Posts

Showing posts from June 27, 2012

Matukio mbali mbali hospitali ya Muhimbili leo

Image
  Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakimpakia kwenye Gari Daktari Mwenzao aliepatwa na Mkasa wa Kutekwa Nyara na watu wasiojulikana na ambao walimjeruhi vibaya sana,Dk. Steven Ulimboka aliepatwa na mkasa huo usiku wa kuamkia leo huko katika msitu wa Mabwepande,jijini Dar Wanahabari wakihangaika kupata picha ya Dk. Steven Ulimboka alieinginzwa kwenye gari hiyo tayari kwa kupelekwa kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa matibabu zaidi. Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiisukuma gari iliyokuwa imempaki Dk. Stevan Ulimboka. Madaktari na Wauguzi wa Muhimbili wakiwa wamesimama huku wakizungumzia hali iliyompaka mwenzao. Wanahabari wakitafuta taswira. hakuna kazi iliyokuwa ikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati Dk. Ulimboka akifikishwa hospitalini hapo.

MSHINDI MWINGINE

Image
WASHINDI WENGINE WAWILI WASHINDA ZAWADI ZA SBL, MMOJA ACHOMOKA NA GENERETA , MWINGINE PIKIPIKI Meneja wa bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo akitangaza majina ya washindi wa promosheni ya Vumbua Dhahabu chini ya Kizibo inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti SBL katika makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbay, kulia ni Tumainieli Malisa kutoka PWC na kushoto ni Abukary kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha. Meneja wa bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo akiongea na mshindi wa pikipikiwakati alipompigia simu kumtaarifi juu ya ushindi wake, kulia ni Joyce Mwijage kutoka kampuni ya bia ya Serengeti, kushoto ni Tumainieli Malisa kutoka PWC na nyuma aliyesimama ni Abubakary kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha

MAREHEMU AMINA CHIFUPA WAKATI WA UHAI WAKE

Image
Amina Chifupa alipenda michezo hali iliyompelekea mara kwa mara kutoa misaada mbalimbali ya vifaa vya michezo. Hapa ilikuwa katika ukumbi wa Manispaa ya Temeke, akikabidhi vifaa hivyo kwa Mh. Nchimbi wakati huo akiwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa

LEO NI KUMBU KUMBU YA MIAKA MITANO TANGU KUFARIKI KWA AMINA CHIFUPA

Image

ASUBUHI YA LEO MNH

Image
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, ambaye anaongoza mgomo wa madaktari nchini Dk.Steven Ulimboka akiwa na majeraha baada ya kutekwa na kushambuliwa na watu wasio julikana na kutupwa msitu wa Mabwe Pande uliopo nje ya jiji la Dar es Salaam usiku wa kuakia leo. Wauguzi na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakilisukuma gari la wagonjwa lililombeba mpigania haki zao Dk. Ulimboka wakati akitolewa chumba cha X-ray akipelekwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI). Madaktari wakisaidia kumuingiza Dk.Ulimboka katika gari la wagonjwa namba T 151 AVD la Hospitali ya AAR. Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo Bisimba (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akitoa taarifa ya kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoratibu mgomo wa madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, Dar es Salaam jana. Dk. Cathbert Mchalo wa Taasisi ya Mifupa ya Moi (kushoto

MAANDALIZI YA SABA SABA

Image
Mafundi wakiendelea na usafi katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika viwanja vya maonyesho ya biashara vya Saba Saba jijini Dar es salaam leo ambapo maonyesho hayo yanatarajiwa kuanza rasmi kesho juni 28/ 2012. Msimamizi wa banda la Home Shopping Centre BW.Faiz Mahamood Said akiongea na waandishi wa habari leo katika banda hilo viwanja vya SABA SABA pia Bw. Faiz Mahamood Said alisema amewataka washiriki wa maonyesho hayo kujitokeza wa kwa wingi pia watembelee banda la Home shopping centre wajionee bidha mpya mbalimbali. Mafundi wakiweka bango katika banda la kampuni ya simu TTCL katika viwanja vya saba saba leo Mafundi wakiweka mabango katika viwanja vya maonyesho ya biashara vya Saba Saba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo

KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo

NEW WINNER

Image
Tigo Public Relations Officer, Ms Alice Maro (left) hands over a dummy cheque of Sh 10,000,000 to Ms Zumra Mohamed during a press conference held in Moshi. Ms Mohamed was selected randomly during a live draw last week as the first winner of the on-going Tigo Beatz promotion. Standing in the centre is Mr Abubakari Massoli, Tigo Customer Service and Sales Representative, Kilimanjaro. Far right is Mr Mohamed Hassan Rajabu, Administrative, Kilimanjaro . Ms Zumra Mohamed, the first winner of the on-going Tigo Beatz promotion, proudly holds up a dummy cheque of Sh 10,000,000 from Tigo