Kombani akutana na Katibu pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Ajira

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani amesema anaona ni wakati muafaka sasa kupitia upya miundo ya tumishi wa umma ili kuendana wakati pamoja na soko la ajira nchini.
Kombani amesema hayo jana wakati alipokuna na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira, Bw. Xavier Daudi  pamoja na Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Bakari Mahiza pamoja na Makamu Mwenyekiti Bibi Rose Lugembe walipokwenda kumtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha pamoja na masuala mengine ya kikazi.
Amesema ni vyema miundo hiyo ikapitiwa ili kuweza kubaini fani ambayo inahitajika zaidi katika soko la ajira hivi sasa na kuweza kuwashauri wadau kujikita zaidi katika fani hizo kuliko kuendelea kukimbilia kozi  ambazo zina wataalamu wengi na fursa za ajira ni chache.
“Nadhani ni vizuri tukapitia tena miundo ya utumishi wa umma ili kubaini fursa za ajira na pia kutoa ushauri kwa wadau wa elimu na wanafunzi kujikita zaidi katika fani ambazo hazina wataalamu wa kutosha na bado wanahitajika sana katika soko la ajira, kuliko kukimbilia kufundisha au kusoma fani ambazo kupata kwake kazi ni kwa shida kutokana na wingi wa wataalamu wa fani hiyo sokoni” alisema Kombani.
Aliendelea kufafanua kuwa kuna baadhi ya kazi wahitimu wake ni wengi hivi sasa hivyo kuna haja ya kutoa mwamko kwa wanafunzi kusoma wakiwa na malengo ya kusoma kitu kitakachowawezesha kujiajiri au kuajiriwa kwa haraka kulingana na soko la ajira.
Aidha, amepongeza jitihada za kuanzishwa kwa Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo itatoa fursa kwa wadau wengi wanaotafuta kazi kuweza kupata taarifa kwa urahisi hata kama wako nje ya nchi.
Pia amehimiza wajumbe hao umuhimu wa kuharakisha uazishwaji wa mfumo wa kielektroniki utakaowezesha wahitimu kuomba nafasi za kazi kwa njia ya mtandao kuliko kutegemea njia ya posta pekee.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira, Bw. Bakari Mahiza amesema kuwa hivi sasa wanakabiliwa na  changamoto kubwa ya  mgongano wa kisheria, ufinyu wa bajeti pamoja na baadhi ya waajiri kuendelea kung’ang’ania majukumu ya kuajiri ilihali Sheria ya kuanzisha chombo hicho imeweka wazi majukumu ya kuendesha mchakato wa ajira yanatakiwa kufanywa na Sekretarieti ya Ajira.

Nae Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi amesema licha ya changamoto wanazokabiliana nazo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza majukumu yao. Aidha, amesema ofisi yake itaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali maana kazi ya mchakato wa ajira mpaka kukamilika inahitaji ushirikiano baina ya mwajiri, mwajiriwa na wadau wengine.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA