Posts

Showing posts from October 20, 2012

TANZANIA KUTOUZA GESI ASILIA NJE YA NCHI HADI IJITOSHELEZE MAHITAJI YA NDANI

Image
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akongea wakati wa mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini. Nyuma yake mwenye laptop ni Meneja wa Sekta Kupunguza Umaskini na Kusimamia Maendeleo ukanda wa Afrika wa Benki ya Dunia Dkt Albert Zeufack, akiwa ameongozana na mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na Timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo na  inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani ****** YALIYOSEMWA NA KATIBU MKUU KIONGOZI LEO WAKATI  WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI             Katika miaka ya karibuni kumekuwepo kwa ugunduzi mkubwa wa gesi asili nchini Tanzania katika maeneo ya mwambao na maeneo ya kina kirefu cha bahari ambapo mpaka sasa jumla ya futi za ujazo trilioni 33 zimegunduliwa. Kazi ya utafutaji inaendelea na upo uwezekano wa ugunduzi zaidi.             Kiasi hicho kilich

Kamati ya Bunge yatembelea Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere

Image
Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam linavyoonekana kwa nje baada ya kukamilika. Jengo hilo linalomilikiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  lipo Makutano ya Barabara za Shaaban Robert na Garden Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule (kushoto) akimkaribisha Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb.), Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Katibu Mkuu, Bw. Haule akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere walipokitembelea hivi karibuni. Wajumbe wa Kamati ya NUU na Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati akiwakaribisha. Mhe. Azzan akizungumza na Wajum

ZOEZI LA KUKAMATA MAGARI YA SERIKALI YANAYOTUMIA NAMBA BINAFSI KUFANYIKA NCHI NZIMA

Image
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kusisitiza  utaratibu wa usajili wa magari   ya Umma unafuatwa na kutafanyika zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote. Serikali imetoa muda hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na namba  za kiraia, yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma .  Baada ya hapo Operesheni hiyo iitakamata magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma,Vilevile kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST, PT, MT,JW, DFP, CW, SM na ,SU.Hadi sasa serikali imesajili vyombo vya moto,123,431 yakiwemo magari,,pikipiki,bajaj na mitambo ya umma. Pamoja nae ni kamansda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi, James Mpinga

SHEIKH FARID AREJEA NYUMBANI KWAKE SALAMA

Image
Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho visiwani Zanzibar, Sheikh Farid, (Wapili kushoto), akipiga picha ya ukumbusho na familia yake mara baada ya kjuwasili nyumbani kutoka kusikojulikana, Ijumaa Oktoba 19, 2012 Sheikh Farid, akipokewa na ndugu na jamaa nyumbani kwake Sheikh Farid, na baadhi ya wafuasi wake, wakiomba dua nyumbani kwake mara baada ya kupatikana, Ijumaa Oktoba 19, 2012 Kuna habari kuwa kiongozi wa Jumuiyab ya Uamsho, kisiwani Unguja, Zanzibar, Sheikh Farid amepatikana nay u salama salimin. Picha za mitandao zinaonhyesha sheikg huyo mwenye msimamo makali alionekana akilakiwa na watu b waliotajwa kuwa ni ndugu na jamaa, ambapo picha nyingine zinaonyesdha akiwa na familia yake na moja ikionyesha akiomba dua nyumbani kwake. Kwa mjujibu wa taarifa za mkitandao, Sheikh huyo aliyetoweka tangu Oktoba 16, 2012 na kuonekana tena Oktoba 19, 2012 majira ya jioni, alisema, “alichukuliwa na watu waliojitambulisha kwake, kuwa ni askari polisi na baadhi yao wakiwa n

WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA MSHINDI WA KWANZA WA SHUGHULI ZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2012 KANDA YA IV ILIYOSHINDANISHA MIKOA MITANO

Image
Mkuu wa Wilaya mpya ya Kalambo Moshi Chang’a ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwenye shughuli za kuzima Mwenge wa Uhuru Mkoani Shinyanga akionyesha Kikombe na Cheti alichokabidhiwa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama zawadi ya ushindi kwa Wilaya yake baada ya kushika nafasi ya kwanza katika shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake alipowasili jana Mkoani Rukwa aikitokea Shinyanga. Wawakilishi wa Mkoa wa Rukwa waliokwenda kushiriki kuzima mwenge wa uhuru Mkoani Shinyanga na kurudi na kikombe cha ushindi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a, mratibu wa Mwenge Kimkoa Abubakar Serungwe na Katibu wa Mkuu wa Mkoan Frank Mateny wakipewa mapokezi na uongozi na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa. Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akipokea kikombe hicho c

Watu sita wamekamatwa kwa tuhuma za kumuua Afisa wa Polisi marehemu Said Abdulrahman juzi

Image
Kamishna wa Polisi Zanzibar,Mussa Ali Mussa aliwaambia waandishi wa habari kwamba watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) walikamatwa sehemu tofauti, mmoja amekamatwa Kisiwa kidogo cha Tumbatu, wa pili maeneo ya Mjini Unguja,mtuhumiwa wa tatu alikamatwa ofisi za Idara ya Uhamiaji alikokwenda kushughulikia hati ya kusafiria ili aweze kutoroka hapa nchini. Kamishna Mussa alisema watuhumiwa wengine watatu wamekamatwa Mkoani Tanga ambako walikimbilia kujificha baada ya kufanya mauaji ya Afisa Polisi Koplo Said Abdulrahman.  “Watu hao walitorokea huko na tunaendelea kuwahoji…tunawashukuru wananchi kwa ushirikiano wao mkubwa uliotuwezesha kufanikisha ukamataji huo,tunavishukuru vikundi vya ulinzi shirikishi vilivyo katika Shehia mbalimbali kwa kuimarisha ulinzi wa maeneo yao katika kipindi chote cha fujo na vurugu hizo” Alisema Kamishna Mussa.  Kamishna Mussa aliwaambia waandishi wa habari kuwa Polisi hivi sasa inaendelea kuwahoji Sheikh Fa

SERIKALI YA ZANZIBAR YAAHIDI KUTOA USHIRIKIANO NA UNDP KATIKA KUDUMISHA USTAWI WA JAMII.

Image
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpongeza Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Alberic Kacou kufuatia Umoja wa Mataifa kutimiza Miaka 67 tokea kuasisiwa kwake. Pongezi hizo amezitoa Ofisini kwake katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi uliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa aliyepo Tanzania Bw. Alberic Kacou akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

KASI YA TEKNOLOJIA YAONGEZEKA KWA NCHI ZA AFRICA

Image
KASI YA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA KWA NCHI ZA AFRIKA YAONGEZEKA KASI ya Maendeleo ya Teknolojia kwa nchi za Afrika ni kubwa hali inayosababisha baadhi ya Mashirika ya Viwango nayo kubuni mbinu zitakazoendana na mabadiliko hayo . Hayo yalisemwa na Mratibu wa Masuala ya Viwango  vya Kimataifa kutoka Shirika la Viwango Tanzania wakati alipokuwa akizungumzia na waandishi wa habari juu  ya Mkutano wa Baraza la Mashirika ya Viwango kwa Nchi za Afrika (ARSO) unatakofanyika Oktoba 22 hadi 24 Jijini Arusha na kushirikisha Nchi 12 kutoka Bara la Afrika. Bw.Mnunguli amesema hivi sasa kasi ya ukuaji wa teknolojia ni kubwa katika nchi za Afrika hivyo pia kasi hiyo ni changamoto kubwa kwa mashirika ya viwango na kuongeza kuwa mkutano huo utajadili changamoto za viwango pamoja na kubadilishana uzoefu kwa wataalam wa viwango katika kila nchi za Afrika. Aidha amesema mkutano huo utajadili changamoto za viwango pamoja na kuweka mikakati  itakayoweze