Posts

Showing posts from June 22, 2012
LEO NI GERMANY VS GREECE  NANI ATASHINDA

Mamilioni ya Wamisri wakusanyika Cairo katika Medani ya Tahrir

Image
  Mamilioni ya wananchi wa Misri hii leo wameendelea kukukusanyika katika Medani ya Tahrir mjini Cairo baada ya Swala ya Ijumaa, kulalamikia hatua ya Baraza la Kijeshi linaotawala nchini humo ya kung'ang'ania madaraka. Wananchi hao pia wanalalamikia hatua ya wanajeshi hao ya kuchelewesha kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni. Aidha Wamisri wamelaani kupunguzwa uwezo wa rais wa nchi na uwezekano wa wanajeshi hao kufanya mapinduzi dhidi ya mwenendo mzima wa demokrasia nchini humo. Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, Baraza la Kijeshi la Misri (SCAF) limesema kwamba litatumia vikosi vya jeshi dhidi ya waandamanaji ambao wamejikusanya katika Medani ya Tahrir kwa madai ya kulinda maslahi ya taifa. Aidha baraza hilo limeikosoa harakati ya Ikhwanul Muslimin eti kwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais mapema na kudai kuwa kutangaza matokeo hayo yasiyo rasmi kumesababisha mgawanyiko na vurugu nchini Misri.

WANAFUNZI WA MAABALA KIFUPI DMLS NA WANAFUNZI WENGINE WACHANGIA DAMU LEO- MUHIMBILI

Image
Mtaalamu wa Maabara kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Eliza Mgaya, akiweka vizuri mfuko wa damu kutoka kwa mwanafunzi wa Chuo Cha Afya Muhimbili Paul Boniface, ambaye ameshiriki kwenye zoezi la kujitolea damu linaloenda sambamba na upimaji wa bure wa magonjwa mbalimbali, linaloratibiwa na Wanafunzi wanao hitimu mafunzo ya Maabara kwenye Chuo cha Maabara Muhimbili Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakijiorodhesha Hospitali ya taifa Muhimbili ili kuweza kupata huduma za bure za kupima afya zao, zoezi hilo linaratibiwa na wanafunzi wa maabara wanao maliza kwenye chuo cha maabara cha Muhimbili. Wanafunzi wanaohitimu ngazi za Astashada na Stashahada za Maabara kwenye Chuo cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambao ndio walioandaa zoezi la upimaji afya linaloendelea hapa Muhimbili wakifuatilia hotuba mbalimbali kwenye hafla yao ya kuhitimu masomo ambapo wanaelekea kuhitimisha masomo hayo.

STIKA MPYA

Image
 Kamanda Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kuzindua kampeni ya kubandika stika zenye namba za simu za vituo mbalimbali ambazo abiria watazitumia kwaajili ya kutoa taarifa za usalama na matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani. Kampeni hiyo inadhaminiwa na benki ya posta (TPB) Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi  akibandika sitika hizo. Mmoja wa Madereva waliokabidhiwa Stika hizo kwaajili ya kuzibandika kwenye magari .

Wabunge watahiriwa kupunguza HIV

Image
Wabunge karibu 10 nchini Zimbabwe wametahiriwa kama moja wapo ya hatua zao ya kukabiliana na kusambaa kwa virisi vya Ukimwi nchini humo Hazahanati walipotahiriwa wabunge Zimbabwe Njee ya majengo ya bunge mjini Harare , kulijengwa zahanati ndogo kwa sababu ya shuhuli hizo za kuwapasha wabunge tohara. Blessing Chebundo, ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wanaopambana na Ukimwi amesema nia yake hasa ya yeye kuamua kupashwa tohara ni kuchochea wanaume nchini Zimbabwe kutairiwa. Bwana Chebundo anasema kuna wabunge zaidi ya 120 na wafanyikazi wa bungeni ambao wameonyrsha nia yao ya kutairiwa. Shirika la afya duniani WHO linasema kupasha tohara kunapunguza atari ya wanaume kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa asilimia 60. Zimbabwe ni moja wapo wa mataifa 13 barani Afrika ambapo mwaka wa 2007 shirika la WHO inasema kuna haja kub

RAIS KIKWETE AREJEA DAR ES SALAAM

Image
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Mecky Sadik leo katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea Dodoma katika ziara ya kikazi PICHA NA IKULU

MISRI YAOMBA KUCHEZA NGORO NGORO HEROES

Image
Chama cha Mpira wa Miguu Misri (EFA) kimeomba mechi mbili za kirafiki kwa timu yao ya vijana na timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania (Ngorongoro Heroes).        EFA imeomba mechi hizo zichezwe Julai 3 na Julai 5 mwaka huu kwa masharti maalumu. Ikiwa zitachezwa Misri, mwenyeji (EFA) atagharamia Ngorongoro Heroes kwa malazi, chakula, usafiri wa ndani na sehemu ya kufanyia mazoezi. Ikiwa mechi hizo zitachezwa Dar es Salaam, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaigharamia timu ya Misri kwa malazi, chakula, usafiri wa ndani na sehemu ya mazoezi. Hivyo kila timu itajigharamia kwa usafiri wa ndege na posho kwa timu yake.   Sekretarieti ya TFF inafanya uchambuzi wa gharama ili kujua ipi ni nafuu kabla ya kufanya uamuzi wa wapi mechi hizo zichezwe.   Ngorongoro Heroes imeingia raundi ya pili ya michuano ya Afrika ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Algeria baada ya kuitoa Sudan katika raundi ya kwanza.
Image