KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA MASHIRIKA YA UMMA YASIFU UTUNZAJI WA KINU CHA NMC IRINGA

Mwenyekiti wa kamati ya bunge hesabu za mashirika ya umma Zitto Kabwe na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM ) Lediana Mng'ong'o ambaye ni mjumbe wa bodi wakipata maelezo ya kinu cha NMC Iringa
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga (CUF) Amina Mwidau akiwa na mbunge wa Mwimbala Mhe.Lugolla
 
 Mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe (kulia) akipata maelezo ya mitambo mbali mbali katika kinu hicho

 Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo ya kinu hicho
Hiki ndicho kinu cha NMC Iringa kilivyotunzwa vema
Mjumbe wa kamati hiyo na mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga (CUF) Amina Mwidau (kulia) akiwa na mbunge wa viti malum mkoa wa Iringa Lediana Mng'ong'o ,RAS Iringa Getrude Mpaka , na mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma imetembelea mali za kilichokuwa Kinu cha Kusaga na Kuhifadhi Chakula (NMC) tawi la Iringa na kujiridhisha kwamba ipo haja ya kumbukumbu zake zote kupitiwa upya huku ikisifu utunzaji wa kinu hicho na kuahidi kuwaita bungeni viongozi wa NMC ili kuwapongeza kwa uzalendo wao

Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka mnong’ong’o kwamba sehemu ya kinu hicho inafanya kazi kinyemela huku mapato yake yakiwa hayapelekwi hazina.

Pamoja na tetesi hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo na badala yake yeye pamoja na wajumbe wa kamati hiyo na wenyeji wao walijifungia kwa muda ndani ya ofisi, huku wakiwazuia waandishi kusikia kilichokuwa kikijadiliwa.

Hata hivyo wakati akitembelea kinu hicho na kuingia katika moja ya majengo yaliyokuwa yanatumika kwa ajili ya kufunganishia unga kwenye mifuko ya ujazo tofauti, Kabwe alishangaa kuona lundo la mifuko mipya kwa ajili ya kufungashia unga uliokuwa ukizalishwa katika kinu hicho.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo alisema kwa sauti ya kunong’ona kwamba kuna haja ya kujua mapato yaliyokuwa yakikusanywa tangu kinu hicho kisimamishe uzalishaji wake rasmi yanakwenda wapi.

Tangu kinu hicho kistishe shughuli zake za uzalishaji kwa zaidi ya miaka kumi, kumekuwepo na shughuli zingine za watu binafsi zikiendelea hapo, hata hivyo taarifa ya kilichokusanywa na kinachoendelea kukusanywa hazikuwa bayana.

Pamoja na ahadi ya kamati hiyo, Kabwe alitoa mwaliko kwa wafanyakazi kumi wa iliyokuwa NMC kutembelea bungeni wakati kamati hiyo itakapokuwa ikiwasilisha taarifa yake kwa kile alichodai wameisadia serikali kulinda mali za kinu hicho tangu kisimame uzalishaji.

“Wasingekuwa waaminifu, hii mitambo iliyomo katika kinu hiki na mali zake nyingine nyingi zingepotea au kuhujumiwa, tunawapongeza na nawalika rasmi bungeni,” alisema.

Akitoa ahadi hiyo, Kabwe pia alisema mali na mipaka ya kinu hicho itahakikiwa ili uhalali wake uwe bayana.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA