ASKOFU GAMANYWA
Askofu Sylvester Gamanywa, Rais wa Wapo Mission International. |
Katika toleo lililopita tulianza uchambuzi wa
nadharia za kitheolojia ambazo zimekuwa chimbuko la chuki dhidi ya Israeli
ndani ya kanisa. Nadharia hizo ni “Theolojia ya Mbadala”, “Theolojia ya Utenganisho”
na “Theolojia ya Mabaki”. Kati ya hizi nadharia tatu, inayoongoza kwa chuki
dhidi ya Israeli ndani ya kanisa ni ile “Theolojia ya Mbadala”. Hebu tuchunguze
kwa ufupi baadhi ya vipengele vinachoashiria kuchochea na kueneza chuki dhid ya
Israeli:
Chanzo na madhara
ya thelojia ya mbadala
Nadhari ya Theolojia ya Mbadala ilianza
kati ya karne ya pili na ya tatu tangu kuzaliwia kwa kanisa na ikaanza
kujenga mizizi yake yapata muda wa miaka 200 tangu mwanzo wa kanisa.
Kilichotangulia ni kuweka kutengeneza “hadharia” kwanza, na baadaye ndipo
yakatafutwa maandiko ya kuhalalisha ubaguzi na chuki dhidi ya Israeli.
Baada ya
nadhariia hii kuota mizizi katika kanisa la wasio wayahudi, ikajitokeza jeuri, ukaidi na ubinafsi na kujigamba dhidi ya wayahudi na
Israeli. Kanisa la wasio wayahudi likashusha thamani na nafasi ya Israeli na kujitoa katika nafasi ya
kuitambua na kuiheshimu Israeli
Wakristo wasio wayahudi wengi wakawa wanajivunia kuwa
wafuasi wa Agano Jipya kama ilivyokuwa katika
kitabu cha Matendo ya Mitume. Lakini pamoja na majivuno haya bado wakasahau
kwamba, maandiko yaliyotumika katika kanisa la Matendo bado yalikuwa ni
maandiko ya Kiebrania, ya Agano la Kale mpaka kwenye karne ya nne ambapo
Maandiko ya Agano Jipya yalikusanywa na kutambuliwa rasmi
Hata baada ya Agano Jipya kutambuliwa rasmi, ndani yake bado
Israeli imetajwa kiasi kwamba, pasipo nafasi ya Israeli na wayahudi hivi leo,
huwezi kutafsiri nabii za kibiblia, hususan nabii zile zinazoendelea kutimia
ndani ya nchi hiyo kwa hivi sasa Aidha, Maandiko mengi katika Agano Jipya
hupoteza maana yake halisi pale inapodaiwa kuwa
wayahudi nafasi yao imechukuliwa na kanisa
Mpaka hivi sasa kutokuitambua Israeli kunayafanya maandiko
ya kiebrania ya a Agano la Kale kupoteza uzito na maana yake kwa matumizi ya
sasa; Ikiwa ni pamoja na kupoteza fursa ya kushiriki katika mpango wa Mungu na
unabii kwa ajili ya Kanisa, Israeli na ulimwengu wa leo
Kanisa kutokuamini kutimia kwa
unabii kuhusu urejeo wa Israeli
Nadharia
ya theolojia ya Mbadala iliota mizizi ndani ya kanisa tangu karne ya pili.
Pamoja na kwamba ziko nabii ndani ya maandiko katika Biblia zilizotabiri
urejesho wa Israeli kutoka kwenye mataifa lilipotawanyikia, kanisa halikuamini
kwamba kutumia kwa unabii huo kutafanyika kablal ya ujio wa Kristo mara ya pili
duniani.
Changamoto
dhidi ya nadhari ya Mbadala ilianza rasmi baada ya Israeli kurejea katika nchi yao, na kuanza kuumiliki mji wa Yerusalemu kama zamani za historia yake. Urejeo huu wa Israeli
uliifanya theolojia ya Mbadala kupoteza maana yake, na ndipo hila za kibaguzi
za miaka mingi dhidi ya Israeli zilipoanza kuwa dhahiri.
Kuanzia
wakati huo, baadhi ya viongozi wa makanisa wakaanza kurejea katika maandiko na
kuchunguza nabii zilizotabiriwa kuhusu Israeli na kugundua kwamba urejeo wa
Israeli ni kutumia kwa baadhi ya nabii hizo. Ndipo zilipoanza juhudi za
makusudi za kulitaka kanisa kutubia dhambi ya kukumbatia nadharia potofu na za
kibaguzi dhidi ya Israeli.
Kwako
msomaji mpenzi, niseme waziwazi pasipo kumung’unya maneno hapa. Amini usiamini,
kubali usikubali, ukweli uko dhahiri katika macho ya ulimwengu kwamba, uwepo wa
Israeli pale Mashariki ya Kati, ni utumilifu wa nabii zilizotangulia kutolewa
juu ya Israeli. Wakati ulimwmengu wa kisiasa na kidiplomasia unadai kuwa ni
“uvamizi na kukalia kwa mabavu” maeneo yale; kinabii kwa mujibu wa Biblia, huko
ni “kurejeshewa na Mungu ardhi yao waliyopewa na Mungu kama wenye hatimiliki ya
kudumu”. Najua hii inweza kuudhi au
kukera sana,
lakini ndio ukweli wenyewe ambao unapaswa kusemwa na kutetewa na kila Mkristo
mwenye imani halisi katika Biblia takatifu.
“Ukawaambie,
Bwana MUNGU asema hivi; tazama nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa
walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao
wenyewe; nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya
Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa mataifa
mawili, wala hawatagawanyika kuwa falme mbili tena, hata milele.”
(Eze.37:21-22)
Kwa mujibu
wa maandiko haya ya kinabii, hivi sasa tunashuhudia kwamba, Israeli ni taifa
huru na taifa moja na kiongozi mmoja. Hakuna mgawanyiko wa kitaifa kama ilivyokuwa pale waliposambaratishwa na kutawanywa
ulimwengu mzima. Ni muhimu kuzingatia maneno yasemayo: “…..name nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe…”
Pengine
msomaji unaweza kujiuliza ni kwanini Mungu aliamua kuwarejesha tena? Jibu ni
moja tu. Mungu akisema neno lake
halitanguki. Lazima
atalitimiza. Na hasa anpokuwa amesema katika mfumo wa ahadi. Pamoja na kwamba
Israeli waliendelea kumwasi Mungu kwa njia zote, ahadi za Mungu kwa Ibrahimu
ziliwekewa kinga ya ulinzi mpaka zitimie. Unaweza kusoma maandiko hapa chini
ili kuona uzito wa maneno yalimo ndani yake:
“BWANA
asema hivi, awapaye watu jua, ili kuuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi
na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake
kuvuma; BWANA wa Majeshi, ndilo jina lake; amri hizi, zikiondoka, zisiwe mbele
zangu, asema BWANA, ndipo na wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele
zangu milele.” (Yer.31:35-36)