Posts

Showing posts from June 10, 2012
Image
Ripoti kutoka Damascus zinaonesha mapambano makali baina ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa upinzani katika mji mkuu. Walioshuhudia matukio hayo wanasema wapiganaji wa Jeshi Huru la Syria walifanya mashambulio yaliyopangwa dhidi ya vituo vya serikali siku ya Ijumaa. Kinu cha umeme kilishambuliwa na moshi ulionekana. Basi lilobeba wafanyakazi wa sekta ya mafuta kutoka Urusi lilipigwa. Baraza la Kitaifa la Syria Mashahidi wanasema wapiganaji wengi waliohusika waliuwawa au kukamatwa. Haijulikani jeshi la serikali lilipata hasara gani na wakuu mjini Damascus hawakusema kitu juu ya tukio hilo. Abdelbaset Sayda Huku nyuma Baraza la kitaifa la Syria (SNC) limemchagua mwanaharakati mwenye asili ya Ki-Kurdi kama Rais wake mpya. Abdelbaset Sayda  alichaguliwa kuchukua pahala pa  Burhan Ghalioun , aliyeshikilia wadhifa huo tangu kundi hilo liundwe mnamo mwezi Septemba.
Image
Bingwa wa Dunia wa uzani wa welter tawi la masumbwi la WBO Manny Pacquiao amepoteza taji lake kwa mara ya kwanza aliposhindwa na Mmarekani Timothy Bradley kufuatia uwamuzi wa kutatanisha mjini Las Vegas.         Licha ya Pacquiao kupiga ngumi 94 ikiwa ni zaidi ya mpinzani kiwango cha kwake, Mfilipino huyo alishindwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka saba baada ya waamuzi wawili kuamua kuwa Timothy Bradley ameshinda kwa 115-113, uwamuzi uliegemea hilo. Mwamuzi mwingine alitofautiana na wenzake akimpa ushindi Pacquiao wa 115-113. Watazamaji wa pambano hilo hawakuridhika na uwamuzi uliotangazwa na walizomea sana baada ya Bradley kutangazwa kua mshindi na hilo limezua uwezekano wa pambano la marudio baadaye mwaka huu. "nilihisi nimeshinda," alisema Bradley, ambaye hapo kabla alikua amechapisha tiketi kabambe za kuonyesha pambano la marudano kufanyika tarehe 10 novemba. Bradley aliongezea kusema kua "sidhani ni hodari kama

MASHUJAA BENDI

Image
Kiongozi na mwimbaji wa Bendi maarufu wa Mashujaa Chaz Baba jana akizikonga nyoyo za mashabiki wake kwa nyimbo zake mpya ndani ya ukumbi wa Business Centre Maeneo ya makumbusho. Mpiga tumba maarufu Afrika Mashariki wa Bendi ya Mashujaa MCD akipafomu ndani ya Business Centre jana Usiku. Maua ya Mashujaa Band yakiwachengua mamia ya washabiki wao ndani ya Business centre jana usiku. Bendi ya Mashujaa ni moja ya Bendi maarufu Nchini ambazo zinakuja juu katika medani ya muziki wa bendi na kuthamini thamani ya mwanamuziki.

MAONYESHO YA KWANZA YA HOMES EXPO

Image
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa  Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa, NHC, kutoka kwa Ofisa Masoko wa Shirika hilo, Mariam Ndabagenda, wakati Makamu  alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja  vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Shirika hilo, William Genya (wa pili kulia) ni Ofisa  Mauzo mwandamizi wa Shirika hilo, Emmanuel Lymo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu utengenezaji  wa Viage vya ujenzi wa Nyumba kutoka kwa Ofisa Masoko wa Kampuni ya Insignia Ltd, Obed Machoka, wakati Makamu alipokuwa  akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya  Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.Picha na Muhi

KONGAMANO LA WANA TAALUMA

Image
 Mwanataalum mkonge Profesa Goran Hyden akijibu hojana maswali mbalimbali yalitolewa na wahadhiri na wanataalum mbalimbali kutokandani na nje ya Tanzania jana mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la sikumoja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam lakutambua mchango wake kitaalum.  Waziri Mkuu Mstaafu wa Uganda Profesa Apolo Nsibambi(kulia)akichangia mada jana mjini Dar es saam wakati wa kongamano la siku moja lawanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambuamchango wa Profesa  Goran Hyden alioutoandani na nje Tanzania. Wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti yaUtumishi wa Umma George Yambesi(katikati) na Profesa Goran Hyden(kushoto)  Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es  salaam Profesa Rwekaza Mukanda (kulia) akibadilishanamawazo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uganda Profesa Apolo Nsibambi (katikati) na Balozi wa Zambia nchini Judith Kangoma( kushoto) jana mjini Dar es salaam wakatiwa kongamano l
Image