Posts

Showing posts from December 30, 2012

Wazalishaji Wa Chumvi Bagamoyo Walalamikia Kupanda Kwa Ushuru

Image
by David Mathias WAZALISHAJI wa Chumvi katika Wilaya ya Bagamoyo wamelalamikia ongezeko la ushuru wa chumvi unaodaiwa kupanda kwa asilimia 50 zaidi ya kiwango kilichokuwa kikitozwa hali inayowasababishia kuongezeka kwa gharama za uzalishaji kuliko bei halisi ya masoko.   Malalamiko hayo yametolewa mwishoni mwa wiki na Katibu  wa Chama cha Wazalishaji Chumvi Tanzania (TASPA), Julius Mosha wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa  habari mjini hapa kuhusiana na malalamiko yanayotolewa mara kwa mara na wadau wa sekta ya chumvi.   Mosha alisema kuwa mwaka 2008 Halmashauri hiyo ilipitisha sheria ndogo ya ongezeko la ushuru wa chumvi toka kutoka Sh.50 kwa mfuko wa kilo 50 sawa na Sh,1000 kwa tani, ikafikia Sh.200 kwa mfuko wa kilo 50 sawa na Sh.4000 kwa tani, hata hivyo ongezeko hilo lililalamikiwa sana na kudai kuwa inashangaza licha ya kuwa na malalamiko hayo kuna taarifa nyingine ya ongezeko la asilimia 50 zaidi.   Alisema licha ya kuwa na malal

HERI YA MWAKA MPYA

Image
 IN ENGLISH: AS THE OWNER OF THIS BLOG ONCE KNOWN AS ''UMOJA BLOG'' BUT NOW IT WILL BE KNOWN AS ''KANYELELE BLOG'' STARTS FROM TODAY, I WISH ALL OF YOU MY FOLLOWERS WHO READ NEWS FROM THIS BLOG HAPPY NEW YEAR OF 2013 Katika Kiswahili: Kama mmiliki wa hii blog ambayo zamani ilifahamika kama Umoja blog na sasa inafahamika kama Kanyelele blog kuanzia leo, nawatakia wote wasomaji wangu wa blog hii Heri ya mwaka mpya wa 2013

BILALI AMJULIA HALI PADRI AMBROSE LEO

Image
by David Mathias  on December 30, 2012         Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsalimia Padri  Ambrose Mkenda, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Zanzibar, leo Desemba 30, 2012 aliyelazwa katika  Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kujeruhiwa na risasi na watu  wasiojulikana wakati akiwa getini akisubiri kuingia nyumbani kwake mjini Zanzibar hivi karibuni. Kulia ni Muuguzi  mwangalizi wa mgonjwa huyo, Namsifu Fue.         Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Padri  Ambrose Mkenda, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Zanzibar, leo Desemba 30, 2012 aliyelazwa katika  Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kujeruhiwa na risasi na watu  wasiojulikana wakati akiwa getini akisubiri kuingia nyumbani kwake mjini Zanzibar hivi karibuni. Kulia ni

MSHINDI WA UNIQUE MODEL 2012 APATIKANA

Image
Mwanamitindo bora wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Unique Model Photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na Unique Model Talent Vestina Charles mara baada ya kutangazwa kwa mshindi. Mwanamitindo wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) amepatikana jana usiku kwenye shindano lililofanyika kwenye Klabu ya New Maisha jijini Dar es Salaam akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa pili Cesilia Michael (kushoto) na mshindi watatu Amina Ayubu. Washiriki waliongia tano bora. Washiriki waliongia tano bora. Majaji wa shindano hilo kutoka kushoto ni Gymkhana Hilal kutoka Paka Wear , Asia Idarous na Martine Kadinda. Unique Model Talent of the year 2012 Vestina Charles akionyesha uwezowake wa kucheza jukwaani. Wakitumbuiza mashabiki mapema kabla ya kuingia kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali. Washiriki 12 wa shindano hilo wakiwa wamejipanga

CHAKULA CHA JIONI KATI YA UONGOZI WA FLIGHTLINK NA WAFANYAKAZI WAKE

Image
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink,Munawer Dhiren akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichokuwa kimeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.Picha zote na Othman Michuzi.   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink,Munawer Dhiren akiendelea kuzungumza.  Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink pamoja na familia zao wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,Munawer Dhiren (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.   Mazungumzo ya hapa na

MKUTANO WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TASWA WAFANYIKA BAGAMOYO LEO

Image
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwan Kikwete  akifungua mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA unaofanyika kwenye Hoteli ya Kiromo View Bagamoyo mkoani Pwani ambao unajadili mambo mbalimbali ya Maendeleo na changamoto zinazokabili chama hicho. Waanishi wa habari za michezo ambao ni wanachama kutoka vyombo mbalimbali nchini wanahudhuria mkutano huo ambao ni wa siku moja. Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Juma Pinto akimkaribisha mgeni rasmi ili kufungua mkutano huo leo asubuhi unaofanyika kwenye  hoteli ya Kiromo View Bagamoyo. Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Amir Mhando akizungumza katika mkutano huo, kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA Maulid Kitenge, Mwenyekiti Juma Pinto, Mgeni rasmi Ridhiwan Kikwete na kushoto ni George John Katibu Msaidizi. Mtaalam wa SACCOS kutoka Manispaa ya Ilala Bw. Luamb