WAKULIMA WA TUMBAKU WAHIMIZWA KUSHIRIKI SENSA
Wakulima
wa Tumbaku wilayani Singida, wamekumbushwa kujitokeza kushiriki sensa
ya watu na makazi itakayofanyika Agost 26, mwaka huu.
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Fatma Toufiq, alipozungumza na wakulima pamoja na wakazi wa kijiji cha Mitundu.
Alisema
sensa hiyo inalenga kupata idadi ya watu waliopo ili kufahamu shughuli
za kiuchumi, kielimu na kiundombinu kwa lengo la kupanga maendeleo ya
nchi na watu wake.
“Sensa
ni muhimu na inawezesha kufahamu idadi ya watu katika maeneo yetu ili
kufahamu shughuli zao za kiuchumi, kielimu na miundombinu ili tupannge
maendeleo” alisema Toufiq.
Toufiq
alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi wilayani Singida, kujitokeza kwa
wingi pindi muda utakapofika ili kila mmoja ahesabiwe kwa faida yake na
taifa.
Mwenyekiti
wa chama kikuu cha ushirika cha Wakulima wa tumbaku (CETCU), kanda ya
kati Yassin Dagaki, akitoa taarifa ya maendeleo ya kilimo cha zao hilo ,
alisema msimu wa mwaka 2009/2010 uzalishaji uliongezeka kwa wastani wa
asilimia 34.