UZINDUZI WA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI TAIFA LEO
Msanii
wa Kundi la Vichekesho, Mkwere kutoka kundi la Mizengwe akiigiza kama
Askari wa Usalama wa Barabarani akisimamisha magari wakati wakitoa
burudani katika Uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa leo
mjini Iringa katika Uwanja wa Samora. Maadhimisho hayo yameanza leo
Septemba 17-22, 2012. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA
NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani. Dk. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed
Jabri Sasi, baada ya Waziri kuwsili uwanja wa Samora Iringa.
Waziri Nchimbi akisalaimMbunge wa Viti Maalum, Rita Moto Kabati na viongozi wengine wa Mkoa wa Iringa
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando (kushoto) akimkabidhi
Moderm ya Airtel 3.75G Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi
wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ya Simu ambao ni wadha,mini
wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa inayofanyika mkoani Iringa. Wengine
katika picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza
la Usalama Barabarani. Pereira Silima (wapili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa
Iringa, Dk. Christine Ishengoma. Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa
Usalama yameanza leo kitaifa Mkoani Iringa.
Mkaguzi
wa Polisi, Abel Swai Kutoka Trafiki Makao Makuu jijini Dar es Salaam
akitoa maelezo ya namna ajali za barabarani zinaweza kuepukika endapo
watumiaji wa barabara watakuwa waangalifu na kufuata sheria za
barabarani. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.
Mkaguzi
Msaidizi wa Kikosi cha Polisi zima Moto na Uokoaji, Elia Kakwembe
akitoa maelezo ya namna kusajili makampuni binafsi ya Zimamoto na
uokoaji kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, akisaini kitabu cha wageni
alipotembelea banda la SUMATRA katika uwanja wa Samora. Wanaoshuhudia
katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Ahmad Kilima, na Meneja
Uhusiniano, David Mzirai.
Waziri
wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, pamoja na viongozi wengine
wakimsikilizo Meneja Mauzo na Masoko wa Makampuni ya ASAS ya Mjini
Iringa, Ahmed Omar Kassu juu ya bidhaa mbalimbali za maziwa
wanazozalisha na ubora wake Afrika Mashariki, Wakati Waziri
alipotembelea banda la ASAS lililopo katika maonesho ya maadhimisho ya
Wiki ya Nenda kwa Usalama inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Iringa leo.
Wanafunzi wakipatiwa maelezo ya matumizi yaa yasiyo sababisha ajali.
Baadhi
ya walemavu wakiingia uwanjani katika uwanja wa Samora mjini Iringa
katika Uzinduzi wa Wiki ya kitaifa ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa
jana mjini hapa huku Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel ikiwa mdhamini
mkuu.
Meza
Kuu, Mgeni Rasmi, Waziri wa Mambo ya ndani, Dk.Emmauel Nchimbi (kulia)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma na Mwenyekiti wa
Kamati ya Usalama Barabani Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed Jabri wakipokea
maandamano.
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia maadhimisho hayo.
Mtaalam wa Kughani utenzi, Mpemba Asilia akiwajibika
Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed akizungumza.
Kamnada wa Kikosi cha Polisi Usalkama Barabarani, Mohamed Mpinga, ambaye pia ni Katiraza la Usalama Barabarani, akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma akizungumza
Kaimu Mkurugenzi wa SUMATRA, Ahmed Kilima akipokea cheti cha heshima kutoka kwa Waziri wa Mambo ya ndani.
Waziri
wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, akimkabidhi cheti cha heshima
kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali
barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, Meneja wa Airtel
Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Beda Kinunda.Makabidhiano hayo
yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa
mkoani Iringa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Makampuni ya ASAS, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki
ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed, akipokea cheti cha
heshima kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza
ajali barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, kutoka kwa
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi. Makabidhiano hayo
yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa
mkoani Iringa.
Kiongozi
wa Kundi la Wazee Sugu, King Kikii, akiongeza waimbaji wa kundi hilo
kutoa burudani ya muziki katika uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda
kwa Usalama Kitaifa iliyoanza jana mkoani Iringa.
Wanafunzi wa shule mbalimbali za Mkoani Iringa wakiimba nyimbo za kuhamasisha jamii kufuata sheria watumibara kuepusha ajali.
Bendi ya Polisi Jazz kutoka Dar es salaam ilitumbuiza.