UMOJA WA VYAMA VYA SIASA WAZUNGUMZA NA WAANDISHI

Katibu Mkuu wa Chama cha siasa TADEA Juma Ali Khatibu akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali hawapo pichani kwa niaba ya Umoja wa Vyama vya TADEA,SAU,NLD na AFP kuhusiana na kuimarisha Amani na Utulivu Zanzibar na Kulaani matukio ya uvunjifu wa Amani yaliotokezea hivi karibuni huko Zanzibar.

Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Vyama vitano vya siasa vimesema mafanikio ya kukua kwa uchumi wa Zanzibar ni matokeo ya kushamiri kwa amani,utulivu na mshikamano wa wananchi.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari  Mjini Zanzibar, Viongozi wa Vyama  vya TADEA,AFP, NLD, SAU, kwa pamoja vimeridhishwa na ukuaji wa uchumi na kuongezeka kwa pato la wananchi.
“Mafanikio ya kukua kwa uchumi wetu yanaendelea kutupa funzo juu ya umuhimu wa kuilinda amani, utulivu na mshikamano wetu ambao umetujengea sifa kubwa” Alisema Katibu Mkuu wa TADEA, Juma Ali Khatib.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake katika mkutano huo, Katibu Mkuu huyo wa TADEA alisema taarifa za uchumi zinaonesha kuwa Zanzibar imepata mafabnikio katika kukuza uchumi.
“Kwa mujibu wa bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/2013, pato la mtu mmoja limeongezeka kutoka wastani wa shilingi 782,000 mwaka 2010 na kufikia shilingi 960,000 mwaka huu” Alisema Kiongozi huyo.
Alisema hayo ni mafanikio makubwa. “Kwa wenzetu hawa wa Chama Tawala-CCM tayari wameshavuka lengo lao la miaka mitano katika muda wa miaka miwili tu…wao walilenga pato la mwananchi lifikie wastani wa shilingi 884,000 ifikapo mwaka 2015” Aliongeza Juma Ali Khatib.
Kutokakana na mafanikio hayo, vyama hivyo vimetoa shutuma kwamba kuna mkono wa kisiasa unaolenga kuvuruga mafanikio yaliyokwisha patikana na ndio maana kumekuwa na matukio vurugu katika siku za hivi karibuni.
“Hapa ndipo inapokuja hofu kwamba kuna mkono wa siasa kuvuruga mafanikio haya hasa kwa vile hayo ni matunfa yanayotokana na hali ya amani,utulivu na mshikamano wa Wazanzibari ambapo wananchi waliweza kuendelea na shughjuli zao za uzalishaji na biashara bila usumbufu,wageni waliendelea kufurika nchini na wawekezaji wameendelea kuwekeza” Alisema Katibu Mkuu wa TADEA.
Vyama hivyo, pia vimewakumbusha wananchi ulazima wa kuilinda amani iliyopo na kutokubali kutumiwa na watu wasioitakia mema Zanzibar.
Katika hatua nyengine katika tamko la vyama hivyo  vimeituhumu Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam kwenda kinyume na masharti ya uanzishwaji wake na kuiomba Serikali kuangalia usajili wa Jumuiya hiyo.
Aidha, imewasihi Mashekh na Maulamaa wote wasitumi dini kama ngao ya kuwapotosha wananchi na kusababisha vurugu ndani ya nchi. “Tunawaomba wananchi walioanza harakati za kutaka kuigawa nchi kwa misingi ya uzawa kuachana na kasumba hizo kwani hazina  hatma njema miongoni mwa Wazanzibari” Limesisitiza tamko la vyama hivyo.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA