Posts

Showing posts from July 31, 2012

MWANAHALISI LAFUNGIWA

Image
Jana serikali imeifungia gazeti la Mwanahalisi kuanzia tarehe 30 ya mwezi wa saba mwaka huu wa 2012 kwa mda ambao usiofahamika kwa kile kinachodaiwa kuwa gazeti hilo hutoa habari za uchonganishi na za uchochezi kwanik halifuati taaluma za habari.

KUTOKA GAZETI LA MWANANCHI

Image
Monday, 30 July 2012 21:07 Wanafunzi wa shule za Msingi za Temeke wakiingia kwenye ofisi za Manispaa ya Temeke kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana na kuwasababishia kukosa masomo.Picha na Elizabeth Edward WALIMU WAGOMA KILA KONA, WANAFUNZI NAO WACHACHAMAA, SERIKALI YAONYA, YATISHIA KUWAFUTIA MISHAHARA Waandishi Wetu NCHI imetikiswa. Mgomo wa walimu ulioanza jana katika sehemu mbalimbali nchini, umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu huku kukiwa na taarifa za matukio yasiyokuwa ya kawaida yaliyoambatana na mgomo huo usio na ukomo. Katika sehemu mbalimbali nchini, walimu waliripotiwa kugoma kwa kutoingia madarasani na wengine walifika kazini na kusaini vitabu vya mahudhurio kisha kuondoka hali iliyosababisha wanafunzi kurandaranda ovyo katika sehemu za miji iliyo karibu na shule hizo. Mjini Dodoma ,wabunge jana walimbana Naibu Spika, Job Ndugai wakitaka shughuli za Bunge zisitishwe ili kujadili mgomo wa walimu ambao umeanza rasmi jana nchi nzima

KUTUMA PESA BUREEE

Image
Kupata huduma ya Airtel money  sasa piga *150*60# Bure Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuboresha huduma ya Airtel money kwa kurahisisha upatikanaji wa  muongozo (menu) kwa kupiga *150*60# Bure pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma pesa Bure   Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” Airtel tunaendelea kutoa uhuru kwa wateja kupata huduma zetu kirahisi zaidi  nchini kote, kuanzia sasa mteja akipiga *150*60# anapelekwa mojakwamoja kwenye horodha yake ya huduma  na kuweza kuchagua anachohitaji kufanya ikiwa ni pamoja na kuongeza salio, kufanya malipo, kutoa pesa  na mengine mengi tumefanya hivi hii ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote kupata huduma za kibenki na kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa mteja anauhuru wa kuchagua kutumia njia ya awali ambayo ni kwenda mojakwa moja kwenye muongozo wa simu yake na kupata horodh

FUTARI PEMBA

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kushoto) akijumuika na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa kaskazini Pemba katika chakula cha Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba jana.{Pichana Ramadhan Othman,Ikulu.} Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,Dadi Faki Dadi,akitoa shukurani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wake baada ya chakula cha Futari alkiyowaandalia katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba jana. {Pichana Ramadhan Othman,Ikulu.} Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakiitikia dua iliyoombwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,baada ya chakula cha Futari,huko Ikulu ya WEte Pemba jana. {Pichana Ramadhan Othman,Ikulu.} Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Moh