Posts

Showing posts from June 14, 2012

HOTUBA YA BAJETI YA MWAKA 2012/2013

1.          Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liweze kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013.  Pamoja na hotuba hii, nimewasilisha vitabu vinne vya Bajeti vinavyoelezea takwimu mbalimbali za Bajeti. Kitabu cha Kwanza kinaelezea makisio ya mapato.   Kitabu cha Pili kinaelezea makisio ya matumizi ya kawaida kwa Wizara, Idara zinazojitegemea; Taasisi na Wakala wa Serikali; cha Tatu kinahusu makisio ya matumizi ya kawaida kwa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na cha Nne kinaelezea makadirio ya matumizi ya maendeleo kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za Serikali; Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2012 ambao ni sehemu ya Bajeti hii. 2.  Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nitumie fursa hii kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa imani kubwa aliyon