Posts

Showing posts from June 7, 2012

MISS KIGAMBONI YATOA MSAADA

Image
SEHEMU ya mapato yatakayopatikana katika shindano la urembo la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu yataenda kusaidia ukarabati wa madarasa yaliyopo kwenye Shule ya Msingi Kigamboni iliyopo jijini Dar es Salaam imeelezwa. Shindano la urembo la kitongoji cha Kigamboni linatarajiwa kufanyika Juni 15 kwenye Ukumbi wa Navy Beach kuanzia saa 1:00 usiku. Akizungumza jana, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa wameamua kutoa sehemu ya fedha zitakazopatikana kwa lengo la kuipa heshima ya shule hiyo ambayo ni moja ya sehemu zilizotoa washiriki wa kinyang'anyiro hicho na wajumbe wa kamati ya maandalizi. Alisema kuwa wanawaomba wakazi wa Kigamboni na wengine kutoka sehemu mbalimbali jijini kujitokeza kushuhudia warembo wao ambao hapo baadaye wataenda kukiwakilisha kitongoji hicho kwenye mashindano ya Kanda ya Temeke. Aliongeza kuwa katika kusindikiza shindano hilo, bendi muziki wa dansi ya FM maarufu kama 'Wazee wa Ngwasuma' pamoja na msanii wa vic

UCHAMBUZI

Image
Serikali inapendekeza Bajeti ya TZS 15 trilioni(USD 8.75 Billion) katika mwaka 2012/13. Uchambuzi wa vitabu vya Bajeti unaonesha kwamba mafungu ya juu 5 kwenye Bajeti ni Kama ifuatavyo; 1    Huduma kwa Deni la Taifa          Tshs 2.7 trilioni(USD 1.69 Billion) 2    Wizara ya Ujenzi.                          Tshs 1 trilioni (USD 625 Million) 3    Wizara ya Ulinzi                          Tshs 920 bilioni (USD 575 Million) 4    Wizara ya Elimu                              Tshs 721 bilioni (USD 451 Million) 5    Wizara ya Nishati na Madini    Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)  TOTAL                                        TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion) Chanzo: Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge Jumla ya mafungu haya ni sawa na asilimia 40% ya Bajeti. Kwa hiyo asilimia 40% ya Bajeti yote imepangwa kwa mafungu 5 tu. Fungu lenye kiwango kikubwa zaidi ya Bajeti kuliko vyote ni fungu 22 ambalo ni malipo kwa Deni la  Taifa. Pia sehemu kubwa ya fedha zilizotengwa kwa Ujenzi
Image
EXCITING CAREER OPPORTUNITIES IN BANKING Promoters of new bank are seeking to recruit high caliber, Results- oriented and self driven people with high integrity to fill the following positions in Dar es Salaam 1.  IT Manager (one position) In-charge of organizing the IT department DUTIES AND RESPONSIBILITIES: Head of IT will take a lead role in supporting our IT Systems. Installing and maintaining servers and integrating applications software. Ensures the operations and administration of the core banking system (CBS) and peripheral software Manages the Network System and network infrastructures projects of the bank To provide adequate training and assistance users of the Management Information System (MIS) KEY QUALIFICATIONS: A good degree or an advanced Diploma in IT/computer Science Minimum 3 years experience as IT manager in a company. Banking sector is an asset In-depth knowledge and use experience

FREEMASON

Image
Siku Ya leo katika Kipindi Cha Leo Tena Katika Radio Maarufu ya Clouds FM pamoja na kwenye Clouds TV wamejitokeza Watu wanaodai wao ni Freemasons na Kueleza Wanavyofanya kazi. Watu hao ambao inaonekana hawakuwa wamejipanga kwenda kwenye Media Wameshindwa kujibu baadhi ya Maswali waliyokuwa wakiulizwa na Mtangazaji Zamaradi. Mara Kwa Mara watu hao Wamekuwa Wakikinzana katika Maelezo wanayotoa kuhusu Freemasons. Katika moja ya Maelezo Yao wameeleza Kila Mtu ni Freemason akiwa Mkristo ama Muislam anaweza kuwa Freemason walijichanganya zaidi baada ya kuulizwa kama ndivyo basi hawa Jamaa hawana ibada, wakasema "Huwezi Kuwa Mroman, Kama Hauendi Kwenye Ibada Za Waromani, vivyo hivyo kila Freemason lazima aje kwenye Ibada". Kumekuwa na Wimbi la Watu Wanaoibuka na Kudai kuwa na ufahamu wa Kutosha Kuhusu Freemasons. Mungu aisaidie Tanzania Mungu atuepushe na roho ya Ujinga na Kukataa Mafundisho Ya neno la Mungu. Hawa ndio wataalam wa level ya u-DR waliokuwa leo kwenye

Kombani akutana na Katibu pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Ajira

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani amesema anaona ni wakati muafaka sasa kupitia upya miundo ya tumishi wa umma ili kuendana wakati pamoja na soko la ajira nchini. Kombani amesema hayo jana wakati alipokuna na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira, Bw. Xavier Daudi  pamoja na Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Bakari Mahiza pamoja na Makamu Mwenyekiti Bibi Rose Lugembe walipokwenda kumtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha pamoja na masuala mengine ya kikazi. Amesema ni vyema miundo hiyo ikapitiwa ili kuweza kubaini fani ambayo inahitajika zaidi katika soko la ajira hivi sasa na kuweza kuwashauri wadau kujikita zaidi katika fani hizo kuliko kuendelea kukimbilia kozi  ambazo zina wataalamu wengi na fursa za ajira ni chache. “Nadhani ni vizuri tukapitia tena miundo ya utumishi wa umma ili kubaini fursa za ajira na pia kutoa ushauri kwa wadau wa elimu na wanafunzi kujikita zaidi katika fani ambazo hazina wataalamu

SOMO KTOKA KWA POLISI

Image
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar   Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, leo imezindua rasmi somo la Polisi  litakalojulikana kama Usalama wetu kwanza kuwa moja ya masomo yatakayofundishwa kwa wanafunzi wa shule za msingi visiwani humo. Akizungua mpango huo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mh. Ali Juma Shamhuna, amesema kuwa somo hilo litaanza kufundishwa kwa majaribio katika shule kumi za msingi kisiwani Unguja na hivyo kulifanya somo hilo kuwa sehemu ya masomo yaliyopo katika mitaala ya shule za msingi Visiwani hapa. Mh. Shamhuna amesema kuingizwa kwa somo hilo katika mitaala ya shule za msingi, kutasaidia kujenga uwezo na uwelewa wa kujitambua na katika kuwabaini wahalifu mbalimbali wakiwemo maadui wa taifa letu. Mh. Shamhuna ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa mpango huo, amekagua vitabu vitakavyotumika katika kufundishia somo hilo ambavyo vimeandaliwa na Jeshi la Polisi hapa nchini kwa ajili hiyo.

BASATA

Image
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeendesha semina ya siku moja kwa majaji wa shindano la Epic Bongo Star Search 2012 kwa kuwataka kuzingatia maadili ya kazi zao.   Akitoa somo kwa majaji hao mratibu wa matukio wa Basata Malimi Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa asilimia kubwa   ya washiriki wanategemea zaidi msaada wao katika kukuza vipaji.   Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa mazingira waliyotoka washiriki na kuangalia namna ya kuwasaidia kulingana na mikoa yao kwa kuwa wapo ambao wana vipaji lakini wanatatizwa na suala la kuyazoea mazingira.   Alisema kuwa kwa kuwa mwaka huu EBSS itaruhusu washiriki wa miaka 16 hivyo ni vema zaidi wakazingatia suala la sauti kulingana na umri wa mshiriki sababu watakuwepo wenye sauti za kitoto pia.   Pia aliwataka majaji hao kuhakikisha kuwa hawatoi aina yoyote ya upendeleo na wala kuwa karibu zaidi na baadhi ya washiriki wa shindano hilo.   Pia alisisitiza kuwa majaji wanalo jukumu kubwa la

COPA COCA COLA KUTUMUA VUMBI JUNI 24

Image
Michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa inaanza kutimua vumbi Juni 24 mwaka huu kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Pwani huku pambano la ufunguzi likiwa kati ya Kigoma na Lindi litakalofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.   Upangaji ratiba (draw) umefanyika leo (Juni 7 mwaka huu) kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kushuhudiwa na waandishi wa habari, makocha wa timu za mikoa za Copa Coca-Cola na wadhamini kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola. Makocha 35 wa timu za Copa Coca-Cola kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani wako kwenye kozi ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoendeshwa na wakufunzi Ulric Mathiot wa FIFA kutoka Seychelles na wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Sunday Kayuni wa Tanzania.   Mikoa 28 ya kimpira ya Tanzania itashiriki katika mashindano hayo na imegawanywa katika makundi manne ya timu saba saba. Baadaye timu zitapambana kat

RAGE AWAKA

Image
Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage akizungumza na Waandishi wa Habari, mchana huu makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi kuhusu sakata la Yondan MWENYEKITI wa klabu ya Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage amesema atawashitaki wapinzani wao wa jadi, Yanga, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kwa kitendo chao cha kumsajili beki wao, Kelvin Patrick Yondan wakati bado ana makataba na klabu yake. Rage amesema leo mchana katika Mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya Simba, Mtaa wa Msimbazi kwamba ushahidi wa Yanga kumsajili Yondan wakati amekwishasaini Simba, ni picha anayoonekana akisaini wakati amevaa jezi mpya ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars yenye nembo ya wadhamini wapya, Kilimanjaro Beer. Rage amesema kwamba kitendo walichofanya Yanga ni uhuni ni kinautia aibu mchezo wa soka, hivyo amewaagiza mawakili wa klabu hiyo kukaa leo kuandaa mashitaka ya kupeleka FIFA. Aidha, Rage alionyesha nakala ya mkataba ambao Simba imesaini na Yondan, ik

YONDANI AMWAGA WINO

Image
KELVIN Patrick Yondan, beki wa kati wa Simba amekana kusaini mkataba wowote na Simba na amesema yeye amesaini Yanga tu mkataba wa miaka miwili. Yondan amesema Simba wanampakazia kusaini mkataba mpya na anataka wapenzi wote wa soka Tanzania watambue kwamba kuanzia sasa yeye ni mchezaji halali wa Yanga. Yondan aliikana Yanga awali kwa sababu walimsainisha fomu bila kumpa fedha, lakini leo amepewa Milioni 30 zake taslimu na amemaliza kila kitu.

WAZIMBABWE KUCHEZA NA TAIFA STARS NA GAMBIA

Image
Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia itakayochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) mwamuzi wa kati atakuwa Ruzive Ruzive. Waamuzi wasaidizi ni Salani Ncube na Edgar Rumeck wakati mwamuzi wa akiba ni Norman Matemera.   Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Fanie Wallace Mabuza kutoka Swaziland wakati mtathmini wa waamuzi (referee assessor) ni Ali Baligeya Waiswa.   Waamuzi hao watawasili nchini kesho (Juni 8 mwaka huu) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways wakati Kamishna wa mechi hiyo atawasili siku hiyo hiyo saa 12.50 jioni kwa ndege ya South African Airways. Mtathmini wa waamuzi atatua pia Juni 8 mwaka huu saa 7.55 mchana kwa ndege ya Kenya Airways.   Taifa Stars inayodhaminiwa na Kil

MILIONI 421.8 ZAPATIKANA

Image
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (kulia), Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) na Mwenyeji wa harambee ya kuchangia mpango wa elimu wa Kata ya Kipawa, Diwani wa Kata  hiyo Bonah Kaluwa, wakimuongoza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi kuingia ukumbini Katika hafla iliyofanyika jana usiku ndani ya hoteli ya Kilimanjaro (Kempiski hotel) jijini Dar es Salaam .  (PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE) Wadau mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akitoa neno la shukurani kabla ya kuanza kwa harambee hiyo. Mgeni rasmi wa Hharambee hiyo akimpa mkono wa asante mwakilishi wa kampuni ya Home Shopping Centre Bi Madiha Al Harthy (kushoto),Salma baada ya kuchangia sh. milioni 22. Mkurugenzi wa SONGAS Limited Bw;Christopher Ford(katikati),akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya dolla za kimarekani 10,000, mgeni rasmi wa harambee hiyo.kushoto meneja  rasil

TANGAZO

Image
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa inapenda kuutangazia Umma kuwa imepotelewa na v itabu ishirini (20) vya leseni z a biashara vilivyopotea tarehe 22 Mei 2012 katika moja ya Daladala Jijini Dar es Salaam. Vitabu hivyo vilivyotolewa na Wi zara ya Viwanda na Biashara vikiwa na kumbukumbu namba 1389501 mpaka 1391500 . Kwa yeyote atakaye ona vitabu hivyo au kuvinunua anaombwa avipeleke kituo chochote cha polisi kilicho karibu yake au kutoa taarifa juu ya mwenye navyo katika kituo hicho . Ifahamike kuwa vitabu hivyo ni batili hivyo haviruhusiwi kutumika kwa namna yeyote ile. Na atakayethibitika kuvitumia atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria zilizowekwa. Ewe mfanyabiashara, epuka manunuzi na matumizi ya vitabu vyenye namba tajwa hapo juu kwa usalama wa biashara yako . Kwa mawasiliano tunaomba mtumie namba zetu hapo juu. Tunaomba ushirikiano wenu. IM ETOLEWA NA HAMZA TEMBA AFISA HABARI MKOA WA RUKWA 07/06/2012

BONDIA JAPHET KASEBA AZUNGUMZA NA MO BLOG KUHUSU FREEMASON

Image
MO BLOG: Kaseba kuna ukweli wowote kwamba kabla ya kucheza pambano ni vyema siku moja kabla mtu unapaswa kufanya mapenzi.?. KASEBA: Kwa kweli kwa kuwa mimi nilianzia kwenye mchezo wa ‘Martial Arts’ , hicho kitu kilikuwa kinapingwa sana na sidhani hata katika michezo mingine kinakubalika. Sana sana ningewaasa watanzania kujituma katika mazoezi na kuacha kudanganyana. MO BLOG: Hebu izungumzie familia yako kwa sababu mengi yamesemwa na hatupendi kuyarudia. KASEBA: Nampenda sana mke wangu , nawapenda ndugu zangu, pia nawapenda sana wazazi wangu na siku zote namshukuru mwenyezi mungu na naamini hiyo ni moja wapo ya mafanikio yangu, kwa kuwa kila ninachohangaikia nahaingikia kwa sababu ya familia yangu .  Kusoma mahojiano yote Bofya hapa

AJALI YA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO

Image
Baadhi ni picha hizo maeneo ya kashai wilayani bukoba mkoa wa kagera.