Posts

Showing posts from August 5, 2012
Image
Said Bahanuzi ni mshambuliaji mahiri wa timu ya Yanga ya nchini Tanzania jana alithibitisha kwamba yeye ni mchezaji halali wa Yanga na ataendelea kuwa mchezaji wa Yanga kwa muda wa miaka miwili kwa tamko hilo Bahanuzi ameondoa utata uliokuwa unaanza kuvuma jijini Dar Es Salaam na nchi kwa ujumla kwamba huenda mchezaji huyo amehamia timu pinzani ya Simba ambao haikufanya vizuri katika mashindano ya hivi karibuni ya Kagame Cup iliyoshirikisha timu mbali mbali za klabu za afrika mashariki na kati na ikiwemo kuiwakilisha timu ngeni ya kutoka Congo ya Vita FC ingawa timu hiyo ilishika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.

TENGA KUFUNGUA KOZI YA UONGOZI YA FIFA

Image
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na pia Rais wa shirikisho la CECAFA Bw. Leodiger Tenga anatarajia kufungua Kozi ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoanza kesho (Agosti 6 mwaka huu) Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.

MKUU WA MKOA ATOA CHANGAMOTO

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida ,Dr.   Parseko Kone (kushoto) akitoa changamoto kwa watumishi wa Chuo cha Mipango cha Dodoma kuwa na mitaala ambayo itawaandaa wananchi kuanzia ngazi ya chini juu ya kuwa na mipango mizuri ya matumzi bora ya ardhi ili kukabiliana na ongezeko la watu nchini. Mkuu Mkoa huyo alitoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.

UWAMADAMUDA

Image
  UMOJA wa Wamiliki wa Maduka ya Dawa Muhimu Dar es salaam (Uwamadamuda), umesema pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kusitisha zoezi la Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),   bado unaitaka   serikali kutafuta suluhu ya kudumu. Hatua hiyo imekuja baada muongozo mpya wa TFDA unaowataka   wamiliki hao wa maduka ya dawa kuhamia   pembezoni mwa jijji Dar es Salaam.   Akizungumza na wandishi wa habari jijini jana, Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Juma Maganga, alisema waziri anapaswa kutoa suluhu ya kudumu na siyo kwa muda kama alivyoagiza, ili wamiliki hao wafanye biashara zao kwa amani.   “Kwa kuwa serikali yetu ni sikivu na inajali raia wake hivyo tunamsisitiza Waziri , Hussein Mwinyi kuwa tunategemea suluhu ya kudumu atakayotoa itaondoa ubaguzi na ukandamizaji kwa wenye mitaji midogo”alisema Maganga   Maganga alisema iwapo Wizara itashindwa kutoa uwamuzi wa kudumu kuhusu muongozo huo kuna hatari mvutano ukaendelea na hatimaye kufikishana kwenye vyombo vy

FOMU ZA KUGOMBEA NAFASI YA UONGOZI CCM TAIFA ZAANZA KURUDISHWA

Image
Mgombea nafasi ya Mwenyekiti UWT Taifa Bi, Halima Mohamed Mamuya  kulia akirudisha fomu ya kuomba kugombea nafasi hiyo kwa Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni  UWT Makao Makuu Bi Riziki Kingwande Dar es salaam leo.   Pia leo meya wa wilaya ya Ilala Mh.Jerry Silaa naye amechukua fomu ya kuwania nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya UVCCM.