Posts

Showing posts from July 4, 2012

LEO

Image
-Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba(kulia) akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Ofisi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Pilly Mpenda (kushoto)  juu ya faida za kujiunga na mfuko huo wakati kiongozi huyo alipotembelea maonyesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es alaam jana katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere. Katikati ni Afisa wa NSSF anahusika na mambo ya Itifiki Juma Kintu. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo na Masoko David Manyanga(kulia) juu ya faida ambazo mkulima anaweza kuzipata baada ya kununua mashine ya kupanda mpunga aina ya SPW 48C wakati kiongozi huyo alipotembelea maonyesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es alaam jana katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba(kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Fao la Matibabu wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Aisha Marine  (kushoto) 

MATOKEO YA PICHA SABA SABA LEO

Image
Mwanafunzi wa VETA Bw. Onesmo Mrisho akiwapa maelezo baadhi ya washiriki waliotembelea kujionea shughuli mbalimbali zitolewazo na chuo hicho akiwaelimisha juu ya stata ya kuwashia moto kwenye mkaa au kuni badala ya kutumia mafuta ya taa au karatasi na pia railoni ambazo zinaathili kiafya.   Hili ndilo banda la VETA la maonyesho ya bishara ya kimataifa saba saba liloko katika viwanja vya mwalimu JK Nyerere. Dar es Salaam, Mwanafunzi    wa VETA Bw. Salum Machapati akiwaelezea baadhi ya washirika waliohudhuria katika banda la maonesho ya sabasaba ya chuo hicho juu ya matumizi ya kitanda cha kisasa ambacho kinatumika katika hali ya hewa yoyote ambacho kinaundwa kwa kutumia mbao, udongo pamoja na mkaa. Baadhi ya wananchi wakiangalia pampu katika banda la VETA kwenye maonesho ya sabasaba pampu hiyo iliyotengenezwa kwa chuma na inamfumo wa kuvuta maji yenye dawa ambayo yanarahisisha katika kuogesha wanyama. Meneja mhusiano wa VETA    Grace Kabogo akionyesha kabati la sir

YANGA YAPATA KOCHA MPYA

Image
  Kocha mpya wa Yanga, Mbelgiji Thom Saintfiet akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam na kulakiwa na mamia ya wapenzi wa klabu hiyo. wanachama wa timu hiyo wamejitokeza kwa singi katika mapokezi yake tangu anatokea ndani ya Uwanja wa Ndege, hadi akiwa ndani ya gari tayari kwa safari ya Jangwani.   Kochja wa timu ya Yanga akipunga mikono kwa mashabiki mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo mchana. Mashabiki wa timu ya Yanga wakishangilia mara baada ya kumuona kocha wao mpya alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mawalimu J.K.Nyerere.

RAIS JK ARUDI NCHINI AKITOKEA BURUNDI NA RWANDA

Image
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana jioni  wakitokea Burundi na Rwanda walikohuidhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru wa nchi hizo. Anayeongozana nao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Mecky Sadik.   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Afande Saidi Mwema na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana jioni wakitokea Burundi na Rwanda walikohuidhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru wa nchi hizo PICHA NA IKULU
Image
Afisa Maendeleo ya Biashara Mobile Ticketing Limited Bw.Albert Muchuruza akiwaonesha waandishi wa habari njia muhimu za kukata tiketi za mabasi kwa njia ya Mobile Ticketing kwa wasafiri wanaotumia mabasi yaendayo mikoani,anaeshuhudia kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo Juma Mgori. KAMPUNI ya Mobile Ticketing Tanzania Limited imezidi kuboresha huduma zake kufuatia kurahisisha zaidi upatikanaji wa tiketi za kusafiria kwenye Selcom Pay Point kama zinavyopatikana huduma nyingine muhimu nchini. Uboreshaji huo umekuja kutokana na kampuni hiyo kutambua umuhimu mkubwa wa huduma hiyo katika jamii ili kuzidi kuwarahisishia hata wale wasiokuwa na simu za mikononi waweze kupata huduma hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini,Afisa Maendeleo ya Biashara  wa kampuni hiyo, Albert Muchuruza, alisema kuwa amefikia uamuzi wa kuwa na huduma hiyo huku ikiendelea kushirikiana na Vodacom kwaajili ya kuhakikisha huduma hiyo ya tiketi popote inamfikia kila mwananchi hapa nchini. "Tuko kwe

NSSF YAPATA TUZO MBILI KATIKA MAONYEHO YA SABASABA

Image
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar, Balozi Seif Ali Idi akito hotuba yake katika ufunguzi wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Barabra ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Makamu wa Pili wa Rais wa Seriakli ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Idi akifungua rasmi Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa maafufu kama sabasaba. Makamu wa Pili wa Rais wa Seriakli ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Idi akimkabidhi cheti pamoja na tuzo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhan Dau baada ya kuibuka washindi wa jumla katika Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa TANTRADE, Samuel Mvingira akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko, Dk Abdallah Kigoda akizungumza katika hafla hiyo. Mkurugen