Posts

Showing posts from September 4, 2012

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea kwa ukali wakati akionyeshwa ramani na Mpima wa Manispaa Selice Nzyungu ya eneo alilouziwa muwekezaji Ephatta Ministry na lile walilopewa wananchi wa kata ya Mollo katika Manispaa ya Sumbawanga. Mkuu huyo wa Mkoa amelazimika kutembelea eneo hilo baada ya kupewa taarifa za awali na Kamati aliyoiunda katika kufuatilia mgogoro unaoendelea kati ya muwekezaji na wananchi wanaolizunguka shamba hilo. Lengo kuu la ziara yake hiyo ya tarehe 02, Septemba 2012 ilikuwa ni kutembelea mashamba yakiwemo ya muwekezaji na wananchi pamoja na kuzungumza na wananchi na muwekezaji kwa kuchukua kero zao kwa ajili ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo.  Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa akizungumza kwenye Mkutano na wananchi wa kata ya Molo ambapo pia wawakilishi wa muwekezaji walialikwa kuskiliza na kutoa kero zao mbele ya wananchi wa kata hiyo. Hata hivyo baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kusikiliza kero hizo aliwaahidi wananchi pamoja na mu

Waandishi Mbeya waeleka Tukukuyu katika Mazishi ya Mwangosi

Image
Timu ya wanahabari wa mkoani Mbeya kupitia Chama cha Wanadishi wa Habari Mkoa wa Mbeya  wakiwa safarini kuelekea Kijiji cha Busoka Tukuyu wilayani Rungwe mkoani humo Ambapo Mwili wa marehemu Daud Mwangosi aliyekuwa Mwakilishi wa Channel Ten anataraji kuzikwa baada ya kupoteza maisha kwa kushambuliwa na bomu wakati wa fujo baina ya Polisi na Wafuasio wa Chadema Iringa.  Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu, wa kwanza kushoto ndugu Joseph Mwaisango akiwa ndani ya Basina waandishi wengine  kuelekea katika Msiba na Mazishi muda huu.  Safari inaendelea Hapa Mambo yanaenda na safari inaendelea kama kawaida , ni asubuhi kabisa lakini tunajitahidi kuwaletea tukio zima Live moja kwa moja.  Safari inaendelea Hakika hakuna Mwandishi wa habari hata mmoja aliye na Furaha wengi wanaonekana wakiwa na uchungu, juu ya kifo cha Mwandishi mwenzao. SOURCE:Mbeya Yetu Blog

Waziri Terezya huvisa azungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar leo

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)  kuhusu Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira wa Nchi za Afrika, Mkutano huu ni Kutathimini utekelezaji wa Makubaliano ya Mkutano wa 13 Uliofanyika Banako, Mali Mkutano Unafanyika Nchini Tanzania Mjini Arusha kulia Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Julias Ningu