SOMO KTOKA KWA POLISI


Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
 
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, leo imezindua rasmi somo la Polisi  litakalojulikana kama Usalama wetu kwanza kuwa moja ya masomo yatakayofundishwa kwa wanafunzi wa shule za msingi visiwani humo.
Akizungua mpango huo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mh. Ali Juma Shamhuna, amesema kuwa somo hilo litaanza kufundishwa kwa majaribio katika shule kumi za msingi kisiwani Unguja na hivyo kulifanya somo hilo kuwa sehemu ya masomo yaliyopo katika mitaala ya shule za msingi Visiwani hapa.
Mh. Shamhuna amesema kuingizwa kwa somo hilo katika mitaala ya shule za msingi, kutasaidia kujenga uwezo na uwelewa wa kujitambua na katika kuwabaini wahalifu mbalimbali wakiwemo maadui wa taifa letu.
Mh. Shamhuna ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa mpango huo, amekagua vitabu vitakavyotumika katika kufundishia somo hilo ambavyo vimeandaliwa na Jeshi la Polisi hapa nchini kwa ajili hiyo.
Awali katika Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Visiwani hapa Bi. Mwanaidi Salehe Abdallah, alisema kuwa somo la Usalama wetu kwanza litakuwa kama somo linguine na litatungia mitihani ya kujipima na ule wa Taifa.
Somo la Usalama wetu kwanzxa ni somo lililobuniwa na Jeshi la Polisi hapa nchini ili kuwawezesha wananfunzi wa shule za msingi na sekondari kujenga uwelewa katika matumizi salama ya usalama barabara kwa lengo la kuepuka ajali za mara kwa mara.
Naye Mwakilishi wa Kamishna wa Polisi zanzibar ACP Mohammed Ali Mweri, amesema kuwa somo la Usalama wetu kwamza limeanzishwa na jeshi la Polisi na ni moja ya Miradi ya Polisi Jamii inayomjenga mtoto katika kuwatambua watu wabaya na jinsi ya kuwaepuka na hata kuwatolea taarifa katika vituo vuya Polisi.
Wakati huo huo, Mh. Shamhuna amekemea vikali baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu kutaka kuhatarisha usalama wa Taifa letu kwa kudai kura ya maoni juu ya Muungano kabla ya shughuli za ukusanyaji wa maoni ya Katiba mpya Jamhuri kukamili.
Amesema watu hao ni hatari kwa Taifa letu na kwamba Serikali haiwezi kukaa kimya kuona amani inavurugika kutokana na kikundi cha watu wachache kwa imani za itikadi ya kidini.
Amesema tangu kukusanywa kwa maoni yaliyoandika Katiba mpya ya Zanzibar yenye sura ya Umoja wa Kitaifa, hivi sasa Zanzibar vimekuwa tulivu na eneo la mfano kwa nchi za Kiafrika zenye utulivu.
 
Amewataka Watanzania kuwaepuka na kuwabeza wale wote wenye kuleta migogoro na kutaka kuiingiza nchi yetu katika vurugu zisizo na msingi na badala yake kila mmoja awe mtulivu na kujishughulisha na kazi zinazoleta maendeleo.
Wakati wa risala yao, wanafunzi kutoka shule kumi zitakazofundisha kwa majaribio somo la Polisi la Usalama wetu kwanza, wameiomba Serikali kutowafumbia macho wale wote wanaochochea vurugu na ghasia kwani wamesema yanapotokea machafuko, wanaoathirika zaidi ni wale wasiojiweza wakiwemo walemavu, wazee, wanawake na watoto.
Naye mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi darajani Rashidi Ali Mohammed, amesema kuwa somo hilo litawapa wanafunzi ujasiri wa kuweza kutoa taarifa Polisi pale wanapoona vitendo vya uhalifu mbele ya macho yao.
ujasiri kapoa Polisi litamwanafunzi Shule kumi za msingi zitakazoanza kunufaika na Somo hilo la Polisi ni Darajani, Makadara, Migombani, Chumbwini, Muungano, Shaurimoyo, kilimahewa “A”, Rahaleo, Jang’ombe na Mkunazini zote za mjini Zanzibar.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA