UWAMADAMUDA
UMOJA wa Wamiliki wa Maduka
ya Dawa Muhimu Dar es salaam (Uwamadamuda), umesema pamoja na Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii kusitisha zoezi la Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), bado unaitaka serikali kutafuta suluhu ya kudumu.
Hatua hiyo imekuja baada
muongozo mpya wa TFDA unaowataka
wamiliki hao wa maduka ya dawa kuhamia pembezoni mwa jijji Dar es Salaam.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini jana, Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Juma Maganga, alisema
waziri anapaswa kutoa suluhu ya kudumu na siyo kwa muda kama alivyoagiza, ili
wamiliki hao wafanye biashara zao kwa amani.
“Kwa kuwa serikali yetu ni
sikivu na inajali raia wake hivyo tunamsisitiza Waziri , Hussein Mwinyi kuwa
tunategemea suluhu ya kudumu atakayotoa itaondoa ubaguzi na ukandamizaji kwa
wenye mitaji midogo”alisema Maganga