CLOUD'S MEDIA GROUP WATOA MSAADA
Uongozi
wa kampuni ya Clouds Media Group,Wasaniii wa muziki wa kizazi kipya na
filamu,mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,walezi sambamba na watoto wa kituo
hicho wakiwa katika picha pamoja.
Baadhi
ya vijana walioko kwenye mafunzo ya kujitolea kutoka nchi mbalimbali
wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya kituo hicho cha matumaini
kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Uongozi
wa Clouds Media Group kwa kushirikiana na Baadhi ya wasanii
wanaotumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakikabidhi sehemu
ya misaada mbalimbali ikiwemo vyakula kwa kituo cha The Village of
Hope,kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma,kutoka kulia ni msanii wa
muziki wa kizazi kipya aitwaye Shetta,Ofisa Mahusiano wa Clouds Media
Group,Simalenga,mmoja wa walezi wa kituo hicho,Sister Maria Rosaria
sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Mh Lephy Benjamin Gembe
wakiwa na watoto wa kituo hicho cha The Village of Hope baada ya
kukabidhiwa msaada huo ambao walifurahia kuwa kiasi kikubwa.
Wasanii
wa Bongofleva na wasanii wa Filamu kwa pamoja wakifurahi na watoto hao
waishio katika mazingira magumu ndani ya kituo cha The Village
Hope,chenye jumla ya watoto zaidi ya 180 na idadi ya familia 14
Baadhi
ya walezi wa watoto wa kituo hicho wakishuhudia tukio la kukabidhi
msaada huo kwa uongozi wa kituo cha The Village of Hope.
Baadhi
ya vijana walioko kwenye mafunzo mbalimbali ya kujitolea wakisaidia
kubeba baadhi ya misaada iliyotolewa na Kampuni ya Clouds Media Group
ikishirikiana na Wasanii wa bongofleva na wa Filamu.
Mmoja
wa wasimamizi wa kituo cha The Village of Hope,Father Vincent Boselli
akitoa ufafanuzi mfupi wa mambo mbalimbali ya kituo hicho mbele ya Mkuu
wa wilaya ya Dodoma Mjini,Mh Lephy Gembe sambana na wasanii wa muziki wa
bongofleva na wa Filamu
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya,Diamond akijitambulisha mbele ya watoto na
pia aliwaimbia baadhi ya nyimbo zake na kuwafanya watoto hao wafurahi
zaidi,kwani walikuwa wakimuona tu kwenye luninga ama kuzisikia nyimbo
zake kwenye redio.
Mmoja
wa waigizaji mahiri katika tasnia ya Filamu hapa nchini,Aunt Ezekiel
akiwasalimia watoto,kulia kwake ni msaani mkongwe wa bongoflea,Sir Juma
Nature akifuatilia kwa umakini tukio hilo adhimu kabisa.
Ofisa
Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Simalenga akizungumza
machache mbele ya uongozi wa kituo hicho.Kulia ni Ofisa wa Maendeleo ya
jamii ya manispaa ya Dodoma,Bi.Holda Mwassa,Mkuu wa wilaya ya Dodoma
Mjini,Mh Lephy Gembe ,Msanii wa bongofleva,Shetta,Pamoja na walezi wakuu
wa kituo cha The Village of Hope.
Mkuu
wa wilaya ya Dodoma Mjini,Mh Lephy Gembe akiushukuru uongozi wa Kampuni
ya Clouds Media Group pamoja na wasanii kwa kuwa na moyo wa kujitolea
katika suala zima la kuisadia sehemu ya jamii isiyojiweza.
Pichani
juu ni baadhi ya wasanii wa muziki wa bongofleva na Filamu wakisikiliza
kwa makini sehemu ya historia fupi ya kituo hicho iliyokuwa ikitolewa
na Wasimamizi wa kituo hicho (hawapo pichani).
Ofisa
Mahusiano wa Clouds Media Group,Bwa.Simalenga akizungumza na Wasimamizi
wakuu wa kituo hicho cha The Village of Hope kabla ya kukabidhi sehemu
ya msaada iliyowasilisha kwenye kituo hicho chenye zaidi ya watoto 180
waishio katika mazingira magumu,ambapo kwa mujibu wa Wasimamizi wa kituo
hicho walieleza kuwa watoto wanaowalea ni wale wanaotoka mikoa ya
Singida,Dodoma na Morogoro na mikoa ya jirani.
Mkuu
wa Vipindi na Utafiti Clouds Media Group,Bwa.Ruge Mutahaba akisalimiana
na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mjini,Mh.Lephy Gembe ndani ya kituo cha The
Village of Hope,kulia kwake ni Stuwart akiwakilisha sehemu ya Bongo
Movie.
Baadhi ya wasanii mbalimbali wakiwasili kwenye kituo cha The Village of Hope,kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.