KIGODAAITAKA TBS KUFANYA UKAGUZI
WAZIRI
wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amelitaka Shirika la Viwango (TBS),
kuhakikisha linafanya ukaguzi wa bidhaa kutoka nje kabla hazijaingizwa nchini
ili kuepukana na tabia nchi hii kugeuzwa dampo la bidhaa hafifu.
Kauli
hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana, wakati alipokuwa akizindua Ofisi ndogo
ya shirika hilo, inayoshughulika na ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
Dk
Kigoda alisema iwapo shirika hilo litafanikiwa kudhibiti uingizwaji wa bidhaa
hafifu nchini anaamini kelele zote zinazopigwa kuwa wao ndio chanzo cha
uingizwaji wa biadhaa hizo zitakwisha.
“Nawaagiza
TBS kupitia madukani na sokoni ili kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa ubora wa
bidhaa na zile bidhaa mtakazokuta ni hafifu, zitoweni na kuziharibu na hao
wafanyabishara watozwe faini za kuharibu bidhaa zao”alisema Dk Kigoda.
Alibainisha
kuwa Wizara yake inatarajia kupata taarifa juu ya utekelezaji wa maagizo hayo
kwa vipindi vya kila robo mwaka ili kujua utaratibu wa utekelezaji.
Akifafanua
madhumuni ya wizara ni kushirikiana na taasisi nyingine za serikali kama
vile
Mamlaka ya Mapato (TRA) Baraza
la Mazingira ,Mamlaka ya Chakula na Madawa (TFDA), Mkemia Mkuu wa
serikali, pamoja na Tume ya Ushindani ili kuhakikisha bidhaa za nje
zinapimwa
maridhawa.
“Ili
shehena za bidhaa hafifu zizibitiwe kuingia sokoni na kurudishwa zilikotoka”
kwa mujibu Dk Kigoda.
Naye
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi
ya shirika hilo, Oliver Mhaiki alitabanaisha kwamba uzinduzi wa ofisi hiyo ni
muendelezo wa jitihada za shirika kusogeza huduma kwa wateja.