DALALI PETER KAFUMU AVULIWA UBUNGE


 Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora imetengua matokeo ya Ubunge wa Mbunge wa jimbo la Igunga Mh. Dalaly Peter Kafumu ambaye alichukua nafasi hiyo baada ya mbunge wa zamani wa jimbo hilo Rostam Azizi Kujiuzulu.

Mahakama hiyo imemvua Ubunge Dk. Kafumu hii leo katika Hukumu ya kesi ya Kupinga matokero iliyofunguliwa na aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Chadema, Joseph Kashindye dhidi ya Dk Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi. 

Mbali na Dk Kafumu, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi huo, Protace Magayane. Shauri hilo lilianza kusikilizwa rasmi Machi 26 na Jaji Mary Shangali.
 
Zaidi ya malalamiko 15 yaliwasilishwa katika Mahakama hiyo na profesa Safari kwamba waziri wa ujenzi dk. Magufuli alitoa ahadi kwenye mkutano wa kampeni kwamba atawajengea daraja la Mbutu wananchi wa igunga kama watamchagua dk.Kafumu kuwa mbunge wao pia profesa Safari alidai kwamba wasipoichagua CCM hatawajengea na pia aliwatisha kuwa wasipomchagua Kafumu watashughulikiwa.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA