KATIBA MPYA
Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kimesema wananchi hawajafungwa kutoa
mawazo yao katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba,lakini msimamo wa CCM ni
kubaki katika mfumo wa muundo wa Serikali mbili.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Mjini hapa Jana, Naibu Katibu
Mkuu wa UVCCM Zanzíbar, Jamal Kassim Ali alisema kimsingi wananchi wako
huru kutoa maoni yao kuhusu aina ya mfumo wa Muungano,lakini kwa
wanachama wa CCM ni lazima wafuate msimamo wa Chama hicho.
Naibu
Katibu Mkuu huyo alisema kwamba Umoja wake unaamini katika kulinda na
kuhifadhi umoja na mshikamano uliopo hivyo ni muhimu kwa wananchi
kutokubali kushawishiwa kuvunja Muungano.
“Katika
suala la Muungano, CCM imeweka wazi kuwa itaendeleza muundo wa Muungano
wa Serikali mbili kama inavyoelezwa katika ibara ya 221(a) ya Katiba ya
Chama cha Mapinduzi sisi hatuwezi kuikiuka katiba hiyo” Alisema Jamal.