Posts

Showing posts from January 10, 2013

TIGO YAZINDUA HUDUMA YAKE MPYA YA TIGO TIME KWA WATEJA WAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Image
  Meneja mbunifu wa ofa za Tigo,Jacqueline Nnunduma akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema jana asubuhi kwenye hoteli ya Serena,kuhusiana na uzinduzi wa huduma yao mpya iitwayo Tigo Time,kushoto ni kwake ni Mwakilishi wa kampuni ya Frontline Portel Novelli Elias Bandeke Meneja wa Ofa za Tigo,Suleiman Bushagama akitoa ufafanuzi zaidi mbele ya Wanahabari kuhusiana na kampuni hiyo kutambulisha huduma mpya kwa wateja ijulikanayo kama Tigo Time, ambayo inatoa punguzo kubwa sana la gharama ya kupiga simu masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7 ikitegemeana na muda na wakati wa siku na eneo mteja atakalokuwa.

Wanafunzi walioongoza mtihani wa taifa wa darasa la saba wa mwaka 2012 Hapa

Image
 Wanafunzi walioongoza mtihani wa taifa wa darasa la saba wa mwaka 2012, Janeth Kijazi (kushoto) Justina Kalala (katikati)na Kellen Mudogo wakiwa shule ya sekondari ya wasichana, St Marian Bagamoyo, jana, walikoanza kidato cha kwanza. Wanafunzi hao walihitimu elimu ya msingi katika Shule ya Tusiime ya jijini Dar es Salaam.

Lowassa avipiga jeki vikundi saba vya vikoba Monduli mjini

Image
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amevipatia vukundi saba vya Vikoba vilivyopo Wilayani Monduli,kiasi cha shilingi milioni nane kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao.Lowassa amesema yeye ni mkereketwa mkubwa wa Vikoba huku akisisitiza kuwa ni chachu ya maendeleo na kumkwamua mtanzania kutoka katika umasikini. kila kikundi kimepata shilingi millioni moja ambapo kikundi kilichofanya vizuri kimeongezewa shilingi millioni moja zaidi.Pichani ni Mh. Lowassa akikabidhiwa zawadi na mwenyekiti wa Vikoba Kijiji cha Monduli Juu,Dawson Kaaya wakati viongozi wa vikundi hivyo walipomtembelea nyumbani kwake Monduli. Mmoja wa viongozi wa vikundi vya vikoba Kijiji cha Monduli Mjini akisoma risala mbele ya Mh Lowassa. Baadhi ya wanavikoba wa Monduli Mjini wakimsikiliza Mh. Lowassa. Mhe Edward Lowassa akipewa zawadi na Bi Arafa Ismaild kutoka katika vikundi vya Vikoba Monduli mjini ambao walikwenda kumtembelea nyum