Posts

Showing posts from April 15, 2013

KAMATI YAUNDWA UJENZI WA JENGO LA YANGA

Image
Ndugu Ridhiwani Kikwete, mwenyekiti wa kamati hiyo ya ujenzi wa majengo ya Yanga lililopo mtaa wa Mafia na Nyamwezi ameunda kamati ya wajumbe tisa(9) watakaosimamia ujenzi wa majengo hayo huko Zanzibar.   Huku wajumbe wengine ni jaji mstaafu John Mkwawa, Naibu waziri wa wizara ya Miundombinu ya serikali ya mapinduzi Zanzibar,Allan Magoma,Charles Palapala,Izack Chanje na wakili Mavalle Msemo.

RAIS WA ZANZIBAR AKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA.

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt. Ali Mohamedi Shein leo amekutana na viongozi wa wizara ya Miundombinu na Mawasiliano katika kuangalia muenendo wa kazi katika wizara hiyo katika ukumbi wa mikutano Ikulu mjini Zanzibar.

SHULE JIJINI DAR YATEKETEA KWA MOTO

Image
Shule moja ya sekondari jijini Dar es Salaam imeteketea kwa moto, shule hiyo ya sekondari ni Wazo hill nje kidogo ya jiji hilo ambapo hasara za mamilioni zimeripotiwa kupotea. Moto huo uliozuka mapema asubuhi, inadaiwa ulisababishwa na hitilafu ya umeme.

BILIONEA SAMBEKE AFARIKI DUNIA

Image
Hii ndio ndege ambayo imesababisha kifo cha  mfanyabiashara maarufu jijini Arusha na nchini kwa ujumla ndugu Joseph Sambeke(49) ambaye alifariki njiani wakati akipelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi mazishi yake yamepangwa kufanyika Alhamisi katika eneo la Karanga,Moshi.