TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KLABU
ya soka ya Simba imepokea kwa furaha taarifa kwamba Rais wa Shirikisho
la Mpira was Miguu Tanzania (TFF), Leodger Chila Tenga, ameagiza
kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na namna mchezaji wa Simba na Taifa
Stars, Kelvin Patrick Yondani, alivyoondoka kambini usiku wa kuamkia
Juni 7 mwaka huu.
Katika
barua ambayo Tenga ameiandikia Simba, ameahidi kwamba uchunguzi
utafanyika katika maeneo makuu mawili. Mosi, iwapo ni kweli Yondani
aliondoka kambini usiku, pili iwapo aliondoka kwa ruhusa maalumu au
alitoroka.
Tenga
ameahidi kwamba kama ikibainika kwamba aliondoka bila ruhusa, basi
hatua zitachukuliwa kwa wote waliohusika chini ya taratibu za maadili
kwa wachezaji (Players Code of Conduct).
Kutokana
na kauli hiyo ya Tenga, uongozi wa Simba umeamua sasa kwamba
hautozungumza lolote kuhusiana na masuala ya Yondani. Tayari timu
imewasilisha vielelezo vyake TFF na kote kwingine ambako suala hilo
linaweza kufika. Kilichobaki sasa ni kusubiri vyombo husika vifanye kazi
yake.
Simba
SC inapenda kuchukua nafasi hii kuwaomba wapenzi na wanachama wake
kutulia na kutobabaishwa na taarifa za wachezaji wake kusajiliwa na timu
nyingine.
Kwa
sasa Simba inaendelea na mikakati yake ya usajili unaokidhi vigezo vya
kimataifa ambao ulisababisha msimu uliopita itwae ubingwa wa Tanzania na
kuifunga YANGA goli 5-0 !
Simba si timu ya maneno mengi kwenye usajili bali ni vitendo.
Tunaomba
wanachama wetu watulie na mara ifikapo tareje 15 Juni mwaka huu, mbivu
na mbichi zote zitajulikana. Siku hiyo, Simba itatangaza wachezaji wake
wote iliyowasajili na iliyowaacha.
Simba
ndiyo mabingwa wa Tanzania na washabiki wake wanatakiwa kutembea vifua
mbele popote pale walipo na wasichanganywe na taarifa za pembeni.
Uongozi wa Simba uko makini na unafanya kazi zake kisayansi.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC