WAZIMBABWE KUCHEZA NA TAIFA STARS NA GAMBIA


Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia itakayochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) mwamuzi wa kati atakuwa Ruzive Ruzive. Waamuzi wasaidizi ni Salani Ncube na Edgar Rumeck wakati mwamuzi wa akiba ni Norman Matemera.
 
Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Fanie Wallace Mabuza kutoka Swaziland wakati mtathmini wa waamuzi (referee assessor) ni Ali Baligeya Waiswa.
 
Waamuzi hao watawasili nchini kesho (Juni 8 mwaka huu) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways wakati Kamishna wa mechi hiyo atawasili siku hiyo hiyo saa 12.50 jioni kwa ndege ya South African Airways. Mtathmini wa waamuzi atatua pia Juni 8 mwaka huu saa 7.55 mchana kwa ndege ya Kenya Airways.
 
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA