Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kuongoza shughuli ya kuuaga mwili wa muasisi wa Chadema na Naibu Gavana wa benki kuu wa zamani, Bob Makani, leo. Wanaomkaribisha ni viongozi wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Wilbrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe.
 Rais Kikwete akiwa na viongozi wa Chadema, Mbowe, Dk. Slaa na Zitto Kabwe

 Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba Mpya, Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba, na Waziri Mkuu mstaafu ambaye ni Mjumbe wa Tume hiyo, Dk. Salim Ahmed Salim, wakiwasili kwenye viwanja vya Karimjee.
 Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akimsalimia  Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta
 Mwenyekiti wa IPP, Reginard Mengi akisalimiana na Profesa Philemon Sarungi kwenye msiba huo
 Dk. Slaa akimkaribisha Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye alipowasili kwenye msiba huo kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam
 Kisha akamkumbatia
 Rais Kikwete, Mbowe na Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal wakipokea mwili wa Bob ulipowasili Karimjee.
 Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akitoa salama za CCM
Baadhi ya wanasheria wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kuuaga mwili wa Bob Makani ambaye pia alikuwa mwanasheria wa siku nyingi;

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA