Posts

Showing posts from September 17, 2012

CLOUD'S MEDIA GROUP WATOA MSAADA

Image
Uongozi wa kampuni ya Clouds Media Group,Wasaniii wa muziki wa kizazi kipya na filamu,mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,walezi sambamba na watoto wa kituo hicho wakiwa katika picha pamoja. Baadhi ya vijana walioko kwenye mafunzo ya kujitolea kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya kituo hicho cha matumaini kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.  Uongozi wa Clouds Media Group kwa kushirikiana na Baadhi ya wasanii wanaotumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakikabidhi sehemu ya misaada mbalimbali ikiwemo vyakula kwa kituo cha The Village of Hope,kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma,kutoka kulia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Shetta,Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simalenga,mmoja wa walezi wa kituo hicho,Sister Maria Rosaria sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Mh Lephy Benjamin Gembe wakiwa na watoto wa kituo hicho cha The Village of Hope baada ya kukabidhiwa msaada huo ambao walifurahia kuwa kiasi kikub

UZINDUZI WA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI TAIFA LEO

Image
Msanii wa Kundi la Vichekesho, Mkwere kutoka kundi la Mizengwe akiigiza kama Askari wa Usalama wa Barabarani akisimamisha magari wakati wakitoa burudani katika Uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa leo mjini Iringa katika Uwanja wa Samora. Maadhimisho hayo yameanza leo Septemba 17-22, 2012. Kaulimbiu  ya maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani. Dk. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed Jabri Sasi, baada ya Waziri kuwsili uwanja wa Samora Iringa.  Waziri Nchimbi akisalaimMbunge wa Viti Maalum, Rita Moto Kabati na viongozi wengine wa Mkoa wa Iringa  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando (kushoto) akimkabidhi Moderm ya Airtel 3.75G Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ya Simu ambao ni wadha,mini wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kit

HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)

Image
HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T) KWENYE UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWAUSALAMA BARABARANI KITAIFA MKOANI IRINGA TAREHE 17 SEPTEMBA, 2012 Mhe. Mgeni Rasmi Mhe. Eng. Gerson  Hosea Lwenge (Mb), Naibu Waziri wa Ujenzi na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Ndugu Mbarak Abdulwakil, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Herbert Mrango, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ndugu Said Ally Mwema, Inspekta Jenerali wa Polisi Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani (T) Wageni Waalikwa Wanahabari Mabibi na Mabwana Asalaam Aleikum, Amani ya Mungu iwe juu yenu Awali ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwako Mhe. Mgeni rasmi kwa kukubali kwako  kuungana nasi katika ufunguzi wa wiki ya maadhimisho ya nenda