Posts

Showing posts from August 6, 2012

MSAADA KWADELO

Image
  Mama Maria akimkabidhi funguo za trekta moja kati ya kumi aliyokabidhi, mmoja wa wakulima hao Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni Sheikh wa Kata ya Kwadelo .   Mkazi wa kijiji cha Kwadelo, Maulid Msema akipokea funguo moja kati ya 10 za Matrekta yaliyokabidhiwa na Mama Maria Nyerere kwa ajili ya wakulima wa kijiji hicho  kilichopo wilayani Kondoa, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo kijijini hapo, katika hafla iliyofanyika Msasani jijini Dar es Salaam jana. Kushoto anayeshuhudia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati.   Kisha Kariati akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Nyerere kama shukurani ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa Mwalimu mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo.   Halafu akamkabidhi mkoba wa safari kama akitaka kwenda Butiama kijijini kwake   Omary Kariati diwani wa kata ya kwadelo,wilayani kondoa mkoa wa Dodoma akizungumza neno la kufungua shughuli. Kulia ni Mama Nyerere akimsikiliza kwa

JANUARI MAKAMBA AONGOZA MKUTANO WA WANABUMBULI JIJINI DAR ES SALAAM JANA

Image
Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akiongea na wakazi kutoka wilaya ya  Lushoto jimbo la Bumbuli katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo mkutano huo ulikuwa  unajadili maendeleo ya jimbo la  Bumbuli na kutambulisha shirika la maendeleo la  Bumbuli, January Makamba amesema katika kipindi cha mwaka 2011-2012 kiwango cha elimu ya wilaya hiyo imekuwa chini na kusababisha vijana wengi katika mkoa wa Tanga kuwa na sifa ya kuuza chipsi na kubeba mizigo badala ya kufanya kazi kwenye makampuni . Mkurugenzi wa shirika la Bumbuli Bw. Najim Msenga (kushoto), mwenyekiti mteule wilaya ya Bumbuli Bw. Amiri Sheiza (kulia)katibu wa CCM wilaya ya Lushoto Bw. Loth Ole Lemeirut (katikati)wakijadiliana jambo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo jana Wakazi kutoka jimbo la bumbuli wakiwa katika mkutano huo wa kujadili maendeleo ya wilaya ya Bumbuli Kikundi cha ngoma kijulikanacho Mount  Usambara Voice kikitoa burudani katika mkutano huo

NANE NANE DODOMA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua  maoni kutoka kwa   Mhasibu wa Wizara ya Fedha Abbas Myeto(kulia)kuhusu taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wa umma wanapostaafu . Mkuu huyo wa Nkoa wa Singida aliomba ufafanuzi huyo leo alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.   Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua jana mjini Dodoma kutoka kwa watendaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) kwanini kuna utofauti wa ubora katika bendera ya Taifa ya kuweka katika magari kwa viongozi. Mkuu Mkoa huyo aliuliza swali hilo leo alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma. Aliyeshika bendera ndogo ya taifa ni Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia) .  Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kushoto) akipata maelezo mafupi  jinsi