Posts

Showing posts from June 16, 2012

MWENGE WAWASILI ZANZIBAR

Image
 Mwenge wa Uhuru leo Umeingia Kisiwani Zanzibar ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Kapteni Honest Mwanossa ameweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo katika mkoa wa mjini Magharibi. Akiweka jiwe la Msingi la kituo kidogo cha Polisi cha Kombeni Mjini Zanzibar, kiongozi huyo amewataka viongozi wa Kitaifa kuepuka ufujaji wa fedha za wananchi na kujiingiza kwenye ufisadi na kuwataka wafanye mambo kwa maslahi ya Taifa. Awali katika risala yao kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge, wananchi wa Makombeni wameliomba Jeshi la Polisi kuangalia uwezekano wa kuharakisha ujenzi wa kituo hicho ili kupunguza kero ya uhalifu katika eneo hilo. Moja ya ujumbe wa Mwenge wa mwaka huu umehimiza umuhimu wa kila mmoja wetu kuhesabiwa katika Sensa ya kitaifa ili kuiwezesha Serikali kupanga vema maendeleo kwa wananchi wake. Mwenge huo umewasili kisiwani Zanzibar ukiotokea mkoa wa Lindi ambako ulikuwa ukikimbizwa katika wilaya mbalimbali za mkoa huo.

NAPE AKIZUNGUMZA NA WALIMU WA MKOA WA IRINGA MJINI MAFINGA

Image
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na walimu wa shule za sekondari na za msingi mjini Mafinga mkoani Iringa, leo katika ukumbi wa Southern Highland,  ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezaji ilani ya Chama tawala cha CCM mkoani humo. Katika mazungumzo hayo Nape alipata fursa ya kusikiliza kero za walimu na kujadili nao jinsi ambavyo serikali itakavyoweza kuyatatua. Walimu wa shule za sekondari na msingi wa mjini Mafinga, wakimsikiliza Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipozungumza nao leo kwenye ukumbi wa  Southern Highland mjini Mafinga mkoani Iringa