Waandishi Mbeya waeleka Tukukuyu katika Mazishi ya Mwangosi


Timu ya wanahabari wa mkoani Mbeya kupitia Chama cha Wanadishi wa Habari Mkoa wa Mbeya  wakiwa safarini kuelekea Kijiji cha Busoka Tukuyu wilayani Rungwe mkoani humo Ambapo Mwili wa marehemu Daud Mwangosi aliyekuwa Mwakilishi wa Channel Ten anataraji kuzikwa baada ya kupoteza maisha kwa kushambuliwa na bomu wakati wa fujo baina ya Polisi na Wafuasio wa Chadema Iringa.
 Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu, wa kwanza kushoto ndugu Joseph Mwaisango akiwa ndani ya Basina waandishi wengine  kuelekea katika Msiba na Mazishi muda huu.
 Safari inaendelea
Hapa Mambo yanaenda na safari inaendelea kama kawaida , ni asubuhi kabisa lakini tunajitahidi kuwaletea tukio zima Live moja kwa moja.
 Safari inaendelea
Hakika hakuna Mwandishi wa habari hata mmoja aliye na Furaha wengi wanaonekana wakiwa na uchungu, juu ya kifo cha Mwandishi mwenzao. SOURCE:Mbeya Yetu Blog

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA