WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA MSHINDI WA KWANZA WA SHUGHULI ZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2012 KANDA YA IV ILIYOSHINDANISHA MIKOA MITANO


Mkuu wa Wilaya mpya ya Kalambo Moshi Chang’a ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwenye shughuli za kuzima Mwenge wa Uhuru Mkoani Shinyanga akionyesha Kikombe na Cheti alichokabidhiwa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama zawadi ya ushindi kwa Wilaya yake baada ya kushika nafasi ya kwanza katika shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake alipowasili jana Mkoani Rukwa aikitokea Shinyanga.
Wawakilishi wa Mkoa wa Rukwa waliokwenda kushiriki kuzima mwenge wa uhuru Mkoani Shinyanga na kurudi na kikombe cha ushindi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a, mratibu wa Mwenge Kimkoa Abubakar Serungwe na Katibu wa Mkuu wa Mkoan Frank Mateny wakipewa mapokezi na uongozi na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akipokea kikombe hicho cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a muda mfupi baada ya kumpokea akitokea Mkoani Shinyanga alipokwenda kumuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwenye kilele cha kuzima mwenge wa uhuru.
Watumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakifurahia kikombe hicho cha ushindi.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ALhaj Salum Mohammed Chima akifurahia kikombe hicho kwa pamoja na watumishi wenzake.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akimpa Mkono wa pongezi Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a kwa ushindi alioupata wa Wilaya yake mpya kuwa mshindi wa kwanza wa shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chuma.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA