VIWANGO VYA SHULE VYA SHUSHWA


Watoto wa sule
Ripoti ya kujitegemea ya serikali ya Uingereza imebaini kwamba msaada wa Uingereza kwa nchi za Afrika za Ethiopia, Rwanda na Tanzania umechangia kuporomoka kwa viwango vya elimu katika shule za nchi hizo.
Uchunguzi umeonyesha kuwa watoto milioni hamsini na mbili zaidi wanapata elimu kwa sababu ya msaada huo, huku walimu wasio na sifa ya ualimu wakiajiriwa kukabiliana na ongezeko hilo la wanafunzi.
Hii ni kumaanisha kwamba kiwango cha elimu kwa ujumla katika mataifa hayo kimeshuka, huku watoto wengi wakimaliza elimu yao bila kujua kusoma wala kuandika na kuhesabu.
Malcolm Bruce ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya maendeleo ya kimataifa ya bunge la Uingereza na ameiambia BBC kwamba, ingawa imebainika kasoro hiyo, lakini ni muhimu msaada huo uendelee kutolewa kwa nchi hizo.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA