MSAADA KWADELO


 Mama Maria akimkabidhi funguo za trekta moja kati ya kumi aliyokabidhi, mmoja wa wakulima hao Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni Sheikh wa Kata ya Kwadelo.
 Mkazi wa kijiji cha Kwadelo, Maulid Msema akipokea funguo moja kati ya 10 za Matrekta yaliyokabidhiwa na Mama Maria Nyerere kwa ajili ya wakulima wa kijiji hicho  kilichopo wilayani Kondoa, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo kijijini hapo, katika hafla iliyofanyika Msasani jijini Dar es Salaam jana. Kushoto anayeshuhudia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati.
 Kisha Kariati akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Nyerere kama shukurani ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa Mwalimu mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo.
  Halafu akamkabidhi mkoba wa safari kama akitaka kwenda Butiama kijijini kwake
  Omary Kariati diwani wa kata ya kwadelo,wilayani kondoa mkoa wa Dodoma akizungumza neno la kufungua shughuli. Kulia ni Mama Nyerere akimsikiliza kwa makini kama anavyoonekana kwenye picha.
 Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, Maria Nyerere, akimkaribisha, diwani wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa mkoani  Dodoma, Alhaji Omar Kariati, wakati diwani huyo na ujumbe wake wa wakulima kumi, walipofika nyumbani kwa Mama Nyerere kwa ajili ya kukabidhiwa trekta kumi kwa wakulima hao, katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam, jana.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA