGA AFYA

Image
Walimu 18 wa shule za msingi na makocha 12 wa mpira wa miguu wanashiriki kozi ya mpango maalumu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa ajili ya kujenga afya kupitia mpira wa miguu. Kozi hiyo ya siku tano inayoitwa FIFA 11 for Health imeanza leo (Juni 11 mwaka huu) kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na itamalizika Juni 15 mwaka huu. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wakufunzi kutoka FIFA ambapo ujumbe katika 11 for Health ni 1. Cheza mpira, 2. heshimu wasichana na wanawake, 3. jikinge na virusi vya Ukimwi (HIV), 4. epuka dawa za kulevya, pombe na sigara, 5. tumia neti zenye viuatilifu, 6. nawa mikono yako, 7. kunywa maji salama, 8. kula chakula chenye mpangilio, 9. pata chanjo, 10. tumia dawa sahihi na 11. cheza mchezo mzuri. Walimu hao kutoka shule za Mkoa wa Dar es Salaam ni Aloyce Rutta (Montfort, Temeke), David Kazinge (Temeke, Temeke), Rajabu Ased (Mtoni Kijichi, Temeke), Mathew Kambona (Mji Mwema, Temeke), R
Image
Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia (The Scorpions) iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, D ar es Salaam imeingiza sh. 124,038,000. Mapato hayo yametokana na washabiki 31,122 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Washabiki 25,901 walikata tiketi za sh. 3,000. Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 18,921,050.85 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 6,555,000), bonasi kwa Taifa Stars (sh. 15,767,542.37), waamuzi (sh. 13,372,000), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000), umeme (sh. 300,000) na mafuta ya jenereta (sh. 200,000). Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 12,834,481, asilimia 10 ya uwanja sh. 6,417,241, asilimia 5 ya Shiriki

JK AONGOZA KUAGA MWILI WA BOB MAKANI

Image
Rais Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wa Rais wa pili kutoka kushoto na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wa mwisho kushoto wakiongoza waombolezaji  kwenye viwanja vya Karimjee wakati Mwili wa muasisi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mzee Bob Makani ulipoagwa leo jijini Dar es salaam. Mwili wa Marehemu Bob Makani ukiwa umewekwa eneo maalum tayari kwa kuaga mwili huo leo kwenye viwanja vya Karimjee. Mwili wa Marehemu Bob Makani ukiteremshwa kwenyegari ili kuwekwa eneo hilo kwa ajili ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho. Mwili ukiwekwa tayari kwa ajili ya waombolezaji kuuaga rasmi kabla ya kuzikwa huko Shinyanga .