KASI YA TEKNOLOJIA YAONGEZEKA KWA NCHI ZA AFRICA

KASI YA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA KWA NCHI ZA AFRIKA YAONGEZEKA



KASI ya Maendeleo ya Teknolojia kwa nchi za Afrika ni kubwa hali inayosababisha baadhi ya Mashirika ya Viwango nayo kubuni mbinu zitakazoendana na mabadiliko hayo .
Hayo yalisemwa na Mratibu wa Masuala ya Viwango  vya Kimataifa kutoka Shirika la Viwango Tanzania
wakati alipokuwa akizungumzia na waandishi wa habari juu  ya Mkutano wa Baraza la Mashirika ya Viwango kwa Nchi za Afrika (ARSO) unatakofanyika Oktoba 22 hadi 24 Jijini Arusha na kushirikisha Nchi 12 kutoka Bara la Afrika.
Bw.Mnunguli amesema hivi sasa kasi ya ukuaji wa teknolojia ni kubwa katika nchi za Afrika hivyo pia kasi hiyo ni changamoto kubwa kwa mashirika ya viwango na kuongeza kuwa mkutano huo utajadili changamoto za viwango pamoja na kubadilishana uzoefu kwa wataalam wa viwango katika kila nchi za Afrika.
Aidha amesema mkutano huo utajadili changamoto za viwango pamoja na kuweka mikakati  itakayowezesha wajasiriamali ,wafanyabiashara na  kupata maendeleo kutokana na bidhaa wanazozalisha.
Amesema katika mkutano huo watapitia katiba pamoja na kuangalia uwezekano wa kubadilishana wataalam ambao wataweza kufanya kazi kwa muda Nchini Kenya lengo ni kuboresha matatizo ya viwango.
Mkutano huo  utajadili changamoto mbalimbali zinazokumba mashirika ya viwango ya TBS katika nchi za Afrika pia tutahakikisha wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara wanaondokana na vikwazo wanavyokutana navyo.
Naye  Afisa Viwango kutoka TBS, bw.Rocda Andusamile alisema Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Grace Mapunjo anatarajia kufungua mkutano huo  na kuongeza kuwa mkutano huo utashirikisha nchi za Misri, Malawi, Nigeria, Kenya, Sudani, Rwanda, Ghana, Cameroon, Afrika Kusini, Tunisia,Kongo,  Sudan,Madagascar na Gabon

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA